Kicheche ni mnyama anayepatikana katika sehemu ya jangwa la sahara Barani Afrika,ukanda wa savana na mnyama huyu ni adimu sana kupatikana katika misitu mikubwa kama ya Congo na maeneo ya pwani.
Mnyama huyu anafanana sana na NGUCHIRO ana urefu wa sentimeta 60 urefu huo una jumlisha mwili na mkia wake, na mkia pekee una urefu wa sentimeta 20.chakula kikubwa cha kicheche ni ndege,nyoka,mijusi,chura,wadudu na wanyama wengine wadogo kama panya nk.
Wakati wa kukabilina na maadui,mnyama huyo hutoa harufu kali kwa kujamba na kuwafanya maadui kugaili kumkamata na wazungu humuita “Father of stinks kutokana na harufu kali anayo toa wakati akijihami na maadui.
Pia kicheche ana tabia ya kuinua mkia wake kwa kubinua mgongo ili aonekane mkubwa baada ya kumuona adui yake kwa lengo la kumtisha na mara nyingi hupenda kula kila wakati na ana uwezo wa kuishi miaka 13.
Ni namna gani hufanikisha mawindo yake?kumekuwa na dhana nyingi sana wengine wakizani hutumia sehemu ya haja kubwa kukamata ndege au kuku,lakini utafiti unaonyesha kuwa hutumia miguu yake ya nyuma iliyoimara (badala ya miguu ya mbele) kumkatama mnyama mdogo au ndege na kisha kumbana kwa ufundi mkubwa.