Recent Posts

PropellerAds

Tuesday, May 15, 2018

Nguvu katika Kushukuru

s  Image result for asante 
1.shukrani inasimamisha imani
imani hupokea sasa na kuyaona ndani mambo yanayotarajiwa kuonekana nje baadaye. shukrani ni tendo la imani linaloonyesha umeshapokea sasa. pasipo matendo imani haizai, shukrani ni tendo linaloizalisha imani“lakini akiiona ahadi ya mungu hakusita kwa kutoamini bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza mungu” warumi 4:20
2. shukrani inatakasa


luka 17:17 – 19 “yesu akajibu, akanena hawakutakaswa wote kumi? wale kenda wa wapi? (18) je! hawakuonekana waliorudi kumpa mungu utukufu ila mgeni huyu? (19) akamwambi, inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.”1timotheo 4:1 – 5

· kusafisha
· kutenga
mwenye ukoma alipoenda kushukuru kwa yesu, alitakasika kabisa, siyo kupona tu. tunaposhukuru kwaajili ya chakula kinatakaswa. kinatengwa maalum kwaajili ya utukufu wa mungu.


3. shukrani inazidisha
yohana 6:1 – 13 “baada ya hayo yesu alikwenda zake ng’ambo ya bahari ya galilaya, nayo ndiyo ya tiberia.(2)na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa. (3)naye yesu akakwea mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. (4)na pasaka, sikukuu ya wayahudi, ilikuwa karibu. (5)basi yesu alipoinua macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia filipo, tununue wapi mikate, ili hawa wapate kula? (6)na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. (7)filipo akamjibu, mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu. (8)wanafunzi wake mmojawapo, andrea, nduguye simoni petro, akamwambia, (9)yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa? (10)yesu akasema, waketisheni watu. na mahali pale palikuwa na majani tele. basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao. (11)“basi yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. (12)nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee cho chote. (13) basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula.” baada ya yesu kushukuru mikate na samaki viliongezeka. unaposhukuru kwa mambo machache ni rahisi kuongezeka. 
 
4. shukrani inaokoa
1wakorintho 10:1 – 12 “kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;(2)wote wakabatizwa wawe wa musa katika wingu na katika bahari; (3)wote wakala chakula kile kile cha roho; (4) wote wakanywa kinywaji kilekile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba war oho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni kristo. (5)lakini wengi sana katika wao, mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. (6)basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.(7)wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.(8)wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. (9)wala tumjaribu bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. (10)wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. (11)basi mambo hayo yote yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. (12)kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.” badala ya kunungunika kwaajili ya mambo yanayokuhusu, shukuru. shukkrani inaondoa manunguniko na kukufanya uendelee kumfurahia mungu.


5. shukrani inaondoa Ubaya wa Mwanzo
yohana 11:38 – 44“basi yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. nalo lilikuwa na pango, na jiwe limewekwa juu yake. (39)yesu akasema, liondoeni jiwe. martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. (40)yesu akamwambia, mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa mungu? (41)basi wakaliondoa lile jiwe. yesu akainua macho yake juu, akasema, baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. (42)nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. (43) naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, lazaro, njoo huku nje. (44)akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. naye yesu akamwaambia, mfungueni, mkamwache aende zake.”. baada ya yesu kushukuru lazaro alifufuka kwa kuamuru. msiba uliisha! maiti iliyoanza kunuka ikaacha. hali hata ikiwa imechafuka tushukuru na kutamka mapenzi ya mungu kwa kuamuru.


6. shukrani ni mapenzi ya mungu
1wathesalonike 5:18 “shukuru kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya mungu kwenu katika kristo yesu.”
1yohana 5:14 “na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.”
wakolosai 4:2 “dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani”. kuomba twaomba kwa mapenzi ya mungu, tunaposhukuru tunafanya mapenzi ya mungu.


7. shukrani zinaenenda na usafi wa dhamiri

usiache kushukuru, ukishindwa kufanya vyote, usishindwe kumshukuru mungu.