Kati ya viumbe vyote ambavyo Mungu ameviumba hakuna kiumbe hata kimoja chenye thamani
kumshinda Mwanadamu.
Mwanzo1:1
Hapo mwazo Mungu
aliziumba mbingu na nchi,
Mwanzo 1:26
Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale
samaki wa Baharini.na ndege wa again,na wanyama na nchi yote pia na kila chenye
kutambaa kitaambacho juu ya nchi.
Mawazo
ya malaika,
Zaburi
8:4-6.
“Mtu
ni kitu gani hata umkumbuke ? Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo
punde kuliko Mungu Umemvika taji ya Utukufu na Heshima,”
Waebrania
2:5
“Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao
tunaounena ”
Malalamiko sita (6) ya Malaika
1.kwa nini umkumbuke Mwanadamu
Mwanadamu alipewa nafasi ya kufikiriwa na Mungu kila
mahali.
2.Mwanadamu ni nani hata umjali(kwa nini Mungu Umjali
Mwanadamu)
3.Umemfanya kuwa karibu na Mungu(kwa nini umemfanya
Mwanadamu kuwa rafiki yako)
4.Umempa fahari na Heshimu (Utukufu na Heshima)
5.Umemtawaza juu ya kazi zako zote(Madaraka yote juu ya
yote aliyotenda Mungu.)
6.Umetia vitu vyote chini ya mamlaka yake chini ya miguu
yake. Waebrania 2:8
Hivyo basi tunaona mtekaji mkuu wa haki ya mwanadamu ni
malaika Muasi. Huyu aliasi akiwa mbinguni na ndio mtoa hoja juu ya binadamu.
Sifa za huyu malaika muasi ni:-
Malaika mtiwa mafuta.
Mwili wake ulifunikwa kwa vito.
Kerubi afunikae Ezekiel 28:14.
Aliumbiwa mziki (Lucifer)
Alipotaka kufanya mageuzi ya kutaka kuchukua nafasi ya
Mungu, Mungu alimshusha Duniani na majina yake yalifuatanana na kazi zake .
Majina hayo ni:-
1.shetani.
Mshindani wa Mungu.
ufunuo 12:7
Kulikuwa na vita mbinguni;Mikaeli na Malaika zake
wakapigana na Yule joka, Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
nao hawakushinda wala akatupwa yule mkubwa ,nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na
shetani, audanganyae ulimwengu wote;akatupwa hata chini na malaika zake
wakatupwa pamoja nae.
2,Ibilisi
Mshitaki wa uongo, mdanganyifu.
1
Mambo ya nyakati 21:3
Mbona awe sababu ya hatia ya Israel?
Mathayo 4:10
“ndipo yesu alipomwambia Nenda zako shetani kwa maana
imeandikwa,msujudie Bwana Mungu wako umwabudu yeye peke yake”
3.Beelzebuli.
Mungu wa mafanikio ya haraka haraka.Mungu wa mbolea.
Shetani ni adui halali na mpinzani wa haki zote ambazo Mungu aliwandalia
wanadamu.
Shetani huwa hadaa wanadamu kwa udanganyifu wa mali na
maisha mazuri ya kitambo lakini mwisho wake ni mauti na majuto makuu.
Mathayo 12:24
4.joka
Kulikuwa na vita mbinguni;Mikaeli na Malaika zake wakapigana na Yule joka, Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda wala akatupwa yule mkubwa ,nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na shetani, audanganyae ulimwengu wote;akatupwa hata chini na malaika zake wakatupwa pamoja nae.
ufunuo 12:7