Recent Posts

PropellerAds

Thursday, July 14, 2016

Ndege ya kisasa ya Ethiopia yatua Kenya

Ethiopia imekuwa taifa la kwanza barani Afrika
kununua ndege ya kisasa aina ya Airbus A350 XWB.
Ndege hiyo, Airbus A350, ndiyo ya hivi karibuni
kuzinduliwa na kampuni ya ndege ya Airbus ya
Ufaransa.
Ndege hiyo, iliyo na uwezo wa kubeba zaidi ya abiria
300, ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano jioni
ikitokea mjini Addis Ababa, Ethiopia.
"Ndege hii ya kisasa itasaidia katika utoaji wa huduma
zetu, kuimarisha mtandao wetu wa usafiri, na
kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya hewa chafu
inayotolewa wakati wa usafiri wa ndege,” Mkurugenzi
mkuu wa shirika la Ethiopian Airlines Tewolde
GebreMariam amesema.
Ndege hiyo ni ya kwanza kuwasilishwa kwa kampuni
hiyo, huku nyingine 13 ilizoagiza kutoka kwa kampuni
ya Airbus zikisubiriwa hivi karibuni.
Safari ya kwanza ya ndege hiyo ilifanyika tarehe 2 Julai
iliposafiri kutoka Ufaransa hadi mjini Lagos, Nigeria.
Viwango vya juu vya teknolojia iliyotumika kuunda
ndege hiyo, vinachangia katika kuinua utendakazi wake,
kupunguza matumizi ya mafuta pamoja na kupunguza
kwa kiasi kikubwa utoaji wa hewa chafu.
Ndege isiyotumia mafuta yatua Misri
Ndege kubwa zaidi duniani yatua Australia
Kampuni ya Ethiopian Airlines inaorodheshwa ya
kwanza barani Afrika kwa faida na pia idadi ya maeneo
inayosafirisha abiria.
Mwaka wa 2012, shirika hilo pia lilikuwa la pili duniani
na la kwanza barani afrika kununua ndege aina ya
Boeing 787 Dreamliner, ya kampuni ya Boeing, yenye
afisi zake kuu Chicago, Marekani.
Kampuni ya Airbus na Boeing zinaongoza duniani katika
utengenezaji wa ndege za kisasa, japo Airbus ina
umaarufu mkubwa na imeipiku Boeing kwa faida na
uuzaji wa idadi kubwa ya ndege.