Na:
Saphira nyemenohi
Bwana Yesu asifiwe. Habari za jioni wapendwa, napenda kuwasalimu kwa Jina lipitalo majina yote. Bwana Yesu asifiwe. Somo la Leo linahusu unyenyekevu Yoh.13:12-15 Bwana Yesu anawatawaza miguu wanafunzi wake. Kwa hali ya kawaida alikuwa ni vigumu ndio sababu Petro aligoma. Alifikiri kukaa karibu naYesu alistahili heshima na kutumikiwa na si kutumika.Mpaka sasa kanisa la Mungu linataabika kwa kwa sababu ya viongozi mfano wa Petro hawako tayari kuwaosha wafuasi wao miguu. Kila kukicha wanataka utukufu wanadai heshima. Hawako tayari kushuka na kujifunza kwa Yesu.Kanisa la Mungu linahitaji kupona. Yesu akasema jitieni nira yangu mjifunze kwangu maana mimi mpole na mnyenyekevu wa moyo.Wewe unayejiita mkristo kwanini hutaki kuishi maisha ya Kristo? Kama unakosolewa unahama kanisa, peleleza ukristo wako!kama unahitaji heshima na utukufu kuliko Mwana wa Mungu aliye juu, peleleza ukristo wako.Wafilipi 2:5-10Mbarikiwe wana wa Mungu.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha
kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini
ke...
5 weeks ago