Recent Posts

PropellerAds

Tuesday, July 12, 2016

Moise Katumbi: Serikali ya DRC ilijaribu kuniua

Kiongozi wa upinzani nchini DRC ambaye pia ni
mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi ujao
amesema kuwa serikali ya rais Joseph kabila ilimpa
sumu katika njama ya kumuua.
Mwanasiasa Moise Katumbi wa Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo anasema kuwa alidungwa
sindano iliyokuwa na sumu nje ya mahakama ya
Lubumbashi mnamo mwezi Mei.
Katumbi anasema haikujulikana sindano hiyo ilikuwa na
nini.
Hata hivyo anasema askari polisi mmoja alimdunga
sindano katika mshikemshike nje ya mahakama polisi
walipofyatua mabomu ya kutoa machozi kwa mashabiki
wake alipokuwa akienda kujibu mashtaka ya kuwaajiri
mamluki kuwa walinzi wake kinyume cha sheria.
Bw Katumbi anasema kuwa madai hayo dhidi yake ni
ya ''upuuzi''.
Hata hivyo kiongozi huyo ambaye ni mkurugenzi mkuu
wa klabu ya TP Mazembe aligonjeka na akalazimika
kukimbilia nje ya nchi ilikupata matibabu.
Katumbi ameiambia shirika la habari la AFP kuwa
alikwenda Afrika Kusini Uingereza na kisha Ujerumani
kutafuta tiba.
Waziri wa mawasiliano bwana Lambert Mende hakujibu
mawasiliano dhidi ya serikali yake lakini kwa siku nyingi
amepuuzilia mbali tuhuma kuwa polisi wa DRC
walimdhuru bwana Katumbi.