Rais mteule wa Marekani Donald Trump amelitaka azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kusitisha ujenzi wa makaazi ya Israel katika ardhi ya Palestina.
Katika taarifa iliotolewa kabla ya kura hiyo inayotarajiwa baadaye siku ya Alhamisi, Bw Trump amesema kuwa amani haitaafikiwa kupitia hatua ya Umoja wa Mataifa kuweka masharti.
Azimio hilo litaagiza kwamba shughuli zote za makaazi hayo katika eneo hilo la Palestina, ikiwemo Jerusalem mashariki lazima zisitishwe.
Marekani imekuwa ikiunga mkono Israel katika Umoja wa Mataifa, lakini wanaounga mkono azimio hilo wamekuwa wakitumai kwamba utawala wa rais Obama utasusia kura hiyo.
Albania yatangaza kupiga marufuku TikTok kwa mwaka mmoja
-
Waziri mkuu wa Albania ametangaza kuwa serikali inakusudia kuzuia ufikiaji
wa TikTok kwa mwaka mmoja baada ya mauaji ya mvulana wa shule mwezi
uliopita k...
2 hours ago