Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, April 12, 2017

Simu zinaweza kufichua siri kuhusu maisha yako

Simu za fichua siriChembechembe zinazopatikana kwenye simu za mikononi zinaweza kuashiria kiwango cha afya na maisha ya mmiliki, ikiwemo matibabu na aina ya chakula anachopendelea.
Wanasayansi kutoka California waligundua chembechembe za kafeini pamoja, dawa za kupunguza msongo wa mawazo na vipodozi vya ngozi kwenye simu 40 walizozichunguza.
Utafiti unaonyesha kuwa hata kunawa mikono mara kwa mara hakutazuia kusambaa kwa chembechembe hizo katika vitu vingine.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha California kilichopo mjini San Diego, wamefanya tafiti za sampuli 500 kutoka kwenye simu 40 za watu wazima na mikono yao.
Dkt Amina Bouslimani ambaye ni mwanasayansi msaidizi katika utafiti huo alisema matokeo yalionyesha kuwa inawezekana kupata maelezo ya kina kumhusu mtu kutoka kwenye simu,
''Kwa kuchunguza chembechembe zilizoachwa kwenye simu zao...tunaweza kubaini iwapo mtu ni mwanamke, na anatumia vipodozi, na kupaka rangi nywele zake, anakunywa kahawa na, anapendelea bia kuliko divai, anapenda kula vizuri, anatibiwa msongo wa mawazo, anaikinga ngozi na jua, kupulizia marashi, mara nyingi hupenda kutumia muda wake mwingi nje ya nyumba …. na vitu vingine kama hivyo,'' alieleza.
Mara nyingi Chembechembe hizo zinaweza kutoka kwenye ngozi na jasho la mikononi kwenda kwenye simu za watu.
Dawa za mbu na zile za kuzuia miali ya jua zimekuwa zikidumu kwa muda mrefu kwenye ngozi na kwenye simu hata kama hazijatumiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Tafiti zilizopita zilizofanywa na watafiti haohao zinaonyesha kuwa hata kama mtu hajanawa kwa siku tatu hivi, bado ataonekana kuwa msafi na mrembo.
Utafiti unaonyesha uchunguzi wa simu unaweza kutumiwa:
  • Kuonyesha mmiliki wa kifaa bila kutumia alama za vidole.
  • Kuangalia kama mtu alikuwa anatumia dawa
  • Kutoa taarifa sahihi za mtu husika kama ameshika uchafu.
Mtafiti anataka kujua zaidi juu ya wingi wa bakteria walioko kwenye ngozi zetu na wanaanisha nini kuhusu sisi.
Mwandishi mkongwe prof Pieter Dorrestein amesema kuwa mwili wa binadamu una bakteria ambao si chini ya 1000 tofauti tofauti katika sehemu mbalimbali za mwilini.