Safari ya Usagara
Tarehe 10 Novemba 1884 Peters alifika Unguja pamoja na wanakamati wawili ili aendelee kuzunguka kwenye Tanganyika. Serikali ya Kijerumani ya Chansella Bismarck haikukubali mipango yake kwa sababu iliogopa vurugu kwenye mkutano ulioitishwa tayari. Hivyo Peters alipofika kwenye ubalozi wa Ujerumani mjini Zanzibar alipokewa kwa barua kutoka Berlin iliyosema ya kwamba hawezi kutegemea msaada wowote kwani juhudi zake ziko nje ya siasa ya nchi.Peters akimwogopa Sultani pamoja na Waingereza alivuka kwa siri kutoka Unguja kwenda bara. Alifaulu kutembelea masultani au machifu kadhaa waliotia aina ya sahihi kwenye karatasi walizoonyeshwa na Peters. Karatasi hizo ziliandikwa kwa lugha ya Kijerumani zikisema ya kwamba chifu fulani aliweka eneo lake chini ya mamlaka ya shirika la Kijerumani pamoja na kulipatia shirika hilo haki ya kutumia maeneo na malighafi yote.
Kuna hakika ya kwamba machifu hawakuelewa walichofanya kwa kuchora alama zao kwenye karatasi hizo; walifikiri kwamba wameahidiwa ulinzi kutoka kwa mtawala wa mbali ambaye labda siku moja atakuwa na faida kwao, lakini hawakuelewa kwamba walitoa kibali kwa wageni kutawala nchi.
Peters mwenyewe alisimulia jinsi alivyowapa machifu pombe kali hadi wakawa tayari kuchora alama zao kwenye karatasi walizoonyeshwa bila kuelewa maana yake.
Kwa njia hiyo katika muda mfupi kati ya tarehe 23 Novemba na 17 Desemba 1884 Peters alipata hati kutoka machifu wa Usagara, Nguru, Useguha na Ukami kwa ajili ya shirika lake, jumla eneo la km² 140,000.
Jinsi alivyowatenda Waafrika
Katika msafara huo tabia za Peters zilionyesha jinsi alivyodharau Waafrika. Aliamini na kuandika kwamba Mwafrika hutawaliwa kwa kiboko tu. Kwake Mwafrika hakuwa mtu kamili. Akijiona mwenyewe ni bwana ambaye wenyeji wanapaswa kumtumikia, aliwadharau.Alipopitia Ugogo alimkasirikia Mgogo aliyecheka alipomtazama akinyoa ndevu zake, akaamuru apigwe kiboko. Tendo hilo liliwasababisha Wagogo kuchukua silaha, ikawa vita ambapo watu wakauawa kwa wingi.
Watu waliosafiri naye na kumjua walisimulia jinsi alivyowapiga mara nyingi mahamali au watumishi wake, hata akapewa nao jina “mkono damu”.
Dr. karl peters (kati) akiwa na wenzake Dr. karl juhike na Joachim Graf, huyo Dr. karl peter ndio aliwaingiza mkenge machief wa Taganyika kwa Mikataba ya Ulaghai.

Dr. karl peters (kati) akiwa na wenzake Dr. karl juhike na Joachim Graf, huyo Dr. karl peter ndio aliwaingiza mkenge machief wa Taganyika kwa Mikataba ya Ulaghai.
Mojawapo ya mikataba hiyo ule maarufu wa Chifu Mangungo wa Usagara na mingine mingi. Katika mikataba yote hiyo machifu walikuwa wanakubali kuyaachilia maeneo ya ardhi yao kuwa chini ya ulinzi wa Mjerumani na kutumiwa kwa faida ya Mjerumani kwa milele yote. Wengi tunafahamu kuwa wazee hawa walikubali kwa sababu moja kubwa walikuwa hawajui kilichomo kwenye mikataba hiyo na hivyo hata walipokuja kugundua kuwa wameuza ardi yao "mikataba" ile ilikuwa halali na Ujerumani ilikuwa tayari kuhakikisha inasimama hata kwa vita (Kilimanjaro ni mfano mmoja wapo).
Mikataba hii ilifichwa kwa wenyewe na ilifanywa na watawala wao; wakulima na wanakijiji wengine hawakujua kuwa machifu wao wameuza ardhi yao. Na hata kama wangetaka kujua wasingeweza kujua kwani mikataba ilikuwa ni siri kati ya watawala na kampuni hiyo ya kigeni. Na hivyo ndivyo kihistoria eneo ambalo baadaye lilikuja kujulikana kama Tanganyika lilivyoangukia mikononi mwa Ujerumani - hii ilijumuisha Rwanda na Burundi. Hii ilibadilika baada ya vita ya kwanza ya dunia ambapo Tanganyika ikawekwa chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa kupitia Uingereza.
Mjerumani kwa kutumia kampuni ya GEAC kujenga reli, kuanzisha mashamba ya katani, pamba n.k na vyote hivi vilifanywa si kwa ajili ya kuwanufaisha wazawa au wananchi bali hatima yake mazao yanayopatikana yapelekwe Ujerumani kuwa malighafi katika viwanda vyao na zile nyingine za kuuzwa sehemu nyingine kuwa chanzo cha mapato kwa Ujerumani. Wananchi hawakuwa na uchaguzi wowote wa nini kinapandwa, nani anasimamia na hata hawakuwa na uamuzi juu ya matumizi ya faida ambayo Mjerumani alikuwa anapata. Hapa ndipo ulipokuwa Ujinga wa Mwafrika.
Sasa ujinga si ugonjwa au tusi; ujinga ni hali ya kutokujua (ignorance). Mtu aliye mjinga akijuzwa anaerevuka na ujinga humtoka katika lile jambo ambalo alikuwa halijui. Na kila mwanadamu ana ujinga wa aina fulani na hivyo katika maisha yote anatakiwa awe tayari kujifunza. Lakini kwenye eneo ambalo ufahamu upo tayari na unapatikana mtu hatakiwi kuendelea kuwa mjinga. Ujinga wa aina hiyo ambao mtu anauchagua ndio huitwa upumbavu au wengine wanaitwa ujuha kwani ni mtu ambaye hata akijuzwa hajui na hawezi kujua kwa sababu hayuko tayari kujua!
Leo hii watawala wetu wametuambia mikataba ni siri na kuwa mikataba hiyo ikiwekwa wazi basi wawekezaji wanaweza kukimbia na kuwa mikataba hiyo ni siri kati ya 'serikali na wawekezaji' hata kama inahusu ardhi ya umma na mali umma. Ujinga ni kuwa tumekubali kuwa hilo ni kweli! Na ujinga zaidi ni kuwa watawala wetu wanaingia mikataba na wanaamini ni vizuri kuifanya siri na hivyo hatujui nini kilichomo. Mkataba ule wa Carl Peters na Chief Mangungo ulikuwa na kipengele kinachosema kuwa ardhi hiyo ingeweza kutumiwa "exclusively" kwa matumizi ya Mjerumani.
Katika mikataba ya kina Chief Mangugo wa leo wanatuuza wananchi kwa kutwambia mikataba ni siri, kwanini iwe siri wakati rasilimali ni za watanzania wote.
wawakilishi wa wananchi wanajifunza nini kutoka kwa chief mangugo na Karl peter?
Je hawana mpango zaidi ya kuhakikisha wanapata maslahi yao na mposho zao wanasahau kazi ambayo wananchi tumewaamini na kuwatuma kutuwakilisha katika mambo yanayohusu maendeleo ya nchi yetu.
hebu tujaribu kufikiri mikataba feki ambayo inapitishwa na Wabunge wetu, huku ikishangiliwa kwa makofi na vigeregere.
inatuumiza wananchi na wawakilishi wetu wako wakipotea kitu kidogo kwa ajili ya maslai yao je? Ni kweli akili zao zipo kama za kina chief mangugo au ni makusudi?
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap








