Shirika la Kimataifa la kutetea haki
za binadamu la Amnesty International limesema maelfu ya raia wa Sudan
Kusini wanasumbuliwa na kiwewe baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, na
walio wengi hawana matarajio ya kupata tiba.Shirika hilo limesema watu
walilazimishwa kula nyama ya binaadamu wenzao na wengine walilazimishwa
kuipasua miili ya binaadamu wenzao wakati huo wa kivita, vilivyoanza
mwishoni mwa mwaka 2013.
Amnesty inasema kwamba katika hali ya
kusikitisha Sudan Kusini ina hali mbaya ya ukosefu wa huduma za afya ya
akili, ikiwa na madaktari wawili tu magonjwa ya akili wakihudumia idadi
ya watu zaidi ya milioni kumi.Wagonjwa wa magonjwa ya akili mara nyingi wamekuwa wakizuia magerezani.