Na;
Damacen Nyemenohi
Kitendo cha Waheshimiwa kushangilia kufutwa kwa ada za magari na kuzihamishia kwenye bei za mafuta ya petroli ni kushindwa kutafakari 'imact' ya bei ya petroli kwa wananchi wa kipato cha chini ambao wengi hawamiliki magari wala mitambo.Ikumkwe kupanda kwa bei ya nishati ni chanzo cha kupanda kwa gharama za usafirishaji wa vitu na watu,na gharama za kusaga nafaka maeneo ya vijijini ambako mashine za kukoboa na kusaga zilizo nyingi zinatumia nishati ya petroli na dizeli.Hapana shaka kwamba wananchi wa kawaida sasa watalazimika kufanya yafuatayo:1)kulipa nauli zaidi ya mwaka uliopita,(2) kukabiliana na bei ya juu katika kukoboa na kusagisha nafaka;(3) kuwalipia wamiliki wa magari 'indirectly' kodi za magari ambayo ada zake zimehamishiwa kwenye bei ya nishati ya petroli,dizeli na mafuta ya taa;(4) kununua bidhaa kwa bei ya juu kutokana na kupanda gharama za usafirishaji.Siibezi mipango ya Dkt.Mpango kwenye bajeti yake bali nadhani alitakiwa kuangalia 'rationally' impact ya kupandisha bei za nishati ya petroli,diseli na mafuta ya taa kama kweli anaangalia kwa macho mapevu Mtanzania wa hali ya chini kikipato.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo January 22, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania January 22,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetini...
6 hours ago