Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, July 6, 2016

Mamba anayebashiri matokeo ya uchaguzi Australia


Gazeti moja nchini Australia limedai kwamba kuna mamaba anayeweza kubashiri matokeo ya uchaguzi nchini Australia.
Gazeti hilo la Northern Territory News ni maarufu kwa habari zake katika ukurasa wake wa kwanza.
Huku raia wakisubiri uchaguzi wa siku ya Jumamosi ,gazeti hilo liliweka picha za wagombea wawili wakuu wa uchaguzi huo katika ndoana ya samaki na kumrushia mamba anayeitwa Burt mwenye urefu wa mita 5.1.
Burt alionekana kuifuata picha ya kiongozi wa upinzani Bill Shorten ,lakini baada ya mda akaamua kuitia mdomoni ndoana ya picha ya waziri mkuu Malcolm Turnbull,ikiwa ishara inayoonyesha kwamba ataibuka mshindi katika uchaguzi huo.
''Wanaobashiri tayari wamesema kuwa waziri huyo ataibuka mshindi'', alisema muhariri wa gazeti hilo Matt Williams.
Ubongo wa mamba huyo ni mdogo sana lakini ni miongoni mwa wanyama werevu sana.
Mamba huyo huishi katika mbuga ya wanyama pori ya Crocosaurus Cove na alishiriki katika katika filamu ya Australia Crocodile.
Ni mnyama wa hivi karibuni aliyebainika kuwa mwerevu huku yule maarufu akiwa Pweza Paul,ambaye alifanikiwa kubashiri matokeo ya mechi saba katika kombe la dunia la mwaka 2010 nchini Ujerumani.

Related Posts:

  • Serikali ya Kenya yasema shisha ina Cocaine Wizara ya afya ya Kenya imekuwa ikitoa tahadhari dhidi ya matumizi ya uvutaji wa shisha ,katika siku hii ya kuadhimisha siku ya tumbaku duniani. Siku hii ilitengwa na Shirika la Afya duniani kuwaonya watu kuhusu hatari za… Read More
  • UM kupeleka misaada zaidi nchini Syria Maafisa wa kibalozi jijini New York wanasema kuwa hiyo kesho Umoja wa Mataifa utaomba rasmi Serikali ya Syria kuruhusu kudondosha vyakula na madawa katika maeneo wanakoishi wananchi walio katika hatari ya kufa kutokana n… Read More
  • Waliokuwa maafisa wa Fifa walijipatia $80m Mawakili wa FIFA wasema washukiwa wakuu wa madai ya ufisadi ambao hadi hivi majuzi walikuwa wakiliongoza shirikisho hilo la kandanda duniani walijilimbikizia nyongeza za mishahara na marupurupu mengineyo ambayo yamejumui… Read More
  • Bondia Muhammad Ali alazwa hospitalini Bingwa wa dunia wa uzani wa juu wa zamani Muhammad Ali amelazwa hospitalini kufuatia maambikizi ya mapafu. Bondia huyo nyota mwenye umri wa miaka 74 aliyekonga nyoyo za wapenzi wa ndondi kote duniani anasemekana kuwa kati… Read More
  • Thoughts for the Next Generation of Leaders  Last week Athletes in Action launched a NextGen Leadership initiative. Nearly two years in the planning, we had 19 staff members and 19 coaches from the business world taking part. It was a spectacular launch to th… Read More