Katika kitabu
cha Hosea 4:6 imeandikwa “watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa…”
Inawezekana umesikia mara nyingi sehemu hii; swali ambalo nataka tujiulize kwa
pamoja na kulitafakari ni, je kwanini Mungu hamzuii au hajamzuia muangamizaji
wa watu wake? Kumbuka hawa wanauhusishwa hapa si wapagani bali ni watu wa
Mungu; hivyo swali linabaki kwanini Mungu hajamzuia mwangamizaji na ameacha
mpaka wanaangamizwa?
Isaya anandika,
“Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na
maarifa;...” Isa5:13. Hapa pia nataka tujiulize kwa pamoja, kwanini Mungu
hakumzui mtekaji au watekaji mpaka watu
wake wanatekwa? Kwanini watu wake wanatekwa mbele yake na ameacha mpaka wamechukuliwa
mateka?
Dr. David
Oyedepo amewahi kusema, “God cannot help you and I beyond our level of
knowledge of Him” yaani Mungu hataweza kutusaidia zaidi ya kiwango chetu
cha maarifa (ufahamu) tulichonacho (Tafasiri isiyo rasmi). Mpaka umeujua
na kuelewa ‘ukweli’ huu hauwezi kuelewa pale Mfalme Suleimani aliposema na
kusisitiza juu ya kuwekeza katika maarifa na ufahamu, “Bora hekima, basi
jipatie hekima; naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu (wisdom is
supreme, therefore get wisdom; though it may cost all you have get
understanding)”.Mith 4:7
Petro anasema,
uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu VYOTE, lakini tunauwezo wa kuvifikia (experience
in our lives) vitu hivyo kwa njia ya maarifa katika yeye (2Petro1:3, msisitizo
umeongezwa). Kumbuka, Mpaka pale umejitoa kuwekeza katika maarifa na
ufahamu katika eneo husika, hautaweza kubadili nafasi uliopo, iwe katika eneo
la elimu, uchumi, biashara, uongozi, uhusiano, kazini.. N.k (Until you give
yourself to the investment in knowledge and understanding, you won’t change
your position)
Uwekezaji
katika maarifa unahitaji uwekezaji wa muda, juhudi na rasilimali zingine
ili kupata matokeo bora katika maisha yetu ya kila siku. Mpaka umewekeza katika
maarifa, maisha yako yanabaki kuwa mawindo mepesi kwa muangamizaji na mtekaji.
Ni ‘kweli’ ulioijua pekee katika eneo husika (specific) ndio
itakayokufanya au kuwezesha kuishi huru katika eneo hilo. Yh 8:32! Kumbuka,
maombi hayawezi kubadili sehemu ya maarifa; kama eneo hilo linahitaji maarifa
ili uweze kuvuka, hata kama utafunga na kuomba bila maarifa hayo hauwezi
kubadili mahali ulipo (Prayer cannot replace the role of understanding and
knowledge)!
Mwenyehekima
mmoja anasema, asilima kubwa ya changamoto alizonazo mtu majibu yake yapo
kwenye vitabu na semina mbali mbali ambazo alikuwa na nafasi ya kuyafikia
maarifa lakini hakufanya hivyo kwa sababu yoyote ile.