Recent Posts

PropellerAds

Monday, June 12, 2017

Je? wajua ufunguo wa maisha yenye ufanisi

  Image result for wisdom picture
Biblia imeweka wazi kwamba, watu wamjuao Mungu wao watatenda mambo makuu. Ufunguo wa maisha yenye ufanisi upo katika kupata maarifa, ufahamu na kujua hekima ya jinsi itupasavyo kuenenda ili kuishi maisha ya ushindi katika Kristo Yesu. Ili kuona na kuishi ushindi katika maisha yetu ya kila siku itategemea na kiwango cha maarifa na ufahamu wetu juu ya “siri” za ufalme wa Mungu. Hakuna njia ya mkato katika hilo. [Mithali 4:7-9]

Mara kadhaa utasikia wapendwa wakisema “shetani kajiinua”, swali ambalo huwa nawauliza watu wengi kila mara ninapopata nafasi ya kuzungumza nao juu ya Habari  za Ufalme wa Mungu  ni kwamba, wakati shetani anajiinua, Mungu wao huwa anakuwa wapi? Inasikitisha kuona watu wa Mungu wanakuwa waathirika (victims) wa mazingira/shetani sawa sawa na watu wasio mjua Mungu; nao wanalalamika na kunungunika kila kukicha. Kwa sehemu kubwa hali hii inatokana na kukosa maarifa ya Neno la Mungu.
“Ikiwa Yesu Kristo ndiye aliyekuweka huru, hakuna anayeweza kukuweka katika utumwa tena. Ikiwa ni Kristo ndiye aliyekubariki, hakika hakuna anayeweza kukulaani.”
Ukweli ni kwamba, Mungu Baba ametuhamisha kutoka katika nguvu za giza, na kutupeleka katika Ufalme wa mwana wa Pendo Lake. Hii ina maana kwamba, mtu akiwa ndani ya Kristo hayupo tena chini ya himaya ya ufalme wa giza. Ikiwa Yesu Kristo ndiye aliyekuweka huru, hakuna anayeweza kukuweka katika utumwa tena. Ikiwa ni Kristo ndiye aliyekubariki, hakika hakuna anayeweza kukulaani. Tukiijua kweli, kweli itatuweka huru na hakuna atakayeweza kuchukua uhuru wetu.
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa…” Hosea4:6
Watu wengi wanaujua mstari huu wa Hosea 4:7 na tena wameukariri vizuri kichwani, lakini si watu wengi wanaelewa uzito wa maneno hayo. Hakuna mahali biblia inasema, watu wanaangamizwa kwa sababu ya uwepo wa shetani katika maisha yao. Adui mkubwa wa mwanadamu sio shetani au mapepo. Adui mkubwa wa mwanadamu ni ukosefu wa maarifa sahihi (Ignorance). Unaweza kukemea pepo kwa Jina la Yesu na likamuachia mtu saa hiyo hiyo, lakini hauwezi kukemea ujinga (ignorance). Silaha pekee ya kuondoa “ujinga” ni kwa kupata maarifa na ufahamu sahihi. Mungu alinena kwa kinywa cha Nabii Isaya kwamba, “kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheowana njaa, na wengi wao waona kiu sana” Isaya 5:13
Tujifunze kwa Joshua
Mafanikio ya Joshua katika njia yake, hayakuwa katika mikono ya Mungu bali katika m ikono yake mwenye. Mungu alishafanya kila kinachotakiwa kufanyika ili Joshua anaweze kufanikiwa. Maneno haya, maana ndipo utakapoifanikisha njia yako yanatupa kujua kuwa mafanikio ya Joshua hayakutegemea mazingira yake, jamii yake, historia yake bali yalitegemea utayari wake katika kutenda na kufuata maagizo ya Mungu katika maisha yake.
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapostawi sana” Yoshua 1:8
Wakati Fulani nikiwa kidato cha nne nilikuwa nasumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara kwa muda mrefu, nakumbuka nikiwa kwa shangazi yangu siku moja niliamua kupekua mavitabu yaliyokuwa yamewekwa bila mpangilio kwenye boxi, ili nione kama nitapata kitabu cha kusoma, baada ya kupekua kwa muda nikakutana na kitabu cha Dr. David Oyedepo, kilichokuwa kimeandikwa “Ufunguo wa Afya ya Ki-ungu” baada ya kukisoma kitabu hicho kilichokuwa kimechakaa na kimeanza kuchanika, ndio ulikuwa mwanzo wa kuishi maisha ya afya bila kusumbuliwa na magonjwa mpaka leo.
“Ikiwa tutasoma Neno la Mungu na kusiwepo na badiliko lolote katika maisha yetu basi tunapoteza muda bure, ni sawa na kukimbiza upepo”
Mwenyehekima mmoja amewahi kusema “The cheapest way to secure a great future is to have great investment in knowledge” (Njia rahisi ya kuwa na maisha yaliyotukuka ni kuanza kuwekeza katika maarifa sasa). Amua kuwekeza muda wako na rasilimali zako katika kupata maarifa sahihi.  Tenga muda wa kujifunza Neno la Mungu, tenga muda wa kusoma vitabu sahihi visivyopingana na Neno la Mungu. Usisome tu kama burudani au kutimiza ratiba ya kusoma biblia au kitabu, Nuia kupata maarifa kila usomapo na jizoeze kumuomba Roho Mtakatifu ili akujalie kupata uelewa kila usomapo. Ikiwa tutasoma Neno la Mungu na kusiwepo na badiliko lolote katika maisha yetu basi tunapoteza muda bure, ni sawa na kukimbiza upepo.