Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Tanzania (NIMR), Dkt Mwele Malecela, ambaye alitangaza kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania, amefutwa kazi.
Taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu Gerson Msigwa inasema Rais wa John Magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi huyo mkuu.
Taarifa hiyo hata hivyo haijaeleza sababu ya kufutwa kazi kwa Dkt Malecela, siku moja tu baada yake kutangaza kwamba kuna virusi hiyo.
Hata hivyo, kulikuwa kumetokea habari za kukinzana kutoka kwake na wizara ya afya kuhusu kuwepo kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
Alitangaza kuwepo kwa virusi hivyo nchini Tanzania siku ya Alhamisi lakini Ijumaa, baada ya habari hizo kuenea kwenye vyombo vya habari, waziri wa afya Ummy Mwalimu akatoa taarifa kukanusha habari hizo.
Njia 10 za kujikinga dhidi ya virusi vya Zika
Dkt Malecela akithibitisha kupatikana kwa Zika Tanzania
"Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR atakayejaza nafasi iliyoachwa na Dkt Mwele Malecela utatangazwa baadaye," taarifa hiyo inasema.
Dkt Mwele Malecela alikuwa ametangaza kwamba virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Kwa mujibu wake, virusi hivyo viligunduliwa wakati wa utafiti uliofanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.
Tanzania yapata maabara ya kipekee
Kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti huo, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi vya Zika.
Hata hivyo wizara afya nchini humo, ilitoa taarifa ambapo inakanusha kuwepo kwa virusi hivyo.
"Kama nilivyoeleza mnamo Februari 2016, ugonjwa huu bado haujaingia nchini, na leo pia napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa kwa sasa Tanzania haujathibitishwa kuwepo na ugonjwa wa Zika," taarifa ya wizara ya afya imesema.
Virusi hatari vya Zika vyafika Afrika
Wizara hiyo inasema uchunguzi uliofanywa na NIMR ulikuwa wa kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya Zika na Chikungunya.
"Matokeo haya bado yanahitaji kuchunguzwa kwa kina zaidi kupitia vipimo vilivyothibitishwa na Shirika la Afya Duniani," wizara ilisema.
Asili ya Zika
Jina la virusi hivyo linatokana na msitu wa Zika, Uganda ambapo virusi hivyo vilitambuliwa kwa mara ya kwanza 1947.
Wengi wa walioambukizwa aina ya awali ya virusi walikuwa wakipatwa na homa ambayo si kali sana, mwasho na maumivu katika maungio.
Watanzania hutafuta nini mtandaoni?
Lakini kwa aina ya sasa, ambayo mlipuko wake ulianza mwishoni mwa mwaka 2015 nchini Brazil, dalili zake zimekuwa kali na virusi hivyo vinaaminika kusababisha kudumaa kwa ubongo na kasoro nyingine mwilini.
Historia ya kuenea kwa virusi vya Zika
1947: Wanasayansi wanaotafiti kuhusu homa ya manjano msitu wa Zika, Uganda wagundua virusi hivyo kwenye tumbili.
1948: Virusi hivyo vyapatikana kutoka kwenye mbu aina ya Aedes africanus msitu wa Zika
1952: Visa vya kwanza vya binadamu kuambukizwa virusi vya Zika vyaripotiwa Uganda na Tanzania
1960-80: Virusi vya Zika vyapatikana kwenye mbu na tumbili maeneo ya kati Afrika
1960-80: Virusi vya Zika vyapatikana maeneo yenye misitu na mvua nyingi Asia, ikiwemo India, Indonesia, Malaysia na Pakistan
2007: Virusi vya Zika vyaenea nje ya Afrika na Asia, kwanza katika visiwa vya Yap kwenye bahari ya pasifiki
2012: Watafiti wagundua aina mbili tofauti za virusi vya Zika, virusi vyenye asili Afrika na vingine vyenye asili Asia
Machi 2, 2015: Brazil yaripoti visa vya watu kuugua kutokana na maambukizi ya virusi vya Zika
Julai 17: Brazil yaripoti visa vya watoto kuzaliwa na ubongo uliodumaa na vichwa vidogo
Okt. 30: Visa vya watoto kuzaliwa an vichwa vidogo Brazil vyaongezeka
Novemba 2015-Januari 2016: Visa vya Zika vyaripotiwa Suriname, Panama, El Salvador,
Mexico, Guatemala, Paraguay, Venezuela, French Guiana, Martinique, Puerto Rico,
Guyana, Ecuador, Barbados, Bolivia, Jamhuri ya Dominika, Nicaragua, Curacao,
Na Jamaica
Feb. 2, 2016: Kisa cha kwanza cha Zika kuenezwa Marekani charipotiwa, kikidaiwa kutokana sana na ngono badala ya kuumbwa na mbu.
Mei 20: WHO yatangaza kupatikana kwa virusi vya Zika kwa mara ya kwanza Afrika kipindi cha sasa cha mlipuko, katika visiwa vya Cape Verde. Virusi hivyo ni vya aina sawa na virusi vilivyosababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Brazil.
Agosti 3, 2016: Wataalamu Marekani watangaza kuanza kwa majaribio ya chanjo dhidi ya Zika.
Australia yapendekeza kupiga marufuku mitandao ya kijamii kwa watoto chini
ya miaka 16
-
Serikali ya Australia imewasilisha muswada wa sheria Bungeni unaopendekeza
kupiga marufuku Watoto chini ya miaka 16 kutumia Mitandao ya kijamii na
Kampun...
3 minutes ago