Recent Posts

PropellerAds

Monday, November 14, 2016

AINA 10 ZA BIASHARA (BUSINESS IDEAS) ZA KUFANYA SASA

0Je, Unahitaji Kufanya Biashara Na
Hujui Ni Biashara Ipi Ya Kufanya? Soma
Hapa Kujua Ni Biashara Ipi Ya Kuifanya
Sasa
Wapo watu ambao mara nyingi hujiuliza ni
biashara gani wafanye katika maisha yao
ambayo itaweza kuwaingizia pesa nyingi ya
kutosha. Ni wazo ambalo hutokea kutokana
na pengine kuona kila biashara
wanayoitazama kwa wakati huo kama
hailipi. Hali hiyo husababisha mkanganyiko
mkubwa wa mawazo ambao husababisha
wabaki njia panda.
Kama imeshawahi kukutokea hali kama hii
kwa namna moja au nyingine makala hi ni
muhimu sana kwako kuisoma. Kwa kusoma
makala hii inakuonyesha kwa uwazi orodha
za biashara ambazo unatakiwa uzifanye
ukiwa katika mazingira uliyopo. Karibu kila
biashara ipo hapo, kazi ni kwako kuchagua
mojawapo unayoipenda na kuifanya, acha
kulalamika tena kuwa huelewi nini cha
kufanya.
Twende kwa pamoja kuzijua biashara hizo
ambazo unauwezo wa kuzifanya na
kukufikisha kwenye mafanikio makubwa:-
1. Kutengeneza na kuuza chaki
Hii ni moja ya biashara nzuri unayoweza
kuifanya na soko lake liko juu. Unaweza
ukanunua mashine yako za kutengeneza
chaki na kisha ukaanza kuzisambaza
kwenye stationary au mashuleni. Uzuri wake
mashine hizi za kutengenezea chaki
gharama yake pia sio kubwa sana ni ya
kawaida tu ambayo hata wewe unaweza
kuimudu. Hii inaweza ikawa ni sehemu
mojawapo ya kuingizia kipato chako.
2. Kufungua duka la kuuza asali
Uzuri wa bidhaa hii muda mwingi soko lake
lipo juu. Ni biashara ambayo unaweza
ukaifanya kwa kuagizia asali kutoka kwa
wakulima kama nilivyo mimi na kisha
kuanza kuiuza moja kwa moja katika
vipimo vinavyotakiwa.
Kama huwezi kufungua duka hili unaweza
ukafanya mbadala wake ukaenda
kutengeneza mizinga wewe mwenyewe na
kuwafuga. Pia hii ni biashara ambayo ni
nzuri kwako kukuingizia kipato kikubwa kwa
urahisi.
3. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula
katika matamasha mbalimbali
Hapa siyo lazima uwe na Hotel au Mgahawa
ndiyo uanzishe biashara ya namna hii.
Kikubwa unahakikisha unakuwa makini na
sherehe katika eneo ulilopo. Kama ni
kuweka mawakala watakao kusaidia
kukujulisha kuwa eneo fulani kuna sherehe
ya aina fulani na siku fulani itakuwa nzuri
zaidi kwako kuchangamkia tenda hizo
mapema.
4. Kujenga nyumba za kulala wageni
Kama mtaji wako unaruhusu hii ni moja
kati ya biashara nzuri kuifanya. Ni
biashara ambayo hahitaji kukimbizana sana
ukishamaliza kujenga, zaidi unatakiwa
kuweka mfumo sahihi wa kusimamia na
kuanza kuingiza pesa. Na kwa bahati nzuri
kwa Tanzania yapo maeneo mengi ambayo
yanauhitaji mkubwa wa huduma hii. Ni
Biashara nzuri kuifanya hata kama umri
umeenda, kwa sababu haihitaji mkimbizano
mkubwa.
5. Kutengeneza matoroli/mikokoteni na
kuikodisha
Katika hili hapa unatakiwa kutengeneza kwa
idadi unayoitaka na unamwachia kijana
ambaye anaikodisha huku ukiendelea na
majukumu mengine. Unaweza ukaiona ni
biashara ndogo lakini fuatilia kwa
waliowekeza nguvu na mawazo yao hapo
wakwambie kile wanachokipata utashangaa.
6. Kuazisha huduma ya AIRTEL MONEY,
MPESA, TIGOPESA, EZYPESA
Hakuna ubishi hii ni moja ya huduma
ambayo imezagaa kila eneo na watu wengi
wanaihitaji. Kikubwa ni juhudi yako na
kuzingatia eneo uliloweka biashara yako liwe
hasa la mzunguko mkubwa zaidi
kukuwezesha kufanya biashara hii vizuri.
7. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/
sherehe
Pia unaweza ukajiingiza hapa na
kushughulika na kupamba tu maharusi.
Kama hujui sana ni kitu cha kujifunza pia,
kisha unachangamkia sherehe
zinazojitokeza mjini.
8. Kuanzisha kilimo cha kisasa
Wengi wanaposikia kilimo kichwa kinakataa.
Lakini ikiwa utawekeza kwenye kilimo cha
kisasa na cha kitaalamu ambacho
unategemea kumwagilia zaidi, uwe na
uhakika unatoka. Yapo mazao mengi
unaweza ukalima lakini mojawapo ni
kitunguu. Inaweza ikawa ni njia rahisi ya
kufikia mafanikio yako kuliko unavyofikiri.
9. Mashine za kusaga na kukoboa nafaka
Pia unaweza ukajitengenezea kipato chako
na kuwa kikubwa na cha uhakika kwa
kufunga mashine hizi. Kila siku watu
wanahitaji kula hivyo ukifunga mashine hizi
ni rahisi sana kupata wateja wa kuwauzia
unga na kupata faida. Na uzuri mahindi ya
kusaga yanapatikana maeneo mengi kwa
wingi kama kule Kibaigwa (Dodoma), Gairo
(Morogoro), Kiteto(Manyara) na maeneo
mengine mengi kama Iringa na mbeya.
10. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
Kitu unachotakiwa hapa ni kununua kiwanja
na kukigeuza kuwa yadi ambapo magari
yanakuwa yanapaki iwe kwa kulala au kwa
muda. Kila gari linalokuwa linapaki linakuwa
linatozwa kiasi fulani cha pesa ambacho
kinakuwa ndiyo hiyo huduma unayoitoa.
In God we trust in money we audit.