Recent Posts

PropellerAds

Tuesday, May 16, 2017

Mambo yanauowaumiza wanaume katika mahusiano.

Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Kilio chao kikubwa ni kukimbiwa na wanaume au kuachwa.
Leo anakuwa na mwanaume huyu, baada ya muda mfupi kunatokea chokochoko, mwanaume anatimka zake.
Jamaa anamkimbia na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine. Baada ya kukimbiwa, mwanamke hakati tamaa. Anaanzisha uhusiano mwingine, ndani ya muda mfupi tu, anaambulia maumivu tena. Anabaki kujilaumu. Hajui chanzo cha yeye
kukimbiwa.
Matokeo ya hili, mwanamke anapoteza uelekeo. Kila mwanaume anayekutana naye anamkimbia. Mwisho wa siku anajikuta umri umeenda. Kuolewa inakuwa ni ndoto. Anaanza kulazimisha kusaka mtoto ili angalau na yeye aitwe mama.
Wanaume wengi hujikuta wakiwaacha wapenzi wao kwa sababu ya tabia fulani ambazo wakati mwingine huanza taratibu na baadaye huwa kikwazo kikubwa.
Ili kuweza kuepukana na tatizo hili ni vyema tukaangalia vitu ambavyo wanaume wamekuwa hawavipendi kutoka kwa wanawake ili kuweza kujua nini cha kufanya kuhakikisha unamweka mwanaume karibu, asikuache.
1. Chokochoko/Maneno Maneno
Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.
Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.
Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.
2. Kutoridhika
Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.
Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao. Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.
Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.
Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake hamtimizii.
Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.
3. Kulinganisha
Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’
Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.
Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata yule anayemvutia.
Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.
4. Kuwa Tegemezi
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.
Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.
Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.
Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.
5. Kutokuwa Muelewa
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.
Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.
6. Kujigamba/Maringo
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.
Isikupite hii: Mambo matano '5' yatakayo kuongezea thamani katika maisha yako
Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.
7. Kuwa bize sana
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.
Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize.

Related Posts:

  • 3 Ways to Love Your Wife I’m a super busy husband and father of three. Sometimes I feel piled under with all the things on my plate. Praise God he’s given my bride as a helpmate; my wife is a superstar! She helps in so many ways, yet, too often… Read More
  • Always Do Your Best.“Popularity is people liking you; happiness is you liking you.” In a world in which we are all trying to discover our full potential and create “happy” lives, I find this to be an interesting quote. In a world that is ofte… Read More
  • The Hardest Sermon You'll Ever Preach (or hear)    By Rich Ryan Nothing can fully prepare you for it. As I reflect over the most challenging sermons I have preached, no difficult text or exegetical conundrum has ever been as difficult as preaching a memori… Read More
  • 3 Ways to See God in Your Suffering Horatio Spafford didn’t know it, but he was about to face incredible suffering. He planned a family vacation to Europe for the fall of 1873, but a business emergency kept him from traveling with his family. Intending to… Read More
  • Health Benefits Of Grape Leaves Grape leaves are very well known as a natural remedy with quite a good number of health benefits. Grape leaves are used in many nations of South Europe and the Middle East for cooking: in particular, grape leaves staffe… Read More