Katika utafiti
wa hivi karibuni, watafiti wamegundua kwamba, wanawake wanawapenda wanaume
wasio waoga na mashujaa kuliko wale waoga. Ushujaa wa wanaume ni kigezo kikubwa
kwa wanawake kuwapenda marafiki wa kiume wa muda mrefu na muda mfupi. Hii
inamaanisha kwamba katika urafiki wa kawaida na wa kimapenzi na wa kindoa, wema
au ukarimu ulionekana kwamba ni kigezo cha kawaida.
Tukirudi kwa mababu zetu wa kale walioishi mapangoni, wanawake waliwapenda wanaume shujaa ambao wangeweza kujitoa muhanga kuwalinda wao na watoto wao. Mwanaume ambaye alikuwa na uwezo wa kujitoa muhanga alionekana kuwa na uwezo wa kuwinda bila hofu na kuzama porini kutafuta chakula kwa Ajili ya familia au kutafuta dawa kwa ajili ya matibabu kwa familia yake.
Bila shaka ushujaa huo kwa wakati huo ulikuwa na maana ya mwanaume kuwa na uwezo wa kuifanya familia ijihisi salama kwa kuhakikishiwa chakula, malazi, mavazi na afya. Kwa maana hiyo, fedha ambayo ndiyo inayotamalaki hivi sasa, ndicho chombo kinachowafanya wengi kuamini kwamba kuwa na fedha inamaanisha wako salama. Kwani huduma zote hizo zinapatikana kwa urahisi pale mtu anapokuwa na fedha.

Kwa hiyo
mwanaume mwenye nazo anaonekana kama ndiye anayeweza kuilinda familia. Ukikuta
wanawake wanavutiwa na wanaume wenye fedha, usishangae, kwani bado wanafuata
ule wito wa asili wa haja ya mwanamke kuhakikishiwa usalama wake.
Kwa maana nyingine ni kwamba
kinachotafutwa na wanawake ni kuhakikishiwa usalama.............Siku hizi
hatuwindi wanyama kama sehemu ya chakula, hatuchimbi miti shamba kwa ajili ya
tiba bali fedha imechukua nafasi katika kujihakikishia usalama wetu........
Kila kitu siku hizi ni pesa na ndio maana wanawake kwa dhana ile ile ya
kujihakikishia usalama wanavutiwa na wanaume wenye nazo........
Sio kwa sababu
ya tamaa......La hasha, ni kutaka kuwa na uhakika na maisha yake na familia
yake baadae, kama akikosa sifa ya fedha ataangalia mwanaume mwenye ujasiri wa
kuthubutu na mchakarikaji, hapo anajua kwamba kwa kushirikiana mbeleni maisha
yatakuwa mazuri na salama................
Ikitokea kwa mfano kaolewa na mwanaume mzigo au siku hizi tunawaita "Dead
alive" Jukumu la kutafuta hulishika mwenyewe kwa sababu hamna jinsi na
mara nyingi hufanikiwa kuzikamata kwa sababu anafanya hivyo kwa nia na dhamira
ya kujihakikishia usalama.
Kama vile wanaume wanavyokosea kuoa kwa
kutopiga hesabu zao vizuri katika kuoa vivo hivyo wanawake nao hukosea kwa
kudanganyika na zile sifa za mwanaume za muda mfupi bila kuchunguza vizuri
zaidi. Wapo ambao wakigundua kwamba mwanaume aliyeolewa naye ni mvivu na
asiyejali familia anafungasha na kuondoka, lakini wapo ambao wanatafuta suluhu
na kuamua kushika hatamu za kuendesha nyumba hawa ni wale wanaoogopa kufanya
makosa kwa mara ya pili yaani kuondoka na kuangukia kwa mwanaume mwingine
mwenye sifa zisizopendeza. Hawa wanakubali matokeo na kuamua kusimama kama wao,
hawayumbishwi na huwakubali wenzi wao kama walivyo.
Wanawake wa aina hii mara nyingi
kufanikiwa sana tofauti na wale wanaojipweteka na kubaki wakilalamika. Lakini
naomba niseme kuwa wanawake kwa kisia kikubwa ni mashujaa hawawezi kukaa na
kuangalia familia ikianguka kwa sababu mwanaume hawajibiki. Wengi sana tena
kiasi cha kutosha husimama na kushika nyumba kwani wanajua kwamba nyumba
ikianguka mara nyingi lawama huwaendea wao.
Kwa mfano wapo wanaume wengi hali
zinapokuwa ngumu huzikimbia familia zao na kuzitelekeza hata kwa miaka kadhaa,
lakini wakirudi wanakuta familia ipo mbali kimandeleo na watoto wana hali
nzuri. Hao ndiyo huitwa wanawake wa shoka.