Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Malala Yousafzai
amezuru kambi ya wakimbizi ya Dadaab kaskazini
mashariki mwa Kenya ambapo atasherehekea siku
yake ya kuzaliwa.
Malala alizaliwa 12 Julai 1997 eneo la Mingora,
Pakistan katika bonde la Swat.
Alihudhuria shule iliyoanzishwa na babake Ziauddin
Yousafzai na baada ya wanamgambo wa Taliban
kuanza kushambulia shule za wasichana Swat, alitoa
hotuba Peshawar, Pakistan akishutumu Taliban kwa
kumnyima wasichana haki ya msingi.
Akiwa na umri wa miaka 14, yeye na familia wake
walifahamu kwamba Taliban walikuwa wametoa vitisho
kwamba wangemuua.
Tarehe 9 Oktoba, 2012, akirejea nyumbani kutoka
shuleni, akiwa kwenye basi, mtu mwenye silaha
alimpiga risasi kichwani.
Malala ashinda tuzo ya amani ya Nobel
Alipelekwa Birmingham, Uingereza ambapo alipokea
matibabu na Machi 2013 akaanza kwenda shuleni.
Mwaka huo pia, aliandika kitabu kuhusu maisha yake.
Aliteuliwa kushindania tuzo ya amani ya Nobel 2013
lakini hakushinda. Aliteuliwa tena 2014 na akashinda
kwa pamoja na mwanaharakati mwingine Kailash
Satyarthi.
Alikuwa na umri wa miaka 17 na ndiye mtu wa umri
mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo hiyo.
Amekuwa akitetea haki za watoto na wanawake.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo November 24, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 24,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetin...
59 minutes ago