Mara nyingi mkristo amezoelea mabadilko ya mazungumzo na marafiki zake juu ya imani yake . wakati akieleza ni imani zipi ambazo kipekee zilikuwa na umuhimu wa kipekee katika maisha yake binafsi.na vilevile katika kanisa najamii , mjadala ulijikita zaidi juu ya amali maalumu na mambo maalum. Siku hizi, maswali hayo mara nyingi si yenye kuvutia kwa kuwa sasa hivi mjadala.
Unajikumbusha juu ya suala
la haki za mtu binafsi kulazimisha amali zake mwenyewe juu ya wengine
.suala la utandavu wa amali limekwishaibuka mbele ya amali za kipekee
zilizo kwisha tajwa.
Ni rahisi kudai kuwa hakuna amali kamilifu . suala ni kujua
iwapo tamko hili laweza kulindwa. Mtu hahitaji muda mrefu kutafuta bila
kutambua amali binafsi za mpinzani wake . hakatai amali kwa ujumla , bali ana mfumo wake wa kima adili.
Wanafalsafa wachache wamejaribu kufikiri kikamilifu wazo
hilo kuwa hakuna amali kamilifu, na kwamba kila kitu ni chenye uhusiano na kingine.Mmoja kati ya watu muhimu kabisa ni
mwanafalsa wa kifarasa , Albert Camus
1913-1960, ambaye alikifinyanga kizazi kizima cha wanafunzi , Ingawa
wachache walitamani kwenda umbali aliokuwa amekwenda yeye.
Camus aliunda “falsafa ya Mpumbavu”,ambayo kwa ujumla ilinga
amali kamilifu.Alikuwa akitambua matokeo ya mfumo wa amali zenye uhusiano.
“Ikiwa mtu haamini chochote , Ikiwa chochote Kina maana,na ikiwa
hatuwezi kuthibitisha amali, kila kitu kitu chawezekana na hakuna kilicho
muhimu”.
Hakuna kwa ajili ya au kinyume na mwuaji si mwenye haki wala
asiye haki .mtu aweza kuwasha matanuru kwa utayari ulio sawa na Yule anayetoa msaada kwa kilema .uovu na wema
hutokea kwa bahati au ghafla.
Kwa ujumla hakuna miongoni mwetu ambaye yuko tayari kukubali
matokeo ya kupinga kabisa amali kamilifu –kwa hakika.
“Iwapo ningepaswa kuandika bubuso (dogma) la kimaadili ,
kitabu kingekuawa na ukubwa wa kurasa 100, lakini kurasa 99 kati ya hizo
zingekuwa wazi. Katika ukurasa wa mwisho ningeandika , ‘Ninajua jukumu moja tu, jukumu
la kupenda’.Na kwa hayo mengine
yote nasema hapana”.
Kikamilifu ningechagua Uhuru . kwa kuwa wakati haki inaposhindwa
kutambuliwa,basi uhuru hulinda uwezo wa
kupinga dhidi ya ukosefu wa haki, na hivyo kuikokoa jamii”.
Hoja za camus zinapingana zenyewe. Kwa mujibu wa tamko la
kwanza, ikiwa maana na amali ni vitu ambavyo havipo, basi tamko kuwa kila kitu
ni sawa katika thamani haliwezi kufanywa,kwa kuwa linafanya tathmini, japo ni
katika hali hasi . Mkusanyiko katika
hoja ya pili ni wazi zaidi . Jukumu la kupenda ni kanuni ya msingi,kamilifu naya kimaadili, bali lina ikinga mbali na mjadala
na uchunguzi wa kina .msisitizo
wa Camus juu ya kuhuburi mfumo usio na maadili hutengeneza mfumo wake wa
kikamilifu na usiopaswa kuulizwa na ‘jukumu’ lake kuwa asili ya mawazo yote.
Mbali na hayo,wazo kuwa wajibu wa kupenda ni desturi ya
hali ya juu kabisa, ni kanuni ya msingi ya Maadili ya Kikristo.Camus ,
aliyeamini juu ya uwepo wa Mungu, hawazidi wapinzani wake wakristo, kwa chochote
anachoweza kumaanisha kuhusu Upendo.
ITAENDELEA