Ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya mpira kutoka nchini Brazil ambayo ilipata ajali nchini Colombia inasemekana kwa muujibu wa taarifa zilizovuja ndege hiyo iliishiwa mafuta kutoka katika kifaa cha kurekodia mawasiliano.
Katika mnara wa mawasiliano ya ndege , rubani alisikika akirudia mara kadhaa akiomba ruhusa ya kutua kwa dharura kutokana na hitilafu ya umeme iliyokuwamo ndegeni pamoja na kuishiwa mafuta ya ndege.
Kabla hata mawasiliano hayo yaliyorekodiwa kufikia mwisho ,rubani alisikika akisema yuko angani umbali wa futi elfu tisa sawa na mita elfu mbili mia saba na arobaini na tatu.Taarifa za mawasiliano hayo zimekuwa gumzo katika mitandao kadhaa nchini Colombia na hata katika vyombo vya habari nchini humo, na hivyo kumekuwepo fununu za taarifa hizo kuwa huenda zikawa na chembe ya ukweli kwamba kuishiwa kwa mafuta ndiyo chanzo zha ajali ya ndege hiyo.
Wanajeshi wa Colombia waliliambia shirika la habari la AFP, kwamba pamoja na ndege hiyo kuanguka kuna shaka juu ya ajali hiyo kwani pamoja na ndege hiyo kuanguka hakukuwa na mlipuko wowote na kwamba huenda kulitumika nguvu ingine tofauti na nadharia ya kwisha kwa mafuta ndegeni.
Wadadisi wa mambo na wachunguzi bado hawako tayari kufungua mdomo na kuzungumzia juu ya chanzo chochote cha ajali hiyo na kwamba taarifa kamili ya uchunguzi itatolewa baada ya miezi kadhaa.
Wachezaji wa timu ya Chapecoense walikuwa safarini kuelekea nchini Colombian kwenye mji wa Medellin mahali kulikotarajiwa mechi kubwa ya mpira wa miguu ya kihistoria na badala yake wachezaji hao wameacha historia .Kufuatia vifo vya wachezaji wa timu hiyo, ulimwengu mzima umeungana kuomboleza vifo vyao.
Kwa muujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka katika shirika la ndege la Lamia watu wanne waliokuwa wasafiri na ndege hiyo wameponea chupuchupu kuwa miongoni mwa waliokufa baada ya kukosa tiketi.
Mmoja wa manusura wa ajali hiyo ambaye ni fundi wa ndege Erwin Tumiri, ameeleza namna alivyokwepa kifo, kwamba yeye alifuata maelekezo yote ya namna ya kujiokoa ,anasema abiria wenzie , walio wengi walisimama na kuanza kupiga kelele nay eye aliamua kuweka sanduku lake la kusafiria kati kati ya miguu yake na kuamua kubaki hivyo.
Visanduku viwili vya mawasiliano vya ndege hiyo vyote vilipatikana na tayari vimeanza kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa masuala ya anga.
Wachunguzi wataalamu kutoka nchini Uingereza wanasaidiana na mamlaka za Amerika Kusini kwasababu ndege iliyopata ajali ilitengenezwa na wana anga wa Uingereza BAE nchini Uingereza.Brazil imeanza siku tatu za maombolezo wakati maelfu ya watu na washabiki wa timu ya Chapecoense wako katika mji yaliko makao makuu ya timu hiyo Chapeco wanaendelea mkesha wa maombolezo wakati maandalizi ya kuchukua mabaki ya wachezaji hao inafanywa na jeshi kurejeshwa Brazil ili kuzikwa kwa pamoja katika uwanja wa Chapeco.
Nchi ya Bolivia tayari imekwisha tuma ndege ya kuchukua mabaki ya raia wake waliokufa katika ajali hiyo nchini Colombia.
Timu hiyo iliandika historia ya mafanikio katika soka kwa kuwa kileleni mwa ligi ya Brazil kwamara ya kwanza mwaka 2014.Kati ya watu 77 waliokuwa wameabiri ndege hiyo miongoni mwao ni watu sita tu ndiyo walionusurika .Abiria walio wengi walikuwa ni wachezaji wa timu ya Chapecoense na waandishi habari wapatao ishirini walikuwa miongoni mwa walipoteza maisha
Albania yatangaza kupiga marufuku TikTok kwa mwaka mmoja
-
Waziri mkuu wa Albania ametangaza kuwa serikali inakusudia kuzuia ufikiaji
wa TikTok kwa mwaka mmoja baada ya mauaji ya mvulana wa shule mwezi
uliopita k...
3 hours ago