Recent Posts

PropellerAds

Monday, December 19, 2016

Maajabu ya ziwa natron

TANZANIA NA MAAJABU YAKE
Ni kweli usiopingika kuwa mazingira yetu yana mambo mengi ya kustaajabisha na kuvutia, kwa siku chache zilizopita nilielezea kuhusu uwepo wa ziwa lenye rangi ya pinki ambalo linapatikana Bara la Australia, kwa mshangao wa ajabu kabisa nikaja kugundua kuwa hata hapa Afrika yapo maziwa yenye rangi kama hiyo hasahasa la kule Senegal ambapo watu wake wanalitumia kuvuna chumvi kwa wingi sana.
Back to Tanzania nimekutana na hii habari ya ziwa lenyewe lina rangi nyekundu kama damu,
Hili ni ziwa Natron lenye joto linalofikiwa kuwa digrii 60 za sentigredi na uwepo wa chumvi kali ya kufa mtu, linavutia sana na hata wakati mwingine unaweza kujisikia kutaka kuogelea ndani yake hasahasa kipindi ambacho unasikia joto la kufa mtu lakini watch out hapo si mahali pa mzaha hata kidogo na ndugu zetu wazungu wanamsemo usemao, " look, don't touch"
Rangi ya hili ziwa yamekuwa kivutio si tu kwa binadamu ila hata kwa wanyama mbalimbali, ila sasa cha kustaajabisha na kuogofya ni kuwa pale wanapothubutu kutia mdomo tu kuonja hayo maji hapo hapo wanageuka jiwe/kakamaa/kauka, jambo jema kabisa flamingo, algae na wakati mwingine hata samaki wenyewe hawadhuriki na kiasi kikubwa cha alkaline ipatikanayo katika hili ziwa ndio kwanza wanalitumia kwa ajili ya kuzaliana (breeding zone)
kijana wa kimasai akiwa ndani ya ziwa natron, mcheki amefunika pua kwa sababu ya harufu nzito ya magadi itokayo ndani ya hili ziwa
ziwa Natron
mfano wa ndege aliyekakamaa uonyeshao madhara ya kusogelea hili ziwa, kuna kitu kinaitwa bizzare phenomena ndicho huelezea kwa usahihi madhara ya kuthubutu sogelea hili ziwa
wengi tutajiuliza ni kitu gani hupelekea viumbe vinavyothubutu kusogelea hili ziwa kukakamaa au kuwa kama majiwe, sababu ni kuwa hili ziwa linakiasi kikubwa cha alkaline, na kaustic soda/ magadi ambacho huingia ndani ya mwili wa hicho kiumbe na kupelekea kufa na kukakamaa kabisa
Kweli nimeamini tembea uone, huo ndio uzuri wa Tanzania na maajabu yake,asante kwa kuendelea kutembelea blogu hiiusiache kutembelea kwani kwa siku za mbeleni nitakwenda kuelezea sayansi iliyo nyuma ya uwepo wa rangi nyekundu katika hili ziwa.