Si jambo jepesi kulanyama za ndugu zetu wapendwa , lakini kwa nini? Mungu anasema mtakula Nyama za binti zenu na wana wenu. endelea kusoma vifungu hivi vya biblia na utaona na kujifunza.
A.MTAKULA NYAMA ZA WANA WENU NA BINTI ZENU.
Mambo ya Walawi 26:28-30
[28]ndipo katika hasira yangu nitaweka
uadui nanyi, nami mwenyewe nitawaadhibu
mara saba kwa ajili ya dhambi zenu.
[29]Mtakula
nyama ya wana wenu na nyama ya binti zenu.
[30]Nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia
miungu, nitabomoa madhabahu zenu za
kufukizia uvumba na kuzilundika maiti zenu juu
ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami
nitawachukia ninyi sana.
B.UTAKULA NYAMA ZA BINTI ZAKO NA WANA WAKO AMBAO BWANA MUNGU WAKO AMEKUPA.
Kumbukumbu la Torati 28:53-59
[53]Kwa sababu ya mateso yale adui zako
watakayokuletea wakati wa kukuzingira, utakula
uzao wa tumbo lako, nyama ya wana wako na
binti zako ambao BWANA Mungu wako
amekupa.
[54]Hata yule mtu mwungwana sana na
makini miongoni mwako hatakuwa na huruma
kwa ndugu yake mwenyewe au kwa mke
ampendaye au watoto wake waliosalia, 55naye
hatampa hata mmoja wao nyama ya watoto
wake ambao anawala. Kwa kuwa hakuna kitu
kingine kilichosalia kwake katika mazingirwa
makali ambayo adui yako watakuletea kwa miji
yako yote.
[56]Mwanamke ambaye ni mwungwana
sana na makini miongoni mwako, yaani, ambaye
ni makini sana na muungwana kiasi kwamba asingethubutu kugusa ardhi kwa wayo wa mguu
wake, yeye atakuwa mchoyo kwa mume
ampendaye na mwanawe mwenyewe au binti
yake,
[57]kondo la nyuma kutoka kwenye tumbo
lake na watoto anaowazaa, kwa kuwa
anakusudia kuwala kwa siri wakati wa
kuzingirwa na katika taabu zile ambazo adui
yako atazileta juu yako na miji yako.
[58]Kama hutafuata kwa bidii maneno yote ya
sheria hii, ambayo yameandikwa katika kitabu
hiki na kama hutalicha hili jina la fahari na la
kutisha la BWANA Mungu wako,
[59]BWANA
ataleta mapigo ya kutisha juu yako na kwa
wazao wako, maafa makali na ya kudumu,
magonjwa mazito na ya kudumu.
C.NJAA YASABABISHA ULAJI WA NYAMA YA MTOTO.
2Wafalme 6:28-29
[28]Kisha akamwuliza, “Kwani
kuna nini?’’
Yule mwanamke akamjibu, “Huyu
mwanamke aliniambia, ‘Mtoe mwanao ili tupate
kumla leo na kesho tutamla mwanangu.’
[29]Basi
tukampika mwanangu na kumla. Siku iliyofuata
nikamwambia, ‘Mtoe mwanao ili tupate kumla.’
Lakini akawa amemficha.”
D.BWANA ASEMA:NITAWAFANYA KULA NYAMA YA WANA WAO NA BINTI ZAO.
Yeremia 19:9-12
[9]Nitawafanya
wao kula nyama ya wana wao na binti zao, kila
mmoja atakula nyama ya mwenzake wakati wa
dhiki ya kuzungukwa na jeshi lililowekwa juu yao
na adui wanaotafuta uhai wao.’
[10]“Kisha livunje lile gudulia wakati wale walio
pamoja nawe wanaangalia,
[11]uwaambie, ‘Hili
ndilo BWANA Mwenye Nguvu asemalo:
Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili
la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi
kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa
huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi.
[12]Hivi
ndivyo nitakavyopafanya mahali hapa na kwa
wale waishio ndani yake, asema BWANA.
Nitaufanya mji huu kama Tofethi.
E.WANAWAKE WALE WAZAO WAO, WATOTO WALIOWALEA.
Maombolezo 2:20
[20]“Tazama, Ee BWANA, ufikirie:
Ni nani ambaye umepata kumtendea namna
hii?
Je, wanawake wale wazao wao,
watoto waliowalea?
Je, kuhani na nabii auawe mahali patakatifu pa
Bwana?
F.WANAWAKE WENYE HURUMA WALIPIKA WATOTO WAO WENYEWE AMBAO WALIKUWA CHAKULA CHAO.
Maombolezo 4:10
[10]Kwa mikono yao wenyewe wanawake wenye
huruma
walipika watoto wao wenyewe,
ambao walikuwa chakula chao
wakati watu wangu walipoangamizwa.
G.ASEMA BWANA:BABA WATAKULA WATOTO WAO NA WATOTO WATAKULA BABA ZAO.
Ezekieli 5:10-11
[10]Kwa hiyo katikati yenu baba
watakula watoto wao na watoto watakula baba
zao. Nitawapiga kwa adhabu, nami
nitawatawanya watu wenu walionusurika pande
zote za dunia.
[11]Kwa hiyo hakika kama niishivyo,
asema BWANA Mwenyezi, kwa kuwa mmenajisi
mahali pangu patakatifu kwa sanamu zenu
mbaya sana na desturi zenu za machukizo,
mimi mwenyewe nitaondoa fadhili zangu kwenu.
H.ASEMA BWANA: MTAKULA NYAMA ZA WATU MASHUJAA NA KUNYWA DAMU ZA WAKUU WA DUNIA.
Ezekieli 39:17-18
[17]“Mwanadamu, hili ndilo BWANA Mwenyezi
asemalo: ‘Ita kila aina ya ndege na wanyama
wote wa mwituni, waambie: ‘Kusanyikeni mje
pamoja kutoka pande zote kwa ajili ya dhabihu
ninayowaandalia, dhabihu kuu katika milima ya
Israeli. Huko mtakula nyama na kunywa damu.
[18]Mtakula nyama za watu mashujaa na kunywa
damu za wakuu wa dunia kana kwamba ni za
kondoo waume na kondoo wake, mbuzi na
mafahali, wote walionona kutoka Bashani.
2.KAFARA YA BINADAMU.
A.KUTOLEWA KAFARA KWA MAKUHANI NA KUCHOMWA KWA MIFUPA YA BINADAMU KATIKA MADHABAHU.
1 Wafalme 13:1-2
[1]Kwa neno la BWANA mtu wa Mungu
alifika Betheli kutoka Yuda wakati
Yeroboamu alipokuwa amesimama kando ya
madhabahu ili kutoa sadaka.
[2]Akapiga kelele
dhidi ya madhabahu kwa neno la BWANA : “Ee
madhabahu, madhabahu! Hivi ndivyo asemavyo
BWANA: ‘Mwana aitwaye Yosia atazaliwa katika
nyumba ya Daudi. Juu yako atawatoa dhabihu
makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia miungu
wale ambao wanatoa sadaka hapa sasa, nayo
mifupa ya wanadamu itachomwa juu yako.’ ’’
B.WAWEZA TOA BINADAMU KWA BWANA KAMA SADAKA NA MTU AKITOLEWA ILI AANGAMIZWE HAWEZI KUKOMBOLEWA.
Mambo ya Walawi 27:28-29
[28]“ ‘Lakini cho chote kile mtu alichonacho na
kukitoa kwa BWANA, ikiwa ni binadamu au
mnyama au ardhi ya jamaa, chaweza kuuzwa
au kukombolewa, cho chote kilichotolewa ni
kitakatifu sana kwa BWANA..
[29]“ ‘Mtu ye yote aliyetolewa ili kuangamizwa,
hawezi kukombolewa. Mtu kama huyo lazima
auawe.
C.TOA MWANAO KAMA SADAKA YA KUTEKETEZWA.
Waamuzi 11:31-40
[31]cho chote kile kitakachotoka katika
mlango wa nyumba yangu cha kwanza ili
kunilaki nirudipo kwa amani katika kuwashinda
Waamoni, kitakuwa ni cha BWANA na nitakitoa
kuwa sadaka ya kuteketezwa.”
[32]Ndipo Yefta akavuka kupigana na hao
Waamoni, naye BWANA akawatia mkononi
mwake.
[33]Akawapiga kwa ushindi mkubwa
kuanzia Aroeri mpaka karibu na Minithi na
kuendelea mpaka Abel-Keramimu, miji yote
iliyopigwa ni ishirini. Basi Israeli wakawashinda
Waamoni.
[34]Yefta aliporudi nyumbani Mizpa, tazama,
binti yake akatoka ili kumlaki kwa matari na
kucheza. Alikuwa ndiye mtoto pekee, hakuwa na
mwana wala binti mwingine,
[35]Alipomwona
akararua mavazi yake akalia, “Ee binti yangu!
Umenifanya niwe na huzuni na kunyong’onyea
sana, kwa kuwa nimeweka nadhiri kwa BWANA,
ambayo siwezi kuivunja.”
[36]Akajibu, “Baba yangu, umetoa neno lako
kwa BWANA. Nitendee mimi kama vile
ulivyoahidi, kwa kuwa BWANA amekupatia
ushindi dhidi ya adui zako Waamoni.
[37]Naye
akamwambia baba yake, “Naomba nifanyiwe
jambo hili, mimi na nipewe miezi miwili ili
kuzunguka vilimani nikaulilie ubikira wangu,
mimi na wenzangu.”
[38]Baba yake akamwambia, “Waweza
kwenda.” Naye akamwacha aende kwa miezi
miwili. Hivyo akaondoka pamoja na wasichana
wenzake, naye akaulilia ubikira wake huko
vilimani kwa sababu asingeolewa kamwe.
[39]Baada ya hiyo miezi miwili, alirejea kwa baba
yake, naye baba yake akamtendea kama
alivyokuwa ametoa nadhiri yake. Naye alikuwa
bikira.
Nayo ikawa desturi katika Israeli,
[40]kwamba
kila mwaka binti za Israeli huenda kwa siku nne
ili kumkumbuka huyo binti wa Yefta Mgileadi.