 
 
Na kenedy Jagaji 
Upendo wa MUNGU kwa mwanadamu hauna mwanzo wala
mwisho, MUNGU hupenda siku zote na yupo tayari kukupokea endapo utamkiri na
kumfuata 
Yakobo 4:8
“mkaribieni MUNGU,naye atawakaribia ninyi”
Na  sisi tumeona na kushuhudia yakuwa Baba
amemtuma mwana kua mwokokozi wa ulimwengu, 
na sisi tumelifahamu pendo alilo nalo kwetu sisi na kuliamini Mungu ni
pendo , naye akaaye katika pendo hukaa ndani yake.
1 yohana 6:14,16
Biblia inatukumbusha
kuhusu Baraka na ahadi ambazo Mungu atupazo kila siku , jambo muhimu la
kuzungumzia ni  kuhusu  jinsi gani Mungu anatupenda hata kumtoa
mwanae kwa kile ambacho alikiumba kwa mkono wake kisipotee. Hii ni moja ya kazi
kubwa na sadaka ya pekee katika ulimwengu ambayo haitatokea daima na ni upendo
usio na kifani katika kazi ya Mungu kwa Mwandamu.
Sasa ni wakati wako wa
kumshukuru Mungu kwa zawadi yake ya pekee kwako na utambue upendo  mkuu wa Mungu katika maisha yako ya kila siku
kuna kitu ambacho ni zaidi ya kazi yako, familia yako pesa na utajiri wako .
jambo ambalo Mungu anahitaji kutoka kwako ni shukrana na kuwapenda wengine kama
alivyo kupenda wewe.
Kristo analikufa  kwa ajili yako.
Hapa tunaweza kufikiri
kuhusu upendo wa yesu kristo kwako, yesu anakupenda sana hata kuutoa uhai wake
kwa ajili yako, tena uiishi milele.
Je ni nani anaeweza
kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake? Jibu ni hapana  kwa wanadamu 
“kwa maana jinsi hii
Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwae wa pekee ili kila mtu amwaminie
asipotee, bali awe na uzima wa milele maana Mungu hakumtuma  mMwana ulimwengununi ili ahukumu aulimwengu  bali ulimwengu uokolewe katika yeye”
Yohana 3:16
Kifo ni ishara ya mwanzo mpya wa maisha  mengine.
Hakuna
hata mmoja ajuae lini na wapi atakufa lakini hutokea kwa kila mmoja , lakini
kifo ni jambo ambalo kila mtu anahitaji kujiaanda nalo. Kwanini? Kwa sababu
kifo ni sehemu ya maisha ya mwandamu . unapopanga mipango yako ya maisha
kumbuka kupanga pia kuhusu maisha yako baadaa ya kufa . ni vema uwe tayari
kuishi na kufa kuanzia  sasa.
 






 
 
