Recent Posts

PropellerAds

Thursday, June 20, 2019

MAMBO MUHIMU KUTOKA KITABU CHA WARUMI



Utangulizi:

Warumi 1: 1 inatambua mwandishi wa kitabu cha Warumi kama mtume Paulo. Warumi 16:22 inaonyesha kwamba Paulo alitumia mtu mmoja jina Tertio kunakili maneno yake. kitabu cha Warumi huenda kiliandikwa 56-58 BK.

 Kama nyaraka zote za Paulo kwa makanisa, kusudi lake la kuandika lilikuwa kutangaza utukufu wa Bwana Yesu Kristo kwa kufundisha kanuni za mafundisho na kuadilisha na kuwatia moyo waumini ambao wangepokea barua yake. Wale ambao Paulo alijali sana ni wale ambao barua hii iliandikiwa-wale walio katika Roma ambao  "walipendwa na Mungu na walioitwa kuwa watakatifu" (Warumi 1: 7).
 Kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ni raia wa Roma, alikuwa na mapenzi ya kipekee kwa wale waliokuwa katika mkutano wa waumini katika Roma. Tangu hadi hapa hakuwa ametembelea kanisa katika Rumi, barua hii pia ilitumika kama utangulizi wake kwao.
Madhumuni makuu ya kuandika waraka huu kwa Warumi ilikua:-
v       Maombi na Shukrani
#
Waraka wa Mtume Paulo unabeba ujumbe maalumu kwa ndugu wote waliokua katika roma. Warumi 1:8 kwanza kabisa, Namshukuru Mungu wangu kwa Njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote,kwa sababu Imani Yenu inatangazwa duniani kote. Kwa maana Munguninaemtumikia kwa Moyo Wangu wote katika kuhubiri Injili ya Mwanae, ni shahidi wangu njisi ninavyowakumbuka.  Ujumbe wa Mtume Paulo unasisitiza Zaidi katika Maombi na shukrani kwa watu wote na kwa ajili ya Imani Ya Yesu kristo Alieshaidi mwaminifu katika utendaji kazi wa Injili na Imani Ulimwenguni Mwote.

Ghadhabu Ya Mungu Kwa Wanadamu
Ghadhabu ya Mungu Imedhirishwa kutoka Mbinguni dhidi ya Uasi wote na uovu wa wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao, kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni Dhahiri kwao, kwa sababu Mungu aliweka wazi kwao. Mtume Paulo anaeleza wazi wazi  kuhusu Hukumu ya Mungu kwa Wanadamu na anaendelea kueleza kwa kina Zaidi kuhusu Umilele na asili yake ya Uungu, Umeonekana Kwa Macho waziwazi ili wanadmu asiwe na udhuru. Warumi 1:21”Kwa Maana ingawa walimjua Mungu,hawakumtukuza yeye kama Ndiye Mungu wala hawakumshukuru,bali  bali fikra zao zimekuwa batili na mioyo yao ya Ujinga ikatiwa giza” ingawa wakjidai  kuwa wenye hekima wakawa wajinga.

Hukumu Ya Mungu.
Katika hukumu ya  Mungu Mtume Paulo anandelea kueleza  ya kua  hatauna udhuru wo wote wewe mtu uwaye yote,,utoaye hukumu kwa mwingine ,kwa maana katika jambo lo lote unalowahukumu wengine unajihukumu wewe mwenyewe kwa sababu wewe unayehukumu unafanya mambo hayo. basi tunajua hukumu ya Mungu dhidi ya wale wafanyao mambo kama hayo ni ya kweli.
Uaminifu wa Mungu.

Kuna faida kubwa kwa kila namna,kwanza kabisa, Wayahudi wamekabidhiwa lile neon halisi la Mungu. Ingekuwaje kama wengine hawakuwa na Imani  je? Kutokuamini kwao kungebatilisha Uaminifu wa Mungu? La hasha! Mungu na onekane mwenye haki na kila mwanadamu kuwa Mwongo, kama ilivyoandikwa katika warumi 3:4  “Ili uweze kujulikana kuwa na haki katika Maneno yako, nawe ukashinde katika hukumu”
Ikiwa uovu wetu unathibitisha haki ya Mungu waziwazi,tuseme nini basi? Je Mungu Kuileta ghadhabu yake juu yetu nikwamba yeye si mwenye haki?
Paulo alikuwa na msisimko juu ya kuwa na uwezo wa kuhudumu mwishowe katika kanisa hili, na kila mtu alikuwa anafahamu vizuri ukweli huo(Warumi 1: 8-15). Barua kwa Waroma iliandikwa kutoka Korintho tu kabla ya safari ya Paulo kwenda Yerusalemu kutoa sadaka zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya maskini huko. Alikuwa na lengo la kwenda Roma na kisha kwenye Hispania (Warumi 15:24), lakini mipango yake ilikatizwa wakati alikamatwa katika Yerusalemu. Hatimaye angeweza kwenda Roma kama mfungwa. Fibi, ambaye alikuwa mshirika wa kanisa la Kenkrea karibu na Korintho (Warumi 16: 1), huenda ndiye alipeleka barua Roma.

kitabu cha Warumi kimsingi ni kazi ya mafundisho na kinaweza kugawanywa katika sehemu nne: haki inayohitajika, 1: 18-3: 20; haki inayotolewa, 3: 21-8: 39; haki inayoonyeshwa, 9: 1-11: 36; haki inayotekelezwa, 12: 1-15: 13. Dhamira kuu ya barua hii ni dhahiri bila shaka-haki. Kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, Paulo kwanza analaani watu wote kwa dhambi zao. Anaonyesha matakwa yake ya kuhubiri ukweli wa Neno la Mungu kwa wale walio katika Roma. Ilikuwa tumaini lake kuwa na uhakika walikuwa wanakaa kwenye njia ya haki. Yeye kwa nguvu anasema kuwa haiionei haya Injili (Warumi 1:16), kwa sababu ni nguvu ambayo kila mtu anaokolewa kwayo.

kitabu cha Warumi kinatueleza kumhusu Mungu, yeye ni nani na amefanya nini. Kinatuambia kuhusu Yesu Kristo, nini kifo chake kilitimiza. Kinatuambia kuhusu sisi wenyewe, nini tulikuwa bila Kristo na sisi ni nani baada ya kuamini katika Kristo. Paulo anasema kwamba Mungu hakudai watu warekebishwe maisha yao kabla ya kuja kwa Kristo. Wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu.

Paulo anatumia watu kadhaa wa Agano la Kale na matukio kama mifano ya ukweli wa utukufu katika kitabu cha Warumi. Ibrahimu aliamini na haki ilihesabiwa kwake kwa imani yake, na si kwa matendo yake (Warumi 4: 1-5). Katika Warumi 4: 6-9, Paulo anarejelea kwa Daudi ambaye alirudia ukweli huo: "Heri waliosamehewa makosa yao, na waliositiriwa dhambi zao. Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi. "Paulo anatumia Adamu kuelezea Warumi mafundisho ya dhambi tulizorithi na anatumia hadithi ya Sarai na Isaka, mwana wa ahadi, ili kuonyesha kanuni za Wakristo kuwa wana wa ahadi ya neema kuu ya Mungu kupitia kwa Kristo. Katika sura 9-11, Paulo anakumbuka historia ya taifa la Israeli na kutangaza kwamba Mungu hatimaye hajakataa kabisa Israeli (Warumi 11: 11-12), lakini amewaruhusu kuwa na "mashaka" tu mpaka idadi kamili ya watu wa mataifa mengine wapate wokovu.

 kitabu cha Warumi kinaweka wazi kwamba hakuna kitu tunaweza kufanya ili kujiokoa wenyewe. Kila tendo "zuri" tumewahi fanya ni kama tambara chafu mbele ya Mungu. Hivyo ndivyo tulivyo wafu katika makosa na dhambi zetu ambapo kwamba ni tu neema na huruma ya Mungu inaweza kutuokoa. Mungu alionyesha neema hiyo na huruma kwa kumtuma Mwana wake, Yesu Kristo, ili afe msalabani kwa ajili yetu. Tunapogeuza maisha yetu kwa Kristo, hatudhibitiwa tena na asili yetu ya dhambi, ila tunadhibitiwa na Roho. Ikiwa tutakiri kwamba Yesu ni Bwana, na kuamini kwamba Yeye alifufuliwa kutoka kwa wafu, tumeokoka, na kuzaliwa upya. Tunahitaji kuishi maisha yetu yaliyotolewa kwa Mungu kama sadaka iliyo hai kwake. Ibada ya Mungu ambaye alituokoa inapaswa kuwa hitaji letu la juu. Labda utendaji bora wa Warumi unaweza ukawa kutekeleza Warumi 1:16 na kutoiionea haya Injili. Badala yake, hebu wote tuwe waaminifu katika kuitangaza
.