wafilipi 3:1
3 Hatimaye
ndugu zangu, furahini katika Bwana. Mimi sichoki kuwaandikieni mambo
yale yale niliyokwisha waandikia kwa maana najua kwamba yatakuwa ni
kinga kwenu. 2 Jihadharini na watenda maovu, hao mbwa, na wale wanaokaza mafundisho ya kutahiriwa. 3 Sisi
tumepokea tohara ya kweli, kwa maana tunamwabudu Mungu katika Roho.
Sisi tunaona fahari kwa ajili ya maisha yetu ndani ya Kristo Yesu.
Hatuweki matumaini yetu katika mambo ya mwili, 4 ijapokuwa
mimi mwenyewe ninazo sababu za kuweka matumaini katika mambo hayo. Kama
mtu mwingine ye yote anadhani kuwa anazo sababu za kuweka matumaini
yake katika mambo ya mwili, basi mimi ninazo sababu zaidi. 5 Nilitahiriwa
siku ya nane, mimi ni Mwis raeli wa kabila la Benjamini; Mwebrania
halisi. Kuhusu mambo ya kushika sheria, mimi nilikuwa Mfarisayo; 6 na
kwa upande wa juhudi, mimi nilikuwa na bidii katika kutesa kanisa; na
kuhusu haki ipatikanayo kwa kutii sheria, mimi nilikuwa sina hatia.