Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, February 14, 2018

Malaria ni nini?

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinavyojulikana kama Plasmodium ambavyo huenezwa na mbu jike aina ya anopheles.
Dalili za malaria isiyo kali
  • Homa,maumivu ya kichwa
  • Maumivu ya mwili
  • Tumbo kuuma,kuharisha
  • Kichefuchefu,kutapika
  • Kizunguzungu
  • Kutokwa jasho
  • Kutetemeka
  • Kifua kuuma
  • Kukosa hamu ya kula
Dalili za malaria kali
  • Mabadiliko katika mwenendo na tabia
  • Uchovu mkubwa kupita kiasi (mgonjwa hawezi kukaa au kusimama)
  • Upungufu mkubwa wa damu
  • Kupoteza fahamu
  • Kupumua kwa shida
  • Degedege/mtukutiko mwili (Kwa watoto wadogo)
  • Kutapika kila kitu,kushindwa kunywa na kunyonya
  • Mzunguko hafifu wa damu,kutokwa damu isiyo ganda kwa urahisi
  • Figo kushindwa kufanya kazi na kukojoa mkojo wenye rangi nyeusi/kahawia.
Kumbuka
Ni muhimu kuzifahamu dalili za malaria isiyo kali na malaria kali.Iwapo utaona mojawapo au zaidi ya dalili zilizotajwa ni wajibu wako kuwahi kwenye kituo cha kutoa huduma za afya ili upate matibabu mapema.Ukubwa wa Tatizo
Hapa inchini inakadiriwa kuwa kati ya watu milioni 16 hadi 18 huugua malaria kila mwaka na kati yao watu 100.000 hufa.Asilimia sabini ya vifo hivyo ni watoto chini ya umri wa miaka mitano.Malaria ni chanzo kikubwa cha upungufu mkubwa wa damu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.Asilimia kumi na nne ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano vinavyotokea vituoni hutokana na upungufu wa damu.Hivyo malaria inachangia asilimia 51 ya vifo vyote vya watoto chini ya umri wa miaka mitano vinavyotokea vituoni.kwa wajawazito,malaria na upungufu wa damu vinachangia asilimia 25 ya vifo vinavyotokana na uzazi.
Mbadiliko ya matibabu ya malaria
Moja ya matatizo makubwa yanayolikabili bara ya Afrika ni usugu wa vimelea kwa dawa za malaria.Kutokana na tatizo hili kuongezeka,Shirika la Afya Duniani limependekeza kuwa nchi zote zinazotumia dawa zisizo mseto kama vile Chloroquine,Amodiaquine na Sulfadoxine-pyrimethamin (SP) zibadilishe na kuanza kutumia dawa mseto hususan zenye Artemisinin.
Kwa nini dawa mseto zitumike?
Dawa mseto zina mchanganyiko wa dawa mbili au zaidi ambazo hufanya kuwa na nguvu ya kutibu zaidi na kuondoa vimelea mwilini  kwa haraka na hivyo mgonjwa kupona mapema.Dawa mseto zenye Artemisinin zikitumiwa kwa usahihi hutibu malaria kwa kiwango cha juu,hupunguza usugu wa vimelea kwa dawa na pia ni salama.
Aina za Dawa Mseto zenye artemisinin
Kuna aina mbalimbali za dawa mseto za malaria zenye artemisinin.Serikali,kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imependekeza dawa yenye artemisinin iitwayo Artemether-Lumefantrine (ALu) kuwa dawa mseto ya safu ya kwanza ya kutibu malaria isiyo kali Tanzania Bara.
Matumizi ya Alu 
Dawa ya Alu inapatikana wapi? 

Inapatikana kwenye vituo vya kutoa huduma za afya vya serikali kwa bei nafuu na ipo kwenye pakiti maalum tofauti na zile zilizopo kwenye maduka ya dawa.
Mambo muhimu ya kuzingatia
  • Tiba ya malaria imebadilika kutoka SP kuwa dawa mseto zenye artemisinin
  • Dawa ya mseto ya malaria ni TIBA na SIO KINGA
  • Malaria inatibika,tumia dawa mseto ya malaria
  • Dawa mseto ya malaria itumike baada yam lo
  • Malaria inaua,okoa maisha yako kwa kutumia dawa mseto ya malaria
  • Wajawazito na watoto wenye uzito chini ya kilo tano wapate ushauri wa mhudumu wa afya kabla ya utumia dawa mseto ya  malaria
  • Matumizi sahihi ya dawa mseto ya malaria humponya mgonjwa
  • Usipomaliza dozi ya dawa mseto ya malaria kama inavyoshauriwa,kuna hatari ya kutokupona
  • Kinga ni bora zaidi ya tiba kwa hiyo zingatia matumizi ya chandarua chenye viuatilifu na matumizi ya tiba ya tahadhari wakati wa ujauzito.