Recent Posts

PropellerAds

Friday, August 31, 2018

heshima kuu kutoka kwa Mungu mwenyewe

Image result for cross

Ufunuo 5;9-10
“Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.”
Kwa Neema yake Mungu hapo tulipokuwa wafu kwasababu ya dhambi alitufufua pamoja na Kristo akisha kutusamehe dhambi zetu kwa damu yake,na kwa Neema yake kuu akatufanya Ufalme na Makuhani kwa Mungu.Nafasi ya Ukuhani ni nafasi ambayo Mungu mwenyewe aliianzisha,kwa ajili ya kutengeneza mazingizingira ya yeye kukaa katika ya wanadamu.Nafasi ya kikuhani ni nafasi ambayo kila mtu aliyempokea Yesu Kristo anapewa.Agano la kale Mungu alichagua Uzao wa Haruni pekee yake kusimama mbele zake katika nafasi ya Ukuhani lakini katika Agano bora (Agano jipya) kila aliyempokea Yesu amefanyika Kuhani mbele za Bwana,pasipo kujali kigezo cha Kabila,lugha,jamaa na taifa.Mungu ni mwaminifu sana na analiheshimu sana Neno lake,Yeye mwenyewe ndiye aliyeanzisha Kiti cha Ukuhani,hivyo mtu yoyote anaposema na Mungu kutokea kwenye Nafasi ya Ukuhani,Mungu anaheshima sana maneno ya mtu huyo na maombi ya mtu huyo anayeomba kutoka kwenye kiti cha Ukuhani.Heshima hii sio kwasababu ya mtu bali ni kwasababu ya Nafasi ya Kikuhani ambayo anayeomba amesimama katika hiyo.
Waebrania 5; 4-6
“Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki”
Neno hili hapo juu linaonyesha wazi kuwa hakuna mtu awezaye kujifanya kuhani au kujipa Heshima hii ya Kikuhani mbele za Mungu. Heshima hii Hutoka kwa Mungu mwenyewe.Haruni alipewa Kiti na Mungu mwenyewe na Yesu pia.
“Naye Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
Ondokeni kati ya mkutano, ili niwaangamize mara moja. Wao wakapomoka kifudifudi.
Musa akamwambia Haruni, Haya, shika chetezo chako, ukatie moto ndani yake, moto wa madhabahuni, kisha utie na uvumba juu ya moto, ukakichukue haraka, wende nacho katika huo mkutano, ukawafanyie upatanisho; kwa kuwa ghadhabu zimetoka kwa Bwana; hiyo tauni imeanza. Basi Haruni akakishika chetezo kama Musa alivyonena, akapiga mbio akaenda katikati ya mkutano; na tazama, tauni ilikuwa imeanza kati ya watu; akatia uvumba juu ya moto na kufanya upatanisho kwa ajili ya hao watu.
Akasimama kati ya hao waliokufa na hao waliokuwa wakali hai; tauni ikazuiwa.”
Mungu ameweka Neno la Upatanisho ndani ya kila Mwamini,ametupa Nafasi ya Heshima sana.Sio kwamba Mungu alimweshimu sana Haruni hata akaghairi uharibifu aliokusudia juu la kusanyiko hapana,Mungu alimweshimu Kuhani Haruni aliyesimama kwenye nafasi ya Ukuhani.
Kutokujua nguvu uliyonayo kama Kuhani mbele za Bwana inakufanya usitumie nguvu hiyo,Kukosa Ufahamu kunamfanya Adui aendelee kuangamiza familia yako wakati Mungu amekupa Heshima ya Kusimama mbele zake kwa ajili ya Familia yako.
Unaweza kuwa Kuhani lakini ukawa huna Fikra na nia anayotakiwa kuwa nayo kuhani.Hiyo ndiyo shida tuliyo nayo ndani ya Kanisa leo.Kama Kuhani wa Bwana yakupasa kufanya yafuatayo.
1.Vaa nia ya Upatanisho
Mungu alipoweka Ukuhani aliweka akiwa na Nia ya kuwa Kuhani atampatanisha Yeye na wanadamu wanapotenda dhambi.Hivyo Nia ya kuu ambayo kuhani anapaswa kuwa nayo ni Kupatanisha watu na Mungu,kupatanisha familia,ukoo,kabila, na hata  nchi na Mungu,kutengeneza mazingira ya amani kati ya Mungu na mwanadamu.
Israel walipotenda dhambi,walikuwa hawajamkosea Mungu tu,ila kosa lao lilikuwa Kumnung’unikia Musa na Haruni.Hivyo Musa angeweza kukaa kando na kuacha Mungu awaangamize Israel,ukizingatia walikuwa wamtendea uovu yeye na Haruni.Lakini Musa alikuwa ndani yake amevaa nia ya Upatanisho,nafsi za Israel zilikuwa na thamani mbele zake.Wakati Mungu anawaadhibu yeye alimsemesha Haruni kufanya Upatanisho kwa ajili yao.
Eliya alikuwa Kuhani, aliteketeza roho 100 kwa moto kutoka mbinguni,akaokoa roho 50 za watu waliokuja mbele zake kwa staili moja.Nini kilifanya wale 100 wa kwanza wakaangamia na hawa 50 wakapona? Thamani ya roho hizi 50.Hawa ndugu 50 walimsemesha Eliya maneno yaliyofunua macho ya Eliya kutazama Thamani za roho zao mbele zake.
 12 Eliya akajibu, akamwambia, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza, yeye na hamsini wake.13 Tena akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako.14 Tazama, moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza wale akida wa hamsini wawili wa kwanza pamoja na hamsini wao; laiti sasa roho yangu na iwe na thamani machoni pako.
Ni hatari sana kwa Kuhani kuacha kufanya Upatanisho kwa ajili ya familia na kuanza kuhukumu familia yako.Familia ikipigwa huwezi kuwa na Amani na furaha,usifikiri nchi kuwa chini na hasira ya Mungu wewe utakaa salama,maandiko yanasema katika amani ya nchi ndiko utakapopata amani yako.

Vile Mungu mwenyewe ndiye anayempa Mtu Heshima hii ya Ukuhani inafanya nafasi hii Kikuhani kuwa ya Heshima sana mbele zake na Kumfanya Mungu kuheshimu sana Maombi yanayofanywa na mtu kama Kuhani juu ya familia,kanisa,ukoo,mkoa,nchi na dunia.
Heshima iliyopo kwenye KITI/NAFASI ya Kikuhani ni Heshima aliyotangulia Mungu kuiweka mwenyewe kwenye Kiti hicho alipoamua kukiweka Kisimame mbele zake.

Mtu anaposimama kwenye nafasi hii mbele za Mungu,anakuwa na Heshima ya kusikilizwa na Mungu kulingana na heshima ambayo Mungu mwenyewe aliiruhusu ikae juu ya kiti hiki mbele zake.Ni sawa na mtu akikuuliza swali hili,Hivi Mungu anaheshimu kwa kiwango gani nafasi ya Kuhani mbele zake..nawe ukamjibu kwa swali,,hivi Mungu aliweka heshima Kiasi gani kwenye Nafasi ya Ukuhani alipoamua Kuianzisha ili idumu mbele zake.? Heshima hii aliyoweka Mungu kwenye nafasi ya Kuhani ndio inayofanya Maombi yanayofanywa na  mtu yoyote anapokuwa amesimama kwenye nafasi hii yawe na Nguvu sana Mbele za Mungu.Kinachoyapa uzito mbele za Mungu maombi ya Kuhani ni Nafasi ya Kikuhani.
Mtu anaposimama mbele za Mungu kama Kuhani maombi yake yanakuwa na nguvu sana,pasipo kujali watu wamefanya uovu gani mbele za Mungu. Hesabu 16:44 Inaonyesha jinsi Mungu anavyoheshimu Nafasi ya Ukuhani na jinsi mtu anaposimama katika maombi kama Kuhani jinsi anavyoweza kuokoa nafsi za wengi hata kama ghadhabu ya Mungu ilikuwa imewaka juu yao.Israel walifanya jambo ambalo lilimkera sana Mungu na ghadhabu yake iliwaka na tauni ilikuwa inawaangamiza,Musa kwa kuijua nguvu ya Maombi ya Kuhani anamsihi Haruni kusimama mbele za Mungu kwaajili ya Israel ili Mungu awasamehe na Utaona jambo la ajabu sana Haruni aliposimama tu mbele za Mungu,Mungu alighairi hasira yake.Ni nafasi ya kikuhani pekee ambayo inaweza kumpa mtu nafasi ya kusimama mbele za Mungu mwenye ghadhabu na akaweza kuituliza ghadhabu hiyo na waliofanya uovu wakasamehewa.
Hesabu 16;44-48

Nia hii ndiyo wengi ambao ni makuhani hawana,wameokoka bado wanania ile ya utu wa kale ya Adui mwombee njaa.Huwezi ukaingia kwenye Ofisi ya Ukuhani ukiwa umevaa fikra za utu wa kale ukaweza kufanya kazi.Kiti cha Ukuhani hakipo kwaajili ya kutoa Hukumu,Nafasi ya Ukuhani ni kwaajili ya Kuombea rehema na kuwapatanisha watu na Mungu ni seme hivi kuhani yoyote anatakiwa aione thamani ndani ya kila nafsi ya mtu awe mwenye dhambi au hana dhambi kama vile Mungu anavyoiona thamani ya nafsi ya mtu mbele zake, hapo ndipo Kuhani atafanikiwa sana kwenye nafasi yake.
Musa aliona thamani kwa zile nafsi zilizokuwa zinaangamia,aliona thamani ya sura na mfano wa Mungu ndani ya wale watu ndio maana pamoja na kwamba walimtenda vibaya yeye aliweza kumsihii Haruni awaombee rehema.
2Wafalme 1;9-14.
9 Ndipo mfalme akatuma akida wa askari hamsini pamoja na hamsini wake, wamwendee Eliya. Akamwendea, na tazama, ameketi juu ya kilima. Akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka.10 Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka, ukamteketeza, yeye na hamsini wake.11 Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi.


Lord, Make Me a City on a Hill

Image result for me on top of mountain
How many pastors would be ordained if Jesus examined them?
Let me be more personal. Would Jesus have ordained me had he sat on my council of examiners? When I look back on my ordination exams, I wonder if I got off too easy.
It’s not that the brothers who examined me pitched me softballs. They grilled me with difficult and complex questions. They required me to give clear evidence that my theological understanding was sound. Some of their questions exposed my weaknesses.
But a text that sets me wondering is this:
“You are the light of the world. A city set on a hill cannot be hidden. Nor do people light a lamp and put it under a basket, but on a stand, and it gives light to all in the house. In the same way, let your light shine before others, so that they may see your good works and give glory to your Father who is in heaven.” (Matthew 5:14–16)
My examiners focused their questions almost exclusively on what I thought, which is, of course, very important for effective pastoring. But I don’t recall any pointed questions about how my intellectual theological understanding was producing the shining light of good works. I wasn’t required to give clear evidence that I was an actual doer of the word, and not just a well-informed hearer of the word (James 1:22).

If Jesus Had Examined Me

Now, my brother-examiners no doubt gave me the benefit of the doubt, assuming I would not have been recommended for ordination if my life wasn’t consistent with my words. But I think Jesus would have been harder on me, knowing me as he does, knowing how I can often talk a better game than I actually play.
I think he would have wanted me to demonstrate that my theological knowledge was in fact fueling the burning of my visible lamp. He might have asked me to describe how those in my neighborhood and relationships were tangibly receiving the benefit of my “light.” He might have required specific examples of the last time I was reviled and persecuted on his account (Matthew 5:11–12). He might have asked me when I was last aware of someone giving glory to my Father in heaven after seeing my good works.
Those questions would have been harder to answer. They would have exposed even more weaknesses, and in certain ways more important ones. My intellectual theological understanding from years and years of hearing the word would have only satisfied him to the degree that it was producing light through my doing of his word.

What Makes Us Light?

Jesus called himself the light of the world (John 8:12). What made him shine? Certainly it was his words (John 7:46). But it wasn’t only his words; it was also his works. He said, “The works that I do in my Father’s name bear witness about me” (John 10:25). Jesus’s works made who he was manifestly clear. His works shone, and they still shine.
Jesus called us the light of the world (Matthew 5:14). What makes us shine? It isn’t only our words, but our works. The works we do in Jesus’s name bear witness about us and about him. Our outward, observable, public works make who we are and whose we are manifestly clear. Just like Jesus, our works cause some to revile us and persecute us and utter all kinds of evil against us falsely on his account, and they cause others to give glory to our heavenly Father.

Shining People

“A city set on a hill cannot be hidden.” What kind of good works shine like that? It’s not a difficult question to answer. Ask yourself, What good works have other Christians done that stand out most in your memory? Who are the people you’ve known who have been most radiant with the light of Jesus?
The shining people haven’t necessarily been the smartest, or most articulate, or most talented, or had the most publicly influential platforms. They’ve been the most servant-hearted and sacrificially loving people. They’ve been the ones who find God’s steadfast love better than life (Psalm 63:3). They’ve consistently loved others in both word and deed (1 John 3:18). Their words and deeds have sometimes been tender and other times tough, depending on the need. Their actions have demonstrated that they truly consider others more significant than themselves (Philippians 2:3), and that they pursue others’ good more than others’ approval.
It’s not merely what the shining people do, but why they do it and how they do it that makes them literally remarkable — people talk about them. Some praise them, and others slander them. But it is their doing, not talking, that sets them apart. And we’ve found ourselves both drawn to them and unnerved by them, because the light of their humble, word-and-deed love has both warmed our chilled hearts and exposed our selfishness and pride.

Whatever It Takes

Would Jesus have ordained me? I trust that through the Spirit operating in my brother-examiners, he did. Seeing how Jesus patiently dealt with his original band, it’s clear he graciously chooses disciples like me whose intellectual knowledge initially outpaces their actions. But he expects that to change. He expects our works to grow into our words and bear shining witness to the reality and power of his words.
I’m grateful for the gift of theological equipping God has provided me. But these days I am asking him to press me harder than ever before, to examine me fully, to search me and try me and transform me so that I shine more with the light of Jesus through my works than I ever have. I don’t want to merely articulate glorious truth more accurately, but to incarnate it more fully, especially in the dark places of the world where it’s most needed. I want to live it more — to so love God and others for his sake that, whether I provoke persecution or the praise of God, my light is more clearly seen.
So, Lord, whatever it takes, make me a doer of your word so that my life shines like a city set on a hill and gives you glory, in Jesus’s name, Amen.

Maneno Yetu Yanafunua Nini?

Image result for your word
Linda Moyo Wako
“Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.”—MITHALI 4:23.
 Kwa nini tunahitaji kulinda moyo wetu?
MZEE mmoja kwenye kisiwa cha Karibea alitoka mahali alipokuwa amejikinga na kimbunga. Alipotazama uharibifu uliokuwa umetokea mahali hapo, aliona kwamba mti mmoja mkubwa sana ambao ulikuwa umesimama kwa miaka mingi karibu na lango lake la mbele, ulikuwa umetoweka. ‘Imekuwaje hivyo,’ akajiuliza, ‘hali miti midogo zaidi karibu na mti huo ilibaki?’ Alipotazama kisiki cha mti huo alijua sababu. Sehemu ya ndani ya mti huo ulioonekana kana kwamba hauwezi kutikiswa ilikuwa imeoza, na kimbunga kilikuwa kimefichua tu kuoza huko.
 Inasikitisha kama nini wakati mwabudu wa kweli anayeonekana kuwa Mkristo thabiti anaposhindwa na jaribu la imani! Kwa kufaa, Biblia inasema kwamba “mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake.” (Mwanzo 8:21) Hiyo yamaanisha kwamba hata mioyo iliyo mizuri inaweza kushawishiwa kufanya mabaya tusipoendelea kuwa macho. Kwa kuwa moyo usiokamilika wa mwanadamu unaweza kupotoshwa, tunahitaji kuchukua kwa uzito ushauri huu: “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo.” (Mithali 4:23) Tunaweza kulinda moyo wetu wa mfano jinsi gani?
Ni Muhimu Kujichunguza Mara kwa Mara
. (a) Ni maswali gani yanayoweza kuulizwa kuhusiana na moyo halisi? (b) Ni nini kitakachotusaidia kuchunguza moyo wetu wa mfano?
 Ukienda kumwona daktari ili kufanyiwa uchunguzi, yaelekea atachunguza moyo wako. Je, afya yako kwa ujumla, kutia ndani moyo wako, inaonyesha kwamba unapata chakula chenye lishe ya kutosha? Shinikizo la damu yako likoje? Je, moyo wako unapiga kwa njia ya kawaida? Je, unafanya mazoezi ya kutosha? Je, moyo wako unapata mkazo mwingi kupita kiasi?
Ikiwa moyo halisi unahitaji kuchunguzwa kwa ukawaida, vipi moyo wako wa mfano? Yehova huuchunguza. (1 Mambo ya Nyakati 29:17) Sisi pia tunapaswa kufanya vivyo hivyo. Jinsi gani? Kwa kuuliza maswali kama haya: Je, moyo wangu hupata chakula cha kiroho cha kutosha kupitia funzo la kibinafsi la ukawaida na kuhudhuria mikutano? (Zaburi 1:1, 2; Waebrania 10:24, 25) Je, moyo wangu unafikiria sana ujumbe wa Yehova kama “moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu,” ukinichochea kushiriki kazi ya kuhubiri na kufanya wanafunzi? (Yeremia 20:9; Mathayo 28:19, 20; Warumi 1:15, 16) Je, ninachochewa kujikakamua kisulubu kushiriki katika aina fulani ya huduma ya wakati wote inapowezekana? (Luka 13:24) Ninaruhusu moyo wangu wa mfano upatwe na mambo gani? Je, ninajitahidi kushirikiana na wengine ambao mioyo yao imeungamanishwa katika ibada ya kweli? (Mithali 13:20; 1 Wakorintho 15:33) Na tuwe wepesi kutambua udhaifu wowote ule katika moyo wetu na kuchukua hatua mara moja kurekebisha jambo hilo.
 Majaribu ya imani yanaweza kutimiza kusudi gani lenye manufaa?
Mara kwa mara sisi hupatwa na majaribu ya imani. Majaribu hayo yanatuwezesha kujua hali ya moyo wetu. Musa aliwaambia hivi Waisraeli waliokuwa karibu kuingia katika Bara Lililoahidiwa: ‘BWANA, Mungu wako alikuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.’ (Kumbukumbu la Torati 8:2) Tunapokabili hali tusizotarajia au majaribu, je, mara nyingi hatushangazwi na hisia na tamaa tunazoonyesha, au jinsi tunavyotenda? Majaribu ambayo Yehova huruhusu yatupate yanaweza kwa hakika kutusaidia kutambua kasoro zetu na hivyo kujirekebisha. (Yakobo 1:2-4) Na tusikose kamwe kutafakari na kusali kuhusu jinsi tutendavyo tunapopatwa na majaribu!
Maneno Yetu Yanafunua Nini?
 Mambo tunayopenda kuzungumzia yanaweza kufunua nini kuhusu moyo wetu?
Tunawezaje kujua mambo tuliyoweka hazina moyoni mwetu? Yesu alisema: “Mtu mwema hutokeza mema katika hazina njema ya moyo wake, lakini mtu mwovu hutokeza ambayo ni maovu katika hazina yake mbovu; kwa maana katika wingi wa moyo kinywa chake husema.” (Luka 6:45) Yale tunayozungumzia kwa ukawaida huonyesha vizuri yale ambayo moyo wetu umeazimia kufanya. Je, mara nyingi sisi huzungumza juu ya vitu vya kimwili na mafanikio ya kilimwengu? Au je, mara nyingi mazungumzo yetu hukazia mambo ya kiroho ? Badala ya kuzungumza kuhusu makosa ya wengine, je, tuna mwelekeo wa upendo wa kuyafunika? (Mithali 10:11, 12) Je, tuna mwelekeo wa kuzungumza sana kuhusu watu na shughuli zao maishani, huku tukizungumza machache kuhusu mambo ya kiroho na ya kiadili? Je, hiyo inaweza kuwa ishara kwamba tunajiingiza kupita kiasi katika mambo ya kibinafsi ya wengine?—1 Petro 4:15.
Ni somo gani kuhusu kulinda moyo wetu tuwezalo kujifunza kutokana na masimulizi kuhusu ndugu kumi wa Yosefu?
Fikiria yaliyotokea katika familia moja kubwa. Wana kumi wa Yakobo wenye umri mkubwa ‘hawakuweza kusema kwa amani’ na Yosefu, ndugu yao mdogo. Kwa nini? Walimwonea wivu kwa kuwa alipendwa sana na baba yao. Baadaye Yosefu alipopata ndoto kutoka kwa Mungu zilizoonyesha kwamba alikuwa na kibali cha Yehova, ndugu zake ‘walizidi kumchukia.’ 
(Mwanzo 37:4, 5, 11) Kwa ukatili, walimwuza ndugu yao awe mtumwa. Kisha ili kuficha dhambi yao, wakamhadaa baba yao afikiri kwamba Yosefu alikuwa ameuliwa na mnyama mwitu. Ndugu kumi wa Yosefu walishindwa kulinda moyo wao wakati huo. Ikiwa sisi ni wepesi kuchambua wengine, je, hiyo inaweza kuwa uthibitisho kwamba tuna husuda au wivu moyoni? Tunahitaji kuwa waangalifu kuchunguza kinachotoka vinywani mwetu na kung’oa haraka maelekeo yasiyofaa.
 Ni nini kitakachotusaidia kuchunguza moyo wetu tunaposema uongo?
Ingawa “haiwezekani Mungu kusema uongo,” wanadamu wasiokamilika wana maelekeo ya kusema uongo. (Waebrania 6:18) “Wanadamu wote ni waongo,” akasikitika mtunga-zaburi. (Zaburi 116:11) Hata mtume Petro alisema uwongo mara tatu alipomkana Yesu. (Mathayo 26:69-75) Ni wazi kwamba tunapaswa kuwa waangalifu kuepuka kusema uongo, kwa kuwa Yehova huchukia ‘ulimi wa uongo.’ (Mithali 6:16-19) Iwapo tumesema uongo, lingekuwa jambo la hekima kuchunguza tujue ni nini kilichotufanya tuseme uongo huo. Je, tulifanya hivyo kwa sababu ya kumwogopa mwanadamu? Je, tuliogopa kuadhibiwa? Labda ni kwa sababu tuliona aibu au ni kwa sababu ya ubinafsi tu? Hata sababu iwe nini, inafaa kama nini kutafakari jambo hilo, kukubali kosa letu kwa unyenyekevu, kumwomba Yehova msamaha, na kutafuta msaada wake ili kushinda udhaifu huo! Huenda ikafaa zaidi kutafuta msaada wa “wanaume wazee wa kutaniko.”—Yakobo 5:14.
Sala zetu zinaweza kufunua nini kuhusu moyo wetu?
Yehova alisema hivi akijibu ombi la Mfalme Solomoni mchanga la kuwa na hekima na ujuzi: “Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu . . . , basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu.”
 (2 Mambo ya Nyakati 1:11, 12) Yehova alijua yaliyokuwamo moyoni mwa Solomoni kutokana na yale aliyoomba na yale ambayo hakuomba. Mazungumzo yetu na Mungu yanafunua nini kuhusu moyo wetu? Je, sala zetu zinaonyesha kwamba tunataka sana kupata ujuzi, hekima, na ufahamu? 
(Mithali 2:1-6; Mathayo 5:3) Je, masilahi ya Ufalme yamo moyoni mwetu? (Mathayo 6:9, 10) Ikiwa tunasali bila kufikiri au kidesturi tu, jambo hilo laweza kudhihirisha uhitaji wa kuchukua wakati wa kutafakari matendo ya Yehova.
 (Zaburi 103:2) Wakristo wote wanapaswa kuwa macho kutambua sala zao zinafunua nini.
Matendo Yetu Yanafunua Nini?
 (a) Uzinzi na uasherati huanzia wapi? (b) Ni nini kitakachotusaidia ‘tusifanye uzinzi moyoni’?
 Imesemekana kwamba muungwana ni kitendo. Matendo yetu hufunua mengi sana kuhusu hisia zetu za ndani. Kwa mfano, kuhusiana na maadili, kulinda moyo huhusisha mengi zaidi ya kuepuka tu tendo la uasherati au uzinzi. Yesu alisema hivi kwenye Mahubiri yake ya Mlimani: “Lakini mimi nawaambia: ye yote atakayemwangalia mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” (Mathayo 5:28) Tunaweza kuepuka kwa njia gani kufanya uzinzi hata katika moyo wetu?
Mzee wa ukoo AYubu aliwawekea kielelezo wanaume na wanawake Wakristo waliofunga ndoa. Hapana shaka kwamba Yobu alikutana na wanawake wachanga katika shughuli zake za kila siku, na hata kuwasaidia kwa fadhili walipohitaji msaada. Lakini Yobu, mtu mwenye uaminifu-maadili, hakujiruhusu avutiwe nao kimapenzi. Kwa nini? Kwa sababu alikuwa ameazimia kabisa kutowatazama wanawake kwa kuwatamani. “Nilifanya agano na macho yangu,” akasema. “Basi nawezaje kumwangalia msichana?” 
(Ayubu 31:1) Na tufanye agano kama hilo na macho yetu na kulinda moyo wetu.
 Unaweza kutumia andiko la Luka 16:10 jinsi gani kuhusiana na kulinda moyo wako?
 Mwana wa Mungu alisema: “Mtu aliye mwaminifu katika lililo dogo zaidi sana ni mwaminifu katika lililo kubwa pia, na mtu asiye mwaminifu katika lililo dogo zaidi sana ni asiye mwaminifu katika lililo kubwa pia.” 
(Luka 16:10) Naam, tunahitaji kuchunguza mwenendo wetu kuhusiana na mambo yanayoonekana kuwa madogo ambayo sisi hufanya kila siku, hata yale ambayo sisi hufanya nyumbani mwetu.
 (Zaburi 101:2) Tunapoketi nyumbani mwetu tukitazama televisheni, au kutumia Internet, je tunakuwa waangalifu kufuata ushauri huu wa Kimaandiko: “Acheni uasherati na ukosefu wa usafi wa kila namna au pupa hata visitajwe hata miongoni mwenu, kama vile ifaavyo watu watakatifu; wala mwenendo wa aibu wala maongezi ya kipumbavu wala kufanya mzaha wenye aibu, mambo yasiyofaa”? (Waefeso 5:3, 4) Namna gani jeuri tunayoweza kutazama kwenye televisheni au katika michezo ya video? “Yehova huchunguza mwadilifu na mwovu pia, na nafsi Yake humchukia yeyote apendaye jeuri,” akasema mtunga-zaburi.—Zaburi 11:5.
Tunahitaji kuwa na tahadhari gani tunapotafakari yale yatokayo moyoni mwetu?
Yeremia alionya: “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha.” (Yeremia 17:9) Udanganyifu huo wa moyo unaweza kuonekana tunapojitetea au kupunguza uzito wa makosa yetu, kupuuza kasoro zetu mbaya, au kutia chumvi mafanikio yetu. Moyo wenye ugonjwa wa kufisha unaweza pia kuwa mnafiki—useme mambo yenye kupendeza, na kutenda kinyume. (Zaburi 12:2; Mithali 23:7) Ni muhimu kama nini kuwa wanyofu tunapochunguza yale yatokayo moyoni mwetu!
Je, Jicho Letu Ni Sahili?
(a) Jicho “sahili” ni nini? (b) Kudumisha jicho letu likiwa sahili hutusaidia jinsi gani kulinda moyo?
14 Yesu alisema, “Taa ya mwili ni jicho.” Kisha akaongeza: “Basi, ikiwa jicho lako ni sahili, mwili wako wote utakuwa mwangavu.” (Mathayo 6:22) Jicho lililo sahili hukazia uangalifu mradi au kusudi moja bila kukengeushwa. Naam, jicho letu lapaswa kukazia uangalifu “kutafuta kwanza ufalme na uadilifu [wa Mungu].” (Mathayo 6:33) Ni nini kiwezacho kuupata moyo wetu wa mfano ikiwa jicho letu si sahili?
 Fikiria hali ya kupata riziki. Kuiruzuku familia yako ni takwa la Kikristo. (1 Timotheo 5:8) Lakini namna gani iwapo tunashawishiwa na tamaa ya kuwa na vitu vya kisasa, vilivyo bora zaidi, na vinavyopendwa zaidi, kama vile chakula, mavazi, makao, na vitu vinginevyo? Je, kweli hali hiyo haitatawala moyo na akili, ikifanya ibada yetu iwe ya moyo nusu nusu? (Zaburi 119:113; Warumi 16:18) Mbona tujishughulishe sana na mahitaji ya kimwili hivi kwamba katika maisha yetu tunafikiria tu familia, biashara, na vitu vya kimwili? Kumbuka ushauri huu uliopuliziwa: “Kazieni uangalifu kwa nyinyi wenyewe kwamba mioyo yenu isiwe kamwe yenye kulemewa na kula kupita kiasi na kunywa sana na mahangaiko ya maisha, na kwa ghafula siku hiyo iwe juu yenu mara hiyo kama mtego. Kwa maana itakuja juu ya wote wale wanaokaa juu ya uso wa dunia yote.” —Luka 21:34, 35.
 Yesu alitoa ushauri gani kuhusu jicho, na kwa nini?
Jicho ni kiungo muhimu sana kwa kuwa linawasilisha habari katika akili na moyo. Mambo linalotazama yanaweza kuathiri sana mawazo, hisia, na matendo yetu. Kwa kutumia lugha ya mfano, Yesu alitaja jinsi macho yalivyo kishawishi chenye nguvu: “Ikiwa, sasa, jicho lako hilo la kuume linakufanya ukwazike, ling’oe kabisa na ulitupilie mbali nawe. Kwa maana ni manufaa zaidi kwako kimoja cha viungo vyako kipotee kwako kuliko mwili wako wote kutupwa katika jehanamu.” (Mathayo 5:29) Jicho lapaswa kuzuiwa lisitazame mambo yasiyofaa. Kwa mfano, halipaswi kuruhusiwa kutazama habari ambayo imekusudiwa kusisimua au kuamsha hamu na tamaa zisizofaa.
 Kufuata andiko la Wakolosai 3:5 hutusaidia jinsi gani kulinda moyo?
Mbali na macho, kuna njia nyinginezo za kupata habari. Uwezo wa kugusa na kusikia hutumika pia, na tunahitaji kuchukua hatua za tahadhari kuhusiana na viungo vingine vinavyohusika. Mtume Paulo alishauri: “Fisheni viungo vya mwili wenu vilivyo juu ya dunia kwa habari ya uasherati, ukosefu wa usafi, hamu ya ngono, tamaa yenye kuumiza, na tamaa, ambako ni ibada ya sanamu.”Wakolosai 3:5.
Twapaswa kuchukua hatua gani kuhusiana na mawazo yasiyofaa?
Tamaa isiyofaa yaweza kutoka katika sehemu ya ndani kabisa ya akili yetu. Kwa kawaida, kuwaza sana juu ya tamaa isiyofaa hufanya iongezeke na kuathiri moyo. “Kisha tamaa, wakati imetungika mimba, huzaa dhambi.” (Yakobo 1:14, 15) Wengi hukiri kwamba hivyo ndivyo mara nyingi mtu huanza kupiga punyeto. Ni muhimu kama nini kuendelea kujaza akili yetu mambo ya kiroho! (Wafilipi 4:8) Wazo lisilofaa likiingia akilini mwetu, twapaswa kujitahidi kuliondoa.
‘Tumikia Mungu kwa Moyo Wako Wote’
 Tunaweza kufanikiwaje kumtumikia Yehova kwa moyo wote?
Alipokuwa mzee, Mfalme Daudi alimwambia hivi mwanawe: “Solomoni mwanangu, umjue Mungu wa baba yako, na umtumikie kwa moyo wako wote na kwa nia thabiti; yeye Mwenyezi-Mungu huchunguza mioyo na anafahamu mipango na fikira za binadamu.” (1 Mambo ya Nyakati 28:9,) Solomoni mwenyewe alisali apewe “moyo mtiifu.” (1 Wafalme 3:9, ) Hata hivyo, haikuwa rahisi kwake kudumisha moyo huo katika maisha yake yote.
 Ili tufanikiwe kumtumikia Yehova kwa moyo wote, ni lazima tujipatie moyo unaompendeza na kuulinda pia. Ili kufanya hivyo, ni lazima tuviweke moyoni vikumbusho vya Neno la Mungu—‘kuvihifadhi ndani ya moyo.’ (Mithali 4:20-22) Pia twapaswa kuwa na mazoea ya kuchunguza moyo wetu, na kutafakari kwa sala yale yanayofichuliwa na maneno na matendo yetu. Kutafakari huko hakutakuwa na matokeo tusipotafuta kwa bidii msaada wa Yehova ili kusahihisha udhaifu wowote tunaotambua. Ni muhimu kama nini kuwa waangalifu sana kuhusiana na yale tunayoingiza moyoni mwetu kupitia hisi zetu! Kwa kufanya hivyo, tunahakikishiwa kwamba “amani ya Mungu izidiyo fikira yote kwa ubora italinda mioyo [yetu] na nguvu [zetu] za akili kwa njia ya Kristo Yesu.” (Wafilipi 4:6, 7) Naam, na tuazimie kulinda moyo wetu kuliko yote tuyalindayo na kumtumikia Yehova kwa moyo wote.
Je, Unakumbuka?
• Kwa nini ni muhimu kulinda moyo?
• Kuchanganua yale tunayosema hutusaidia jinsi gani kulinda moyo wetu?
• Kwa nini tudumishe jicho letu likiwa “sahili”?
Tafadhali tutumie barua pepe kwa Ushauri na Maombi Email: jagaji61@gmail.com