Recent Posts

PropellerAds

Sunday, December 18, 2016

Mugabe kuwania uraisi 2018

Chama tawala cha Zimbabwe kimethibitisha kuwa rais Robert Mugabe ndiye mgombea wake wa uchaguzi wa 2018.
Bw Mugabe ambaye ana umri wa miaka 92 amekuwa madarakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Katika mkutano wa chama hicho, idara ya vijana ya Zanu-PF ilitangaza kuwa Mugabe anafaa kuwa raia wa maisha .
Hatahivyo kumekuwa na maadamano mwaka huu dhidi ya uongozi wa kiongozi huyo pamoja na hali mbaya ya kiuchumi inayokumba taifa hilo.
Chama cha Zanu-PF pia kimekabiliwa na makabiliano ya wenyewe kwa wenyewe huku makundi hasimu yakipigania kumrithi rais Mugabe wakati atakapoondoka afisini.
Wafuasi wake waliimba tongai, tongai, tongai baba wakimaanisha endelea kuongoza baba huku mkutano wa chama hicho ukimchagua Mugabe kuwa mgombea wake wa urais katika mji wa kusini mashariki wa Masvingo.