Sasa wanasayansi wanadhani kuwa, wanajua sababu, ya vifungo hivyo kufunguka.
Wamebaini
kuwa nguvu ya miguu kukanyaga ardhi, huvuta na kisha hulegeza kifundo
cha kamba kilichofungwa, sawa na mkono usioonekana, ukifungua kamba hizo
taratibu.
Watafiti wanasema kuwa uelewa huu wa namna kamba za viatu hufunguka, uko sambamba na namna DNA inavyofanya kazi.
Kwa
kutumia camera inayonasa na kuwasilisha picha kwa mwendo wa pole, na
mfululizo wa majaribio, wahandisi wa mitambo katika Chuo Kikuu cha
California Berkley, wamepata kuwa "kushindwa kwa kifungo cha kamba"
hufanyika kwa sekunde kadhaa, inayochochewa na nguvu kadha wa kadha.
Mtafiti
mkuu Christopher Daily-Diamond, anasema kuwa: "unapozungumzia aina ya
vifundo, ikiwa utaweza kuanza kuelewa kamba ya viatu, bila shaka
utatumia mbinu hiyo hiyo, kwa vitu kadhaa, kama vile DNA au namna kitu
kinapojiunda na kuweza kuonekana tu kwa uwezo wa mtambo wa microscope,
chini ya nguvu imara.
"Hii ni hatua ya kwanza kuelewa, namna vifungo vingine huwa bora kuliko vingine, ambayo hakuna mtu ambaye amewahi kufanya."
Utafiti
huo ulianza kwa ushirikiano wa uasisi na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu
Christine Gregg, alifunga viatu vyake vya kukimbilia na kufanyia
mazoezi kwenye kifaa cha eneo la mazoezi au Gym, huku mwanafunzi
mwenzake akipiga picha ya video.
Kutokana na nguvu hiyo, kifundo hicho hujinyosha na kujikunja tena.