Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, April 12, 2017

Waafrika wanauzwa Libya katika biashara ya utumwa

Raia wa Afrika wanaojaribu kuvuka na
kuelekea barani Ulaya, wanauzwa na watekaji
wao na kuuzwa katika "soko la utumwa"
nchini Libya. Hayo yamesemwa na shirika la
kuwahudumia wahamiaji duniani
International Organization for Migration
(IOM).
Wahasiriwa wameiambia IOM kuwa, baada
ya kuzuiliwa na walanguzi wa biashara ya
watu au makundi ya wapiganaji,
wanapelekwa hadi kwenye viwanja vya mji
au kwenye maeneo ya kuegeshea magari na
kuuzwa.
Wahamiaji walio na ujuzi kama vile upakaji
rangi au ukulima, wanauzwa kwa bei ya juu,
kiongozi mkuu wa shirika hilo la IOM nchini
Libya ameiambia BBC
Libya imekuwa katika ghasia tangu mwaka
2011 pale wanajeshi wa shirika la kujihami
la mataifa ya magharibi-NATO
yalipomuondoa madarakani Rais wa nchi
hiyo Kanali Muammar Gaddafi.
Kwa mjibu wa IOM, maelfu ya wanaume
chipukizi kutoka mataifa ya kusini mwa
jangwa la Sahara wameuzwa katika masoko
hayo ya utumwa wa binadamu.
Mhamiaji mmoja kutoka Senegal, ambaye
jina lake limebanwa ili kumlinda, amesema
kuwa amewahi kuuzwa katika masoko kama
hayo katika mji wa Sabha kusini mwa Libya,
kabla ya kuwekwa katika gereza moja bovu,
ambapo zaidi ya wahamiaji 100 walikuwa
wakizuiwa.
Amesema kwamba, wahamiaji wanaozuiliwa
waliambiwa kuwapigia simu familia zao,
ambao waliulizwa kutoa fedha ya kikombozi
ili waachiwe huru, na baadhi yao wakapigwa
wakiwa bado wanazungumza kwenye simu,
ili kuwafanya jamaa zao wasikie wakiteswa
ili watume haraka fedha hizo.
Ameelezea kuwa ni matendo ya "kutisha"
ambapo wahamiaji walilazimishwa kuhimili
kula kiwango kidogo mno cha chakula, lakini
kwa wale wasioweza kulipia wanauwawa au
wanaachwa ili wafe njaa, ripoti hiyo
inaongeza.
Mfanyikazi mmoja wa IOM nchini Niger,
amesema kwamba ripoti ya biashara ya
utumwa nchini Libya ni ya hakika, baada ya
kuzungumza na wahamiaji waliotoroka
kutoka kambi za kuwazuilia wahamiaji.
"Wote walielezea hatari ya kuuzwa
walipokuwa wamezuiliwa kwenye viwanja na
karakana za magari huko Sabha, aidha na
madereva wao au wenyeji wanaowaandikisha
wahamiaji kufanya vibarua vya kila siku mjini
humo, wengi wao kama wajenzi.
"Baadaye, badala ya kulipwa, wanauzwa kwa
wanunuzi wapya."
Baadhi ya wahamiaji, wengi wao kutoka
Nigeria, Ghana na Gambians
wanalazimishwa kufanya kazi" kama walinzi
katika majumba ya kupokea fedha za
kikombozi au katika 'soko lenyewe",
mfanyikazi huyo wa IOM aliongeza.

Related Posts:

  • Sudan Kusini:Idadi ya waliouawa haijulikani Ripoti kutoka mji mkuu wa Sudan Kusini Juba ,zinasema kuwa mili mingi imepelekwa katika hospitali kuu ya mji huo baada ya ufyatulianaji mkali wa risasi kuibuka karibu na nyumba ya rais siku ya Ijumaa. Idadi ya watu walio… Read More
  • Messi ahukumiwa ‘kufungwa miezi 21 jela’ Mchezaji nyota wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela baada ya kupatikana na makosa ya kutumia ulaghai wakati wa ulipaji ushuru, vyombo vya habari nchini Uhispania vinaripoti. Babake,… Read More
  • Mtandao unaowaunganisha wapenzi wa Kiislamu wadukuliwa Maelezo ya kibinafsi ya takriban wanachama 150,000 wa mtandao unaowaunganisha wapenzi wa Kiislamu umewekwa wazi mtandaoni. Zaidi ya ujumbe 700,000 za kibinafsi kati ya wanachama zimefichuliwa. Ujumbe katika mtandao huo uli… Read More
  • Mamba anayebashiri matokeo ya uchaguzi Australia Gazeti moja nchini Australia limedai kwamba kuna mamaba anayeweza kubashiri matokeo ya uchaguzi nchini Australia. Gazeti hilo la Northern Territory News ni maarufu kwa habari zake katika ukurasa wake wa kwanza. Huku raia w… Read More
  • Magonjwa ya akili yakithiri Sudan Kusini Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema maelfu ya raia wa Sudan Kusini wanasumbuliwa na kiwewe baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, na walio wengi hawana matarajio ya kupata t… Read More