Recent Posts

PropellerAds

Monday, June 12, 2017

msimdharau mshindani wako

Don’t underestimate your rival
Image result for Don’t underestimate your rival 
Ikiwa mhitimu wa chuo kikuu ataambiwa ajiandae kwa mtihahi wa darasa la kwanza, nadhani maandalizi pekee atakayofanya ni kwenda kwenye huo mtihani ambao unaonekana ni wa chini sana ukilinganisha na kiwango chake cha elimu. Lakini ikiwa ataambiwa atafanya mtihani au unaofanana na elimu yake au zaidi bila shaka atajiandaa sana.

Mshindani wako au adui si lazima awe mtu inaweza ikawa ni hali fulani (situation/condition). Inaweza ikawa ni hali ya umasikini, hali ya ugonjwa, kutokukubalika au vinginevyo. Mshindani wako inawezekana ikawa ni tofauti ya mahali ulipo na pale unapotaka kwenda. Yote kwa yote ni lazima tujizatiti, taking this battle very serious!

Ukijua kwamba mpinzani wako ni mwepesi (si lazima awe mtu) unaweza kufanya maandalizi mepesi na ndio chanzo cha kuangamia kwako. Unadhani nini kinatokea kwa wanaojua kwamba, kesho watashindana na mwanadamu mwenye kasi zaidi yaani Usain Bolt? Si siri watajiandaa sana, wanajua mpambano ni wa kufa na kupona.

Nini kinatokea kwa mzungumzaji anapojua katika mjadala huo atakuwapo Rais mstaafu wa Marekani Barrack Obama pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Ni wazi mzungumzaji atajipanga vilivyo, nini aseme na nini asiseme. Ukijua utazungumza mbele ya TD Jakes lazima ujipange. Ukijua kwamba kesho utapambana na Mike Tyson (wakati wa zama zake) na hujajiandaa vizuri, naamini utaomba udhuru kuliko kuweka maisha yako rehani. Preparation is a key!

Maisha nayo yako hivyo tunapaswa kuyaendea kwa kujiandaa kufa na kupona. Ukiwa shuleni soma, kazini fanya kazi kwa bidii, katika biashara pia ni vizuri kuwa na weledi wa kutosha. Ukiyadharau maisha ukisema ndege wa angani wanakula, tutakusubiri tukuone na wewe kama utaruka kwa mbawa. Tutasubiri tuone kama na wewe utaingia kwenye mashamba ya watu bila kibali kama ndege.

Kufurahia maisha haina maana kutokujizatiti kufanya vizuri na kuishi hadhi ya juu. Si kila mwenye nguo yenye kiraka ni bahati mbaya, wengine wanapata malipo ya kazi yao. Wakati wenzao wanasoma wao walilala, wakati wenzao wananunua mashamba wao waliongeza mke wa pili, wakati wenzao wanakwenda mazoezini wao walikwenda kulewa pombe.

Usiyachukulie maisha haya kirahisi, chukua wajibu wa kuyapanga na kupangilia. Wapenda hadithi mnakumbuka hii, Sungura alipomtazama kobe alimchukulia kirahisi sana. Sungura alimdharau kobe akiona hawezi kushindana naye katika riadha, hii ilipelekea sungura kucheka sana kwa nini apambane na kobe. Mbio zilipoanza sungura alikimbia kwa kasi na alivyogeuka nyumba aliona kobe yuko pale pale, Sungura kwa dharau akaamua kulala. Hatimaye usingizi wa pono ukamkuta sungura, na hatimaye kobe akampita na kutwaa ushindi. Japo kobe alikuwa taratibu alikuwa akimaanisha kushindana na alikuwa amejizatiti kweli kweli. Somo, usiwe kama sungura, take this life very serious!