Kiwanda kimoja cha pombe nchini
Denmark kimetengeneza bia mpya kwa kutumia shayiri ambayo imekuzwa kwa
kutumia lita 50,000 za mkojo.
Kampuni ya Norrebro Bryghus
inayomiliki kiwanda hicho hata hivyo imesema bia hiyo haitakuwa na
masalio yoyote ya mkojo wa binadamu.Pombe hiyo imepewa jina Pisner na imeandaliwa kwa kutumia kimea cha pombe kutoka wka shayiri iliyokuzwa kwa kutumia mkojo huo badala ya mbolea ya kawaida.
Mkojo huo ulikusanywa kutoka tamasha ya Roskilde ambayo ndiyo hafla kubwa zaidi ya muziki Ulaya kaskazini miaka miwili iliyopita
"Wakati habari kuwa tulikuwa tumeanza kutengeneza pombe zilifichuka, watu walidhani kuwa tulikuwa tukiweka mkojo huo moja kwa moja kuenda kwa pombe," alisema mkurugenzi wa kampuni ya Norrebro Bryghus.
"Kama ingekuwa na ladha ya mkojo ningeachana nayo, lakini hata huwezi ukahisi," alisema mtu moja ambaye alihudhuria tamasha hiyo ya muziki mwaka 2015.,
Lita hizo 50,000 za mkojo zilizokusanywa kutoka kwa warsha hiyo ya muziki zilitosha kuunda chupa 60,000 za bia.
Kutumia kinyesi au mkojo wa binadamu kwa kiwango kikubwa hivyo ni jambo ambalo si la kawaida, baraza la kilimo na chakula nchini Denmark linasema.
Baraza hilo ndilo lililotoa wazo hilo la kutumiwa kwa mkojo kama mbolea ya kurutubisha shayiri ambayo baadaye inatumiwa kutengeneza pombe.
Lakini usishangae, tayari kuna mtambo wenye uwezo wa kubadilisha mkojo moja kwa moja na kuwa bia.
Mashine iliyotengenezwa na kundi la wanasayansi katika chuo kimoja nchini Ubelgiji, inabadili mkojo wa binadamu na kuwa maji ya kunywa pamoja na mbolea ikitumia nguvu za miali ya jua.
Maji hayo, kutoka kwa mkojo uliokusanywa kwa siku kumi katika tamasha moja la muziki Ghent kisha yalitumiwa kutengeneza bia.