Recent Posts

PropellerAds

Friday, August 5, 2016

Wakonta Kapunda, msichana anayeandika kwa ulimi

Kutana na Wakonta Kapunda, msichana wa miaka 25
kutoka Tanzania ambaye alipata ajali siku ya kuhitimu
sekondari.
Baada ya matibabu na kulazwa hospitalini kwa miezi,
miaka minne baadaye amepooza mwili mzima
isipokuwa shingoni na kichwani.
Lakini sasa amepata matumaini baada ya kujifundisha
namna ya kuendeleleza ndoto yake ya uandishi wa
filamu kutumia ulimi wake, ambao ndio pia anaotumia
kujibia simu na kuandika ujumbe mfupi wa simu ya
mkononi.
BBC ilikutana naye katika mashindano ya uandishi
aliyoshiriki kisiwani Zanzibar.

1 0F THE BEST LYRICS IN GOSPEL IN TANZANIA. NALILIA UZIMA LYRICS BY AIC SHINYANGA CHOIR

Nalilia uzima, kutoka kwa Bwana
Ili nikaishi naye katika uzima,
Uzima wa milele
Shetani anaulilia uzima wangu mimi,
Anisukumia mawimbi ya kila haina
Na mateso makali X2
Anitisha ili nisimuone Bwana
Lakini nimejitoa , Kwa bwana kwa moyo wangu
wote
Liwalo na liwe
Asukuma silaha za maangamizi, eti anisambaze,
bwana wangu kaniwekea walinzi,
Najivuna kwa bwana. X2
Shetani hana nafasi,
kwangu mimi moyoni mwangu
yesu atawala , uzima wangu, niliopewa na bwana
X2
Uzima wangu ni wa dhamani,
gharama yake kifo chake yesu,
dhamani yake ni damu yake,
bwana yesu msalabani. X2
Yesu ni nuru moyoni mwangu,
yesu ni uzima wangu,
yesu ni ushindi , namtegemea yeye katika kila
jambo,
siogopi kitu , bwana ni ngome yangu,
sibabaishwi kitu. X2
Nalilia uzima, kutoka kwa Bwana
Ili nikaishi naye katika uzima,
Uzima wa milele
Shetani anaulilia uzima wangu mimi,
Anisukumia mawimbi ya kila haina
Na mateso makali X2
yesu, u-natosha, u-natosha, wewe peke yako
shetani, u-shindwe, u-shindwe, kwa jina la yesu
X2
Anitisha ili nisimuone Bwana
Lakini nimejitoa , Kwa bwana kwa moyo wangu
wote
Liwalo na liwe
Asukuma silaha za maangamizi, eti anisambaze,
bwana wangu kaniwekea walinzi,
Najivuna kwa bwana. X2