Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, December 7, 2016

Wazazi ambao hujuta kwa kuzaa watoto

Mwandishi mmoja kutoka Ufaransa Corinne Maier, ana watoto wawili lakini ndoto yake ni kumuona kitinda mimba akikua na kuondoka nyumbani, akisema kuwa wamemchosha na kumfilisi.
Yafuatayo ni baaadhi ya maoni ya wazazi wengi duniani kuhusu kuwalea watoto.
Majuto
Ni vizuri kufahamu kuwa si mimi peke yangu ninahisi kutokamilika kwa kuwa mama. Nikiwa ninawapenda watoto wangu wawili sana, leo hii ninahisi kuwa singewazaa watoto hawa. Sio tu ni ghalia, lakini kuwalea watoto kunakuja na changamoto nyingi za kukua kitaaluma, wanawake wanalazimika kusubiri hadi zaidi ya miaka 35. Kuna sababu za kuhusu raha ya kuwa mama, lakini nahisi kuchoka na kutokamilika.
Alex, San Antonio.
Ni vigumu kusema kuwa ninajutia kwa kuwa na watoto kwa sababu ninawapenda. Lakini ikiwa nitafikiria nyuma na kujiuliza maswalia, sidhani kama ningetaka tena kuwa na watoto, bila ya wao ningekuwa na pesa, uhuru na pia singekuwa na hofu. Mary, Edinburgh.
Baada ya kulelewa katika familia iliyovunjika, nimekuwa na ndoto ya kuwa na familia kubwa. Nimebarikiwa na mme mzuri na watoto watatu. Wakati nikiandika haya binti yangu amenishika shingoni , siwezi hata kwenda chooni bila kukosa kusikia kilio na vita na jina mama. Krismasi imewadia na badala ya kufurahia, ninahisi kama ningeingia kwa ndege na mmewangu na kwenda popote pasipo kurudi ili kuweza kumjua tena. Tumechoka sana hadi hata siku hizi hatucheki, vile ninaandika haya ninahisi vibaya lakini ninahitaji nishukuru. Andrea, Italy.
Kumlea mtoto wa kisasa imetuacha mimi na mme wangu na uchovu. Haishii utotoni kwa sababu tunawahofia wakiwa na miaka 24 na 26 mtawalia. Tulijaribu kuwawezesha wajitegemee lakini tukashindwa. Wanaishi mbali nasi lakini mwishowe ni lazima tuwapigie simu kila mara. Ninawapenda wote lakini kama ningerudi ujana singekuwa tena na watoto.
Jennifer,Hertfordshire.
Hisia zilizochanganyika
Nina watoto wawili wa kiume na ninawapenda sana hadi uchovu unapoingia na kelele za kila siku zikionekana kuisha. Nilikuwa mvumilivu na kiali yangu ilikuwa kamili . Hilo linaokena kutoweka. Kwa sasa ni mipango, kulala , chakula, mavazi, kucheza , malezi bora. wakati hali ni ngumu nahisi singekuwa na watoto. Lakini wakati wanakubusu au wanapofanya kitu kizuri kwako unahisi vizuri. Anja, Maastricht.
Hakuna majuto
Kuwa na watoto ndicho kitu kizuri zaidi kuwai kufanyika kwangu. Pia ni kazi ngumu. Sijui mtu anaweza kupata wapi maoni kuwa mzazi ndiyo kazi rahisi ambayo huleta furaha. Kuwa na furaha kwa misingi yote ni kitu ambacho mtu hukutafuta kwa muda mrefu. Brian, Ohio.
Sitafikiria tena kutokuwa na watoto. Wameniwezesha kujua mengi kupitia kwa walimu wao, na wazazi wengine. Karen, Virginia.
Kuwa na mtoto kumeniwezesha kuenzi masuala mengi ya kijamii. Niliandika kitabu kwa mtoto wangu wa kiume, ambacho nilimtumia ajenti mmoja na miaka michache baadaye, nimejipata nikiwa mwandishi wa vitabu vya watoto nikiwa na vitabu kadha ambavyo nimeviandika.. Ninaelewa kuwa singeyafanya hayo kama singekuwa na huyu mtoto. Tumensafiri sana, alisaidia kukutana na watotu wengi. Sam, Worthing.
Niliwalea watoto wawili nchini Japan. Ndiyo ilinigharimu sana kifedha na muda, lakini nimeweza kufanikiwa kitaalumaa. Watoto waliniwezesha kuwa na mipango nadhifu. Kwa ujumla watoto wamerejesha mengi sawa na yale walipewa Bob, Tokyo.

Related Posts:

  • The Hardest Part of Mothering No one warned me. No one told me that after training our children to sleep through the night, after helping them learn the ways of kindness and the value of hard work, after teaching them the joy of reading and the delight… Read More
  • God’s Unexpected Answer to Our Prayers for Revival Doesn’t your heart burn when you read about the early days of the Christian church? “They devoted themselves to the apostles’ teaching and the fellowship, to the breaking of bread and the prayers. And awe came upon every s… Read More
  • Don’t Be Stubborn. Stay Open to Change. “It is better to be a poor but wise youth than an old and foolish king who refuses all advice” (Ecclesiastes 4:13 ).  Men, I hate to say it, but something that many of us have to watch out for is becoming stubborn… Read More
  • Most of Life Is Waiting I wish someone had told me. Looking back now, I wish an older lady had sat me down and told me, “Most of life is waiting, Jani. Learn to wait in hope, not fear.” You see, I grew up believing a lie — a lie I carried with … Read More
  • Peaches in Paradise Why I Loved Elisabeth Elliot Article by  John Piper At 6:15 on the morning of June 15, 2015, Elisabeth Elliot died. It is a blunt sentence for a blunt woman. This is near the top of why I felt such an affection and admiration for her. Blun… Read More