Home »
» Njia Sita za kupata mafanikio
Na,
Mwl. kenny jagaji.
Mtu anafanikia kiukweli kwa kupata njia bora kabisa ya maisha ambayo inatokana a kufuata viwango vya Mungu na kuishi na kusudi la Mungu kwa wanadamu. Biblia inasemakwamba mtu anayeishi maisha ya aina hiyo
"atakuwa kama mti uliopandwa kando ya vijito vya Maji, ambao hutoa matunda yake katika majira yake na ambao majani yake hayanyauki, na kila jambo analofanya litafanikiwa "
Zaburi 1:3
Naam, ingawa sisi si wakamilifu na tunafanya makosa, tunaweza kufanikiwa maishani! je, hilo linakuvutia? ikiwa ndivyo , basi kanuni sita zinazofuata za biblia zinaweza kukusudia ufikie lengo hilo na hivyo kuthibitisha waziwazikwamba kwa kweli mafundisho ya Biblia ni hekima kwa Mungu
Yakobo 3:17
1. Mtazamo unaofaa kuhusu Pesa
"Kupenda pesa ni chanzo cha mambo Mabaya ya namna zote, na kwa kujitahidi kufikia upendo huo wengine..... wamejichoma wenyewe kila mahali kwa maumivu mengi " 1 timotheo 6:10
Ona kwamba tatizo si pesa kwa kuwa sisi sote tunahitaji pesa ili kujitunza na kutunza familia zetu. Tatizo ni kupenda pesa. kwa kweli ,Upendo huo hufanya pesa ziwe bwana, au Mungu.
Watu ambao hukimbizana na utajiri ili wapate mafanikio. kwa kweli wanafuatilia upepo.Mbali na kutamanishwa wanapatwa na maumivu mengi. kwa mfano katika jitahada zao za kutafuta mali nyingi, mara nyingi watu hupuuza uhusiano wao na familia na marafiki. wengine hukosa usingizi , si kwa sababu ya kazi tu, bali pia kwa sababu ya wasiwasi.
"usingizi wa kibarua ni mtamu , awe ameshiba au hakula" Lakini usingizi wa tajairi ni wa wasiwasi daima, maana ziada ya mali yake humsumbua usiku kucha"
Mhubiri 5:12
zaidi ya kuwa bwana mkatili ni bwana mdaganyifu pia. yesu kristo alizungumza kuhusu "Nguvu za udanganyifu za utajiri" Marko 4:19. hilo linamaanisha kwamba utajiri humwahidi mtu kwamba utampa furaha, lakini haufanyi hivyo.Badala yake unamfanya mtu atamani utajiri zaidi. "Anayependa fedha hatatosheka na fedha" Mhubiri 5:10
kwa ufupi,mtu anayependa pesa anajiumiza tu. anavunjika moyo, anakatishwa tamaa, au hata kujihusisha katika uhalifu Methali 28:20. ukarimu kuwa tayari kusamehe usafi wa maadili, upendo, na uhusiano mzuri pamoja na Mungu, ni mambo yanayoleta furaha na mafanikio.
2. Roho ya Ukarimu
"kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko ilivyo katika kupokea" matendo 20:35 ingawa kuwapa watu vitu mara kwa mara kunaweza kumfanya mtu awe na furaha ya Muda roho ya ukarimu kumfanya awe na furaha ya kudumu. ni kweli kwamba kuna njia mbali mbali za kuonesha ukarimu. mojawapo ya njia bora na inayothaminiwa sana ni kutenda wakati ili kuwa pamoja na watu na kufanya mambo nao.
Isitoshe, watu wanaowapa watu vitu kwa kawaida hawapungukiwi na chocote maishani kwa sababu tu ya kuwa wakarimu. methali 11:25 inasema hivi "Mtu mkarimu atafanikishwa, amnyweshe mwingine maji atanyweshwa" kupata na maneno hayo, watu ambao ni wakarimu kutoka moyoni, ambao hawawapi watu vitu wakitarajia kulipwa, wanathaminiwa na kupendwa na Mungu - Waebrania 13:16.
3. Samehe kwa hiari
"Endeleeni ........ kusaemehana kwa hiari ikiwa yeyote ana sababu ya kulalamika juu ya mwingine . kama vile Yesu alivyowasemehe ninyi kwa hiari, nanyi fanyeni vivyo hivyo pia " wakolosai 3:13
siku hizi watu hawako tayari kusamehe; wao hulipiza kisasi baadala ya kuonesha rehema. Matokeo yake ni nini? wanapotukanwa wanatukana , nao hulipiza jeuri kwa jeuri.
unawezaje kusaemehe zaidi? Anza kwa kujichunguza kwa unyoofu. je, nyakati nyingine huwakasirishi watu? unafurahi wanapokusamhe? kwa hiyo mbona usiwaoneshe wengine rehema ? Mathayo 18:21-35 pia ni muhimu kujizuia "Hesabu moja hadi kumi " au tafuta wakati ili utulize hasira. tambua kwamba kujizuia si udhaifu." asiye mwepesi wa hasira ni bora kuliko mwanaume mwenye Nguvu" inasema Methali 16:32 "Ni bora kuliko mwanaume mwenye Nguvu" inaonesha mtu amefanikiwa kikweli.
4.Ishi kulingana na viwango vya Mungu.
"Amri ya Mungu ni safi hufanya macho yang'ae" - Zaburi 19:8 kwa ufupi, viwango ungu vinatufaidi kimwili, kiakili, na kihisia. vinatulinda dhidi ya mazoea yenye kudhuru kama vile kutumia dawa za kulevya , ukosefu wa maadili na kutazama pica za ngono. 2 wakorintho 7:1, wakolosai 3:5 huenda mazoea hayo yantokeza madhara mabaya kama vile uhalifu, Umasikini, kutokuaminiana, kuvunjika kwa familia, matatizo ya kiakili na kihisia, magonjwa na kifo cha Mapema.
kwa upande mwingine , wale wanaoishi kulingana na viwango vya Mungu wanakuwa na Mahusiano mazuri, pia wanjiheshimu na kuwa na imani ya akili . katika Isaya 48:17,18, Mungu anasema kwamba yeye ndiye "anayekufundisha ili ujifahidi mwenyewe , yeye anaekufanya uende katika njia unayopaswa kutembea ndani yake" kisha anaongeza hivi "Laiti ungesikiliza amri! ndipo imani yako ingekuwa kama mto , uadilifu wako kama mawimbi ya bahari"
Ndiyo, muumba wetu anatutakia maisha bora zaidi anataka tuende katika njia ya mafanikio ya kweli.
5. Onesha Upendo na si Ubinafsi.
"upendo hujenga " 1 wakorintho 8:1. Je, unawezqa kuwazia maisha yasiyo na upendo? yangekua maisha yasio na maana kama nini ! ikiwa sina upendo kwa wengine mimi si kitu..... Sipati faida hata kidogo" - wakorintho 13:2,3
Upendo unaotajwa hapa si ule wa kimahaba ambao una mahali pake panpofaa. Badala yake ni upendo unaodumu ambao unaongozwa na kanuni za mungu. - Mathayo 22:37-39 isitoshe , mtu haonyeshwi tu Upendo huo bali anauonesha kwa matendo.Paulo aliendelea kusema kwamba Upendo huo ni wenye subira na pia fadhili. hauna wivu, haujigambi, au kujivuna. hautafuti faida yake mwenyewe (hutafuta faida za wengine), na hauchokozeki kwa urahisi bali ni wenye kusamehe. Upendo kama huo hujenga. Pia unatusaidia tuwe na uhusiano mzuri na wengine hasa washiriki wa familia.- 1 wakorintho 13:4-8.
Kwa wazazi, Upendo unamaanisha kuwa na hisia nyororo kuwaelekea watoto wao na kuwapa mwongozo ulio wazi uaotegemea biblia kuhusu maadili na tabia nyingine watoto wanaolelewa katika mazingira kama hayo hujihisi salama, wanapendwa, na kuthaminiwa wakiwa sehemu ya familia iliyo imara-Wefeso 5:33-6:4, Wakolosai 3:20.
Pia, Upendo unaotegemea kanuni 'Unashangilia pamoja na kweli', yaani kweli kumhusu Mungu inayopatikana katika Biblia 1 Wakorintho 13:6, Yohana 17:17. Ili kufafanua fikiria mfano huu: wenzi walio na Matatizo katika ndoa yao wanaamua kusoma pamoja maneno ya Yesu yanayopatikana kwenye Marko 10:9. "kwa hiyo kile ambacho mungu ameunganisha (katika ndoa) mtu yeyote asitenganishe."
Sasa , lazima wajichunguze mioyo yao. je kweli wnashangilia pamija na kweli za biblia? je, wataiona na kujitahidi kutatua matatizo yao kwa upendo? kwa kufanya hivyo wanaweza kufanya ndoa yao ifanikiwe, na wanaweza kushangilia matokeo mazuri ya jitahada zao.
6. Tambua Uhitaji wako.
"wenye furaha ni wale wanaotambua uhitaji wao wa kiroho"- mathayo 5:3 tofauti na wanyama, wanadamu wana uwezo wa kuthamini mambo ya kiroho. kwa sababu hiyo sisi hujiuliza aswali kama haya , ni nini kusudi la uhai? Je, kuna Muumba? Ni nini hutupata tunapokufa? Wakati ujo utakuwaje?
Ulimwenguni pote, mamailioni ya watu wanyoofu wametambua kwamba Biblia inajibu maswali hayo.kwa mfano, swali la mwisho linahusiana na kusudi la MUNGU kwa wanadamu. kusudi hilo ni nini? Ni kwamba dunia iwe paradiso inayokaliwa na watu wanaompenda Mungu na viwango vyake.
Zaburi 37:29 inasema "Waadilifu wenyewe wataimiliki dunia, nao watakaa milele juu yake."
Ni wazi kwamba Muumba wetu anataka tufanikiwe kwa Muda mrefu zaidi kuliko miaka 70 na 80 tu.
Anataka tufanikiwe milele! kwa hiyo sasa ndio wakati wako wa kujifunza kuhusu muumba wako.Yesu alisema "Uzima wa milele ndio huu, waendelee kupata ujuzi juu yako wewe,Mungu wa pekee wa kweli na juu ya yule iliyemtuma Yesu Kristo." Yohana 17:3 Unapoendelea kupata ujuzi huo na kuutumia maishani, utangundua kwamba "Baraka za Mungu...... ndiyo hutajirisha, naye haongezi maumivu pamoja nayo."- Mithali 10:22.
Itaendelea
Mambo zaidi yanayoleta mafanikio.