Recent Posts

PropellerAds

Tuesday, December 6, 2016

Ethiopia yazindua reli mpya ya kisasa

Ethiopia na Djibouti zimezindua reli ya kisasa ya treni za kutumia nguvu za umeme ambayo inaunganisha mji mkuu wa Addis Ababa na mji wa bandarini wa Djibouti.
Reli hiyo imejengwa na kampuni mbili za Uchina, kwa gharama ya takriban dola 4 bilioni za Kimarekani ambazo zilitolewa na serikali ya Uchina kama mkopo.
Reli hiyo inatarajiwa kuipa Ethiopia njia rahisi ya kufikisha bidhaa zake, hasa mazao ya kilimo, hadi dandarini.
Uchumi wa Ethiopia umekuwa ukikua kwa kasi kutokana na ongezeko la uzalishaj wa kilimo na ukuaji pia wa miji.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Ethiopia, yenye watu 97 milioni ni moja ya mataifa yenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi duniani kwa sasa.
Kenya inajenga reli nyingine ya 'wenye kichaa'?
Tanzania yapokea ndege mpya kutoka Canada
Tanzania yasifiwa na Benki ya Dunia
Kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, uchumi wa taifa hilo ulikua kwa asilimia 10.2 mwaka 2014/15, na kasi hiyo inatarajiwa kuendelea mwaka 2016 na mwaka 2017.
Reli hiyo ni ya umbali wakilomita 752, na kasi yake ya wastani itakuwa kilomita 120 kwa saa, jambo litakalofupisha safari ya kutoka Addis Ababa hadi Djibouti kuwa chini ya saa kumi ikilinganishwa na siku mbili zilizotumiwa awali.
Reli hiyo ndio mradi wa pili mkubwa wa reli inayounganisha mataifa zaidi ya mawili ambayo imejengwa na kampuni za Kichina barani Afrika.
Mradi huo mwingine ni reli ya Tazara inayounganisha jiji la Dar es Salaam, Tanzania na mji wa Kapiri Mposhi nchini Zambia.
Wakati wa ziara yake Ethiopia Mei 2013, naibu waziri mkuu wa China Wang Yang alisema mradi huo wa reli wa Ethiopia-Djibouti ni "Tazara ya enzi mpya."
Rwanda yanunua ndege ya kisasa ya Airbus
Kinyume na mradi wa Tazara, ambao ulijengwa miaka ya 1970 kama mradi wa msaada wa kimataifa kutoka kwa serikali ya Uchina, reli hiyo ya Ethiopia-Djibouti ni mradi wa kibiashara kati ya kampuni za Kichina na serikali za mataifa hayo mawili ya Afrika.