Recent Posts

PropellerAds

Thursday, July 21, 2016

Utafiti: Harufu ya kuku inazuia Malaria

Je unaogopa kuambukizwa na ugonjwa wa malaria ?
Ikiwa jibu lako ni ndio basi nakupa ushauri nasaha,,
Fuga kuku !
Utafiti umebaini kuwa ,harufu ya kuku inaweza
kukulinda dhidi ya maambukizi ya malaria.
Watafiti nchini Ethiopia na Sweden wamegundua kuwa
mbu wanaobeba vimelea visababishavyo ugonjwa wa
Malaria huwa wanafanya kila wawezalo kukaa mbali na
ndege huyo anayefugwa majumbani.
Moja kati ya majaribio katika utafiti huo ilijumuisha
kumweka kuku aliyehai karibu na mtu aliyelala chini ya
chandarua kinachozuia kuumwa na mbu.
Mwaka uliopita watu laki nne 400,000 walikufa kutokana
na ugonjwa wa malaria barani Afrika, kwa mujibu wa
takwimu za Umoja wa Mataifa.
Japo idadi na visa vya maambukizi ya Malaria
vinaendelea kushuka, wataalamu wanaendelea kutafuta
mbinu bora zaidi ya kuangamiza kabisa ugonjwa huo.
Vimelea vya malaria hujificha ndani ya maini kabla ya
kuambukizwa kutoka kwa mwanadamu mmoja hadi
mwengine kupitia kwa mbu wa kike anayefyonza damu.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Malaria
umebaini kuwa mbu hunusa harfu ya mnyama kabla ya
kumuuma.
Hata hivyo hawajui nini katika harufu ya kuku inawapa
kinyaa mbu .
Katika hatua ya pili ya utafiti huo sasa, watafiti hao
wanalenga viungo vya harufu ya kuku ilikuunda kinga
dhabiti dhidi ya mbu hao wanaoambukiza malaria.
Habtie Tekie kutoka chuo kikuu cha Addis Ababa
Ethiopia anasema kuwa mipango inaendelea na huenda
majaribio yakatekelezwa karibuni.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha kilimo cha Sweden
walihusika katika utafiti huu.
Iligundulika kuwa idadi ya mbu ilipungua kwa asilimia
kubwa sana mahala popote ambapo viungo vya kuku
vilitumika ima ni manyoya ama sehemu zingine za kuku.
Wanasayansi wanasema kuwa kuna haja ya kuendelea
kutafuta mbinu mpya za kukabiliana na mbu kwani hata
sasa mbu wanaonesha dalili ya kuwa sugu dhidi ya
madawa yaliyoko sasa.