Recent Posts

PropellerAds

Friday, December 16, 2016

Virusi vya zika vyangunduliwa tanzania

Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR imethibitisha kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela, virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.
Njia 10 za kujikinga dhidi ya virusi vya Zika
Virusi hatari vya Zika vyafika Afrika
Dkt Mwele Malecela ameambia BBC kwamba kwa sasa serikali inaangazia kuzuia wajawazito wasiumwe na mbu ambao wanaaminika kueneza virusi hivyo.
"Bado tunajaribu kuangalia ni aina gani ya virusi vya Zika. Lakini hiyo ni dhahiri, tukizingatia kwamba mbu wanaoambukiza Zika wako nchini kwetu na mazingira yaliyoko nchini kwetu hayatofautiani sana na yale ya Amerika ya Kusini na nchi kama Thailand ambako ugonjwa huo unapatikana," amesema Bi Malecela.
"Ugunduzi huu tumeupata kwa watu na tutaendelea kufanya kazi kuangalia kama tutaupata kwa mbu ambao utatuhakikishia basi kwamba ugonjwa huo ina maana umekuwepo nchini ni vile tu ulikuwa haujaonekana."
"Heri nusu shari kuliko shari kamili, kulielewa jambo na kujua kwamba lipo nchini na kujua kwamba wajawazito wanaweza kuzaa watoto wenye matatizo haya kutatuwezesha kuzuia ugonjwa huyu. Tutahakikisha nguvu zetu za kupambana na mbu wanaoeneza virusi hivi zinaongezeka."
Virusi vya Zika zimekuwa vikisababisha watoto kuzaliwa wakiwa na ubongo uliodumaa na vichwa vidogo katika mataifa ya Amerika Kusini na sana Brazil.
Mapema mwaka huu, serikali ya Tanzania iliwaagiza madaktari wote kuwa macho kuhusu hatari ya virusi hivyo mlipuko ulipotokea nchini Brazil.
Virusi vya Zika huenezwa sana na mbu ingawa kumeripotiwa pia visa vya watu kuambukizwa virusi hivyo kupitia kufanya mapenzi.
"Msishike mimba sasa", mataifa yashauri wanawake
Haijabainika iwapo aina ya virusi vya Zika vilivyopatikana Tanzania ni vile ambavyo vimekuwa vikisababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Amerika Kusini.
Virusi vya aina hiyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza barani Afrika katika visiwa vya Cape Verde mwezi Mei mwaka huu.
Jina la virusi hivyo linatokana na msitu wa Zika, Uganda ambapo virusi hivyo vilitambuliwa kwa mara ya kwanza 1947.
Wengi wa walioambukizwa aina ya awali ya virusi walikuwa wakipatwa na homa ambayo si kali sana, mwasho na maumivu katika maungio.
Lakini kwa aina ya sasa, ambayo mlipuko wake ulianza mwishoni mwa mwaka 2015 nchini Brazil, dalili zake zimekuwa kali na virusi hivyo vinaaminika kusababisha kudumaa kwa ubongo na kasoro nyingine mwilini.

Related Posts:

  • Ugomvi wa kikombe cha chai wasababisha maafa Misri Kumekuwa na maandamano ya hasira yaliofanywa na mamia ya watu mjini Cairo baada ya maafisa wa polisi kumpiga risasi na kumuua mchuuzi mmoja kuhusu kile walioshuhudia wanasema ni bei ya kikombe kimoja cha chai. Mtu mmoja … Read More
  • Atolewa kwenye ndege kwa kuongea Kiarabu Mwanafunzi wa chuo kikuu raia wa Iraq katika jimbo la California nchini Marekani anasema kuwa alitolewa kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Southwest baada ya kufanya mazungumzo kwa lugha ya kiarabu. Shirika hilo … Read More
  • Msumbiji mashakani kwa kuficha madeni yake Shirika la fedha duniani IMF, limesitisha ufadhili wake kwa serikali ya Mozambique, baada ya kugundua kuwa serikali ya nchi hiyo ilikosa kutangaza kuwa ilikuwa na madeni ya zaidi ya dola bilioni moja. Afisa mmoja wa shir… Read More
  • Chris Brown:Nilitaka kujiua kwa sababu ya Rihanna Mwanamuziki Chris Brown amesema kuwa alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009. Katika kipande kifupi cha makala yake ya 'Karibu katika maisha yangu',mwanamuziki h… Read More
  • Helikopta ilivyobeba pochi ya gavana Marekani Helikopta ya polisi ilitumwa kuchukua pochi ya gavana wa jimbo moja nchini Marekani, safari iliyogharimu $4,000 (£2,800), uchunguzi umebaini. Kisa hicho kilitokea mwishoni mwa 2014. Gavana wa Alabama Robert Bentley alion… Read More