Kila mmoja wetu ana namna
yake ya kufikiri na hizi namna tofauti za kufikiri ndizo ambazo
zinatutofautisha binadamu. Ni tofauti hizi pia ambazo zinatufanya tuwe na
tofauti katika mafanikio maishani mwetu. Wale ambao wanafikiri vizuri na
kuamini katika kumudu, huwa wanafanikiwa. Wale ambao wanafikiri vibaya na
kiamini katika kushindwa, siku zote huwa wanaanguka.
Huenda ni vigumu kwa mtu
kujua, huku kufikiri vizuri na kuamini katika kumudu ni kupi na pia huku
kufikiri vibaya na kuamini katika kushindwa ni
kupi. Kwa bahati nzuri hayo yote yameelezwa kwenye mada nyingine
zinazohusu kufikiri kitabuni humu. Kwa bahati nzuri zaidi, wataalamu wa masuala
ya mawazo na mafanikio kama John Gray, Vincent Peale, Anthony Robbinins na
wengine, wanabainisha vigezo ambavyo vinaweza kumfanya mtu kutabiri kama maisha
yake yatakuwa ni ya kushindwa hadi mwisho au yatakuwa ni ya mafanikio.
Mwana mama Rhonda Byrne
kwenye kitabu chake cha ‘The Secret’ ameeleza kwamba, kama mtu akiwa anaamini
kwamba kuna watu wengine wa aina fulani mahali fulani, ambao ndio peke yao
wanaoweza kufanikiwa na kufika juu kwenye ngazi ya kimapato, mtu kama huyo
hawezi kamwe maishani mwake kuja kutoka kwenye lindi la umaskini.
Rhonda, ambae aliishi maisha
ya hali ya chini nayakutisha,anafafanua kwamba, mtu akiwa na mtazamo huo, hawezi
kutoka kwenye lindi hilo kwa sababu juhudi zake ambazo zingemfikisha mbali
zinakuwa tayari zimewekewa mipaka na imani hiyo, kwamba yeye hahusiki katika kufanikiwa, bali kuna wengine ambao ni
Mungu mwenyewe anayewajua na
aliyewateua. Kwa kufikiri hivo, juhudi yake kubwa katika kutafuta itakuwa ni ile ya kumfanya
asife tu kwa njaa na siyo kuvuka hapo. Kama ujuavyo, tunapoamini kuhusu jambo
Fulani, mawazo yetu hutusaidia kulifikia jambo hilo.
Kwa kuamini hivyo, mazingira
tunayojenga ni yale ya kutusaidia kuishi kwa kupata riziki tu. Hata kama “fuko
la fedha” litadondoshwa miguu mwetu tutalipiga teke na kuliambia “mimi
sikuandikiwa kupata bwana, kuna wenyewe, hali kama hii hujitokeza mara nyingi
sana maishani mwetu. Tunakabidhiwa dhamana kubwa ambayo ingetusaidia sana
maishani mwetu, lakini tunacheza nayo hadi inapotea kwa sababu tu hatuamini
kwamba utunastahili kuitumia kufika juu. Tunaziona nafasi za kusonga mbele,
lakini tunaamini kwamba, hatustahili kuzitumia.
Fursa zikija waziwazi kabisa,
tunajifanya hatuzioni kwa kutafuta visingizio mbalimbali ili tusizitumie, kwa
sababu tu, tumeamini kwenye mawazo yetu kwamba, sisi hatustahili. Ni vigumu
kugundua kwamba nafasi au fursa hizo zimekuja kwa sababu tayari tumejifungia
njia kuelekea mafanikio. Wengine kwa bahati baya wanaweza kuona na kubaki
wameshangaa ni kwa nini tushindwa kuinuka katika mazingira tuliyomo.
Mtu ambaye anaamini kwamba
hawezi, yaani ameshashindwa kutokana na sababu mbalimbali, anaelezwa na
wataalamu wa elimu ya mafanikio kwamba, kamwe mtu huyu hawezi kuja kuvuka
kizingiti cha umaskini. Kuna watu ambao kutokana na sababu mbalimbali
walifanywa kuamini kwamba hakun wanchoweza. Wengine kutokanana malezi,
mazingira au uzoefu mbalimbali wa kimaisha.
Mtu anapoamini kwama hawezi,
anayaambia mawazo yake ya kina yamsaidie kumfanya ashindwe zaidi kwenye kila
jaribio analofanya. Badala ya kufanya juhudi kujisaidia ili amudu, hujipweteka
kwa kuamini kwake kwamba hata kama atafanya kitu gani, kamwe hatamudu. Siyo
rahisi kwa mtu mwenye mawazo ya aina hii kuweza kufanikiwa maishani.
Kuna watu ambao kwa sababu
ya kukosa kile ambacho jamii inakiona kuwa ndiyo ufunguo wa mafanikio, huwa
wanaamini kwamba hawawezi kufanikiwa au kufanya vizuri maishani kama hao ambao
wanacho. Kwa mfano, kwa kukosa elimu, ujuzi au utaalamu fulani, watu wengine
hujihesabu kama wanyonge. Huchukulia kwamba ni wale tu wenye elimu, ujuzi na
utaalamu fulani ndiyo wanaoweza au wanaotakiwa kufanikiwa.
Bila shaka umeshawahi
kusikia au hata wewe mwenyewe kusema, “Si wamesoma bwana’ ndiyo wanaojaliwa,
sisi ambao hatuna elimu kazi yetu itakuwa ni kuwatumikia. Kauli kama hizi zina
chimbuko lake mbali sana, pengine katika malezi yetu. Wazazi kwalizoea au
wamezoea kuwaambia watoto wao, “Usiposoma kazi yako itakuwa ni kuwabebea
wenzako mizigo, unafikiri pesa inaokotwa, nk. Kwa bahati mbaya mtoto aliyelishwa “sumu” (‘EARLY CHILD PROGRAMMING’) hii
anaposhindwa shule, huamini kwamba yeye atabaki kuwatumikia wengine tu.
Tunapoamini kwamba kwa sababu
hatuna elimu ya kutosha napengine ujuzi au utaalamu Fulani, hatuwezi kufika juu
kwenye mafanikio, ni wazi hatutafika. Moja ya vigezo muhumu vinavyoweza kutufikisha kwenye mafanikio ni kuamini kwetu
kwamba tunaweza kufika huko. Tunapokuwa hatuna imani kwamba tunaweza kufika
huko hujifungia njia wenyewe.
Baadhi yetu kuwa tunaamini
kwamba tuna mikosi, balaa au nuksi napengine laana ambazo zinatuzuia katika
kufikia malengo yetu. Tunaamini hivyo kiasi kwamba hata tukifikia karibu kabisa
na mafanikio huwa tunajiambia ni kazi bure, tutaporomoka tu. Na kweli kwa
kuamini hivyo hujikuta tukiporomoka kila tukifika karibu na kufanikwa au kufikia
malengo.
Kinachotokea ni kwamba, kwa
kuamini kwetu kuwa tunamkosi, balaa, laana au nuksi, huwa tunatenda kwa mkabala
huo wa kinuksi au kibalaa na kimkosi, ambapo matokeo yake ni kujikwamisha.
Watalaamu wa elimu ya mafanikio wanaeleza kwamba tunapoamini kuwa tuna mkosi au
nuksi huwa tunayashauri mawazo yetu ya kina kutusaidia kuendelea kuwa katika
hali hizo (Niliwahi kufafanua zana hii nilipoandika makala ya BINADAMU NI ZAIDI YA
MWILI WAKE). Ndiyo maana siyo rahisi
kukuta mtu anayeamini katika nuksi akiondoka katika hali hiyo.
Tufanyeje basi, kama ni
kweli kimapato tuko hoi napengine tunachoweza ni kupata riziki yetu ya kila
siku tu? Pamoja na kwamba mengi yameelezwa
tayari kwenye mada nyingine, bado tunaweza kukuambia, tunachotakiwa
kufanya ni kujenga imani ya kumudu. Kamwe hatutakiwi kabisa kujiambia
tulipofikia ndipo basi, hatuwezi kupanda zaidi.
Yupo mjasiliamali fulani,ni dada mpambanaji (Elizabeth Samoja) kwenye ujasiriamali alipata kuandika hivi, maisha ya kijana wa kitanzania aliyechagua kuishi Dar es salaam baada ya kumaliza masomo yake ya chuo kikuu huwa hayaelewiki,(ingawa kwa mtazamo wake yanaeleweka) utashangaa kijana huyu anapomaliza chuo anaanza zungusha cv ndani ya bahasha ya kaki,mtaa kwa mtaa,jingo kwa jingo,atapata kazi kampuni ya simu,au bank,au kampuni ya bia, atapanga chumba mitaa ya sinza, wengine huchukua mkopo na nunua gari aina ya vitis,corora,corona, opa, ama gari lolote lisilozidi milioni kumi, ataoa amakuolewa,atafanya shopping Mr Price, mjanja mwingine atakopa hela za kwendea ‘sendoff’ na wengi wao wakijitahidi hununua mariedo, atavaatai kubwa na kuonekana smart, ataenda club, kuponda raha...
Ukiungalia mlolongo huu vizuri,shughuri nyingi hapo kati zote zinachukua pesa mfukoni mwa ila chanzo cha pato lako ni kimoja tu(ajira), kwa kifupi wewe ni mtumiaji tu....kutoboa kimaisha kwa kufuata mpango huu ngumu sana................
Imefika hatua mpaka mabenki wamejua watanzania si entrepreneurs na investors wanapenda magari ya bei chee,na akijitahidi basi apate nyumba bunju,mbagala,au kitunda.....ndo maana mikopo mingi ya benki wanatangaza kwa kuonyesha nyumba ama gari....maana huko ndo kwenye urahisi na kuna soko na wateja wakubwa maarufu kama ‘victim society’ market. Mtanzania Zinduka......
Usiseme hakuna pesa, pesa zipo nyingi sana, fursa za kumwaga, nina mshangaa huyu mhitimu wa chuo kikuu akiwa mtaani asijue cha kufanya badala yake anaingia kwenye mitandao ya kijamii kama ‘face book na kuanza kumwaga lawama kibao,jiulize umefanya nini,kwani ulikuja duniani ili ubebwe na serikali? Kwa sasa Tupo watanzania milioni 44 wote tukisubiri kubebwa tutakuwa taifa la aina gani hili?