Mwanamke mmoja katika jimbo la Ohio
nchini Marekani ameshtakiwa kwa kum'baka
dereva mmoja wa teksi kwa kutumia kisu
kabla ya yeye na mwanamume mwengine
kumuibia kulingana na maafisa wa polisi.
Brittany Carter mwenye umri wa miaka 23,
anadaiwa kufanya tendo la ngono na dereva
huyo mwenye umri wa miaka 29 huku Corey
Jackson mwenye umri wa miaka 20
akimshikia kisu shingoni.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wawili
hao waliiba dola 32 kutoka kwa mwathiriwa
kabla ya kutoroka katika eneo la mkasa
katika mji wa Findlay.
Hatujui ni kwa nini alifanya hivyo,luteni wa
polisi Robert Ting alisema.Pengine ilikuwa
hali ya kumpumbaza kwa sababu pia
walimuibia pesa .
Unyanyasaji huo ulitokea baada ya bi Carter
kumuita dereva wa teksi hiyo ya kampuni ya
Trinity Express Cab mapema mnamo tarehe
28 mwezi Januari, kulingana na maafisa wa
polisi.
Alikamatwa baada ya dereva kuripoti kisa
hicho .
Bi Carter anakabiliwa na shtaka la ubakaji
pamoja na lile la uhalifu katika mahakama
ya kaunti ya Hancock.
Alishtakiwa mara mbili kwa makosa ya dawa
za kulevya mwaka 2016 na anadaiwa
kumiliki dawa ya kulevya aina ya heroine.
Bi Jackson hajakamatwa huku agizo la
kukamtwa likitolewa kulingana na polisi.
Anashtakiwa kwa kuchochea wizi na njama
ya kutaka kufanya ubakaji.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo January 22, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania January 22,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetini...
6 hours ago