Maelezo ya kibinafsi ya takriban wanachama 150,000 wa mtandao unaowaunganisha wapenzi wa Kiislamu umewekwa wazi mtandaoni.
Zaidi ya ujumbe 700,000 za kibinafsi kati ya wanachama zimefichuliwa.Ujumbe katika mtandao huo ulisema: ''Tumejulishwa kuhusu udukuzi na tunaurekebisha mtandao wetu kwa lengo la kuimarisha usalama wake''.
Ujumbe uliofichuliwa ulihusisha habari za siri kama vile iwapo mwanachama angependa kuwa na wake wengi.
Udukuzi huo ulibainiwa na mtafiti wa maswala ya kiusalama Troy Hunt ambaye anamiliki mtandao wa maswala ya usalama wa mitandaoni.
Maelezo kuhusu waajiri wa wanachama,akaunti zao za Skype na anwani zao za kuingia mtandao kulingana na mtandao wa teknolojia Motherboar.
Ukurusa wa kuwaunganisha waislamu wapendanao katika facebook ulielezea mtandao huo kuwa :Wasio katika ndoa,waliotalakiana,walio katika ndoa,''Ujumbe mmoja uliofichuliwa ulisema: Nataka kukuoa-iwapo unakubali nikutumie picha na maelezo yangu''.