Wanawake wengi wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi tayari(menopause) hukosa hamu ya tendo la ndoa.
Wataalamu wa afya wameshauri vyakula vinavyoweza kuwapa wanawake hamu ya tendo la ndoa.
Mtaalamu wa Saikolojia wa Uingereza, Cassie Bjork, anasema badala ya
kutumia dawa (Viagra) vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kuna vyakula
maalum.
Spinachi
Wataalamu hao wanasema mboga ya majani aina ya spinachi ina wingi wa
madini ya magnesium ambayo husaidia kusambaza damu kwenye mirija. Damu
inaposambaa vyema mwilini hata hamu ya tendo la ndoa huongezeka.
Bjork anasema kula kwa wingi mboga hizo kunamsaidia mwanamke hata kufikia kilele.
Chai ya Kijani (Green tea)
Chai ya kijani ina kompaundi iitwayo catechins. Hii inaelezwa kuwa
inasaidia kuyeyusha mafuta mwilini. Lakini pia inalisaidia ini kuchuja
sumu na kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri. Damu ikitembea
vyema mwilini, ni rahisi kwa mwanamke kujisikia hamu ya tendo.
Mafuta ya samaki
Zipo aina nyingi za mafuta ya samaki. Lakini mafuta ya samaki wenye
asidi ya Omega-3 yana virutubisho ambavyo huongeza kiwango cha
‘dopamine’ kwenye ubongo.
Dopamine ni eneo la ubongo linalofanya kazi ya kudhibiti faraja na
hisia. Kama dopamine itaongezeka basi mwanamke hujisikia kuridhika
anapokuwa na mwenza wake.
Chokoleti
Pamoja na utamu wake, lakini ‘chocolate’ ina virutubisho na madini ya
magnesium ambayo humfanya mwanamke kuridhika. Pia huufanya ubongo wa
mwanamke kutulia kwa kuondoa msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo ukiisha
ni rahisi kwa mwanamke kupata hamu ya tendo la ndoa.
Ushirikiano wa Paul Pogba-Juventus unatarajiwa kumalizika leo
-
Kulingana na ripoti za Sky Sports News inasemekana kuwa Juventus na Paul
Pobga (31) wanakaribia kuvunja makubaliano yao baadaye leo. Pogba aliona
marufuk...
4 hours ago