Waziri mkuu mpya wa Uingereza Theresa May, amemteua Boris Johnson, aliyeongoza kampeni ya taifa hilo kujitoa katika Muungano wa Ulaya kuwa waziri wa mambo ya nje.
Johnson, ambaye aliwahi kuwa Meya wa jiji la London amesema Uingereza sasa ina nafasi kubwa kujenga upya uhusiano wake na Ulaya na ulimwengu mzima lakini ni ulimwengu ambao ameuuudhi kwa namna moja au nyengine kutokana na matamshi yake ya kejeli.
Haya ni baadhi ya maneno ya kejeli aliyoyatamka kuhusu:
Afrika
Mwaka 2002 wakati Waziri Mkuu wa zamani Tony Blair alipofunga safari ya kuzura bara Afrika Boris alisema; 'Ah ni lazima Blair anahisi afueni kuu kwamba hatimae amepata fursa ya kutoka Uingereza. Inasemekana Malkia siku hizi anapendelea sana maswala ya Jumuiya ya Madola, moja wapo ya sababu ni kuwa inampa fursa za mara kwa mara kuona tu umati wa watu wazima kwa watoto wanaomshangilia wakimpeperushia vibendera.!'
Kisha Boris akaongeza kusema '' Na baadayee ataelekea Congo. Sina shaka hizo AK47 itabidi zinyamaze, mapanga yanayotumiwa na waafrika kukatanakatana yatasitishwa kwa muda na wapiganaji wao wakikabila watatoa tabasamu za kama tikitimaji pindi wakimuona chifu mkuu Wakizungu Blair akitua na akiteremka kutoka ndege yake kubwa iliyonunuliwa na watoa kodi wa Uingereza.''
Japo Bw Johnson aliomba radhi kwa matamshi hayo mwaka 2008, alipopata cheo cha meya wa mji wa London, kauli hiyo haijasahaulika.
Kumhusu Obama
Na si hayo tu Machi mwaka huu wakati maafisa wa Marekani wanaohusika na maswala ya offisi ya Rais Barack Obama alipoamua kuiondoa picha ya Winston Churchill kutoka ofisi yake ya Oval , Boris alisema- ''Hakuna uhakika iwapo Obama mwenyewe alihusika katika uamuzi huo wa kuiondoa picha ya Churchill. Baadhi ya watu wanasema ni kwasababu kwa vile yeye ni nusu mkenya alichukizwa na kumbukumbu ya picha ya Winston ambaye aliunga mkono kwa dhati utawala wa Uingereza ulioikalia Kenya kwa mabavu enzi za ukoloni."
Kuhusu Uturuki
Kama Obama alihisi kuchokozwa Basi rais wa Uturuki ndio zaidi.
Utakumbuka mapema mwaka huu wakati Ujerumani ilipomshtaki raia wake mmmoja mchekeshaji aliyetunga shairi lililomdhalilisha rais Recep Tayyip Erdogan, gazeti moja la Uingereza litwalo The Spectator likaongezea maudhi hayo kwa kuandaa shindano la nani anaweza kutunga shairi la kumdhalilisha Erdogan zaidi ya hilo lililotungwa na mjerumani- Si tu kwamba Boris alishiriki shindano hilo bali pia aliibuka mshindi!
Kumuita Assad dikteta
Kuhusu uhusiano wa serikali ya Syria na Urusi - Baada ya majeshi yao kukomboa mji wa hifadhi za kumbukumbu za kale Palmyra
Boris alinukuliwa kusema 'mtu yoyote mwenye akili timamu anapaswa kufurahi kwamba Palmyra imekombolewa na majeshi ya Assad lakini wakati huohuo asibadili msimamo kwamba Assad ni Dikteta na Zimwi'
Kumshutumu Putin
Kisha akamshtumu Putin akisema operesheni zake za kijeshi zimekuwa zikilenga hospitali na shule za Syria lakini wakati huohuo akamsifu Putin na utawala wake huko Urusi.
Hapo May alihoji sera ya EU huko Ukraine ambako Urusi inashutumiwa kuwaunga mkono waasi wa mashariki wa Ukrain lakini Boris akasisitiza kuwa ni mfano wa
maamuzi ya EU yaliyofeli kutatua mzozo huo unaendelea hadi leo.
Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov amesema anatumai uteuzi wa Boris kama waziri wa mambo ya nje unatoa fursa ya mwanzo mpya baina ya mataifa hayo akiongeza kusema kuwa anatumai nafasi hiyo itamfanya Boris kuwa na msimamo mpya wenye mwelekeo wa kidiplomasia.
Tukitazama tena Marekani, Je Boris anasemaje kuhusu wagombea urais wa nchi hiyo ambao itabidi kukabiliana nao baada ya Novemba ambapo mmoja wao anatarajiwa kumrithi Obama?
Clinton na ‘nywele zilizopakwa rangi’
Mwaka 2007 hivi ndivyo Boris alivomwelezea Bi Hillary Clinton- 'ana nywele zilizopakwa rangi, midomo yake ilivyo na anavyokodoa yale macho yake ya blue, utafikiri ni nesi mwenye roho mbaya ndani ya hospitali ya watu wenye matatizo ya kiakili'
Boris anampenda Trump?
Kwa hivyo ni kusema kuwa Boris anampendelea Donald Trump?
La, hebu msikie alivyosema hapo mwezi Machi '' Kwa kweli nna wasiwasi mkubwa kwamba Trump anaweza kushinda! Na siku moja nilikuwa New York, wapiga picha walikuwa wanataka kunipiga picha karibu na mtoto mmoja - mtoto yule akanisogelea kisha akauliza 'Gee, kwani huyu ni Trump?'
Nilijisikia vibaya sana!' Itakumbukwa Boris amekuwa akimtaja Trump kuwa 'mtu asiyejua akisemacho kama vile hana akili nzuri'.
Na kejeli hizo anajulikana kuziendeleza tangu akiwa Meya wa London.
Boris Johnson amewahi kuwaudhi pia baadhi ya mataifa ya Uarabuni na hata Papua New Guinea ambao hawajaupokelea vyema uteuzi wake.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo November 24, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 24,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetin...
48 minutes ago