Ripoti kutoka mji mkuu wa Sudan
Kusini Juba ,zinasema kuwa mili mingi imepelekwa katika hospitali kuu ya
mji huo baada ya ufyatulianaji mkali wa risasi kuibuka karibu na nyumba
ya rais siku ya Ijumaa.
Idadi ya watu waliouawa hatahivyo haijulikani.Ufyatulianaji huo ulianza wakati ambapo rais Salva Kiir na makamu wake Riek Machar walikuwa wakijadiliana kuhusu ghasia siku ya Alhamisi baada ya wanajeshi watano wa serikali kuuawa katika vita vya pande pinzani.
Viongozi wote wawili wametaka kuwepo kwa utulivu.
Ghasia hizo ni mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu makamu wa rais Riek Machar kurudi mjini Juba mnamo mwezi Aprili na vilevile zinajri wakati ambapo taifa hilo changa zaidi duniani liko katika harakati za kuadhimisha mwaka wa tano tangu lijipatie uhuru wake.