SAMAKI anayefahamika kwa jina la kimombo la Electric eel ni moja ya
samaki wenye nguvu za umeme wanaopatikana katika maeneo mbalimbali hapa
duniani.
Samaki huyo anapatikana katika mto Amazoni katika bara la Amerika kusini anatajwa kuwaana uwezo wa kuzalisha nguvu kubwa ya umeme mwilini mwake kwenye ogani maalum za mwili wake.
Nguvu hizo za umeme za samaki huyo aina ya Electric eel zinatajwa
kuwa kwenye misuli na seli za mwili wake na mara nyingi nguvu hiyo ya
umeme huitumia kwajili ya kujihami na maadui na hutumia wakati akitafuta
chakula ambapo hutumia nguvu hiyo ya umeme kwajili ya kuwaua viumbe
wakiwemo samaki wa kawaida kwajili ya kitoweo.
Maajabu ni kuwa samaki aina ya Electric eel anayepatikana katika
mto amazoni kusini mwa bara la Amerika mwenye nguvu ya umeme inayofikia
volt 500 na samaki aina ya Electric catfish anayepatikana katika mto
Nile nchini Misri katika bara la Afrika mwenye nguvu ya umeme
inayofikia volt 350 ndiyo samaki wanaotajwa kuwa na uwezo wa kumuua
hata binadamu au mnyama kama Pundamilia.
Takwimu za watalaam mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa kuna samaki
zaidi ya mia mbili (200) wenye nguvu ya umeme na aina hii ya samaki
wenye nguvu ya umeme wanapatikana katika bahari na mito.
Katika bara la Afrika Samaki hawa wanapatikana zaidi katika maeneo ya
tabia ya kitropiki na baadhi ya maeneo ambayo unaweza kuwaona samaki
hao ni katika Ziwa Tanganyika,Mto Nile nchi ya Misiri na katika mto
Ogooue nchini Gabon na baadhi ya mito katika nchi za Afrika ya kati.
Pia samaki hao wenye nguvu ya umeme wanapatikana kwa wingi zaidi
katika bara la Amerika kusini katika mito ya Amazon na Orinoco na ni
samaki wanaotajwa kuwa wamekuwa wakiuwa viumbe wengi sana majini.
Na katika bahari samaki hao wanapatikana katika bahari ikiwemo ya
Pasific na katika bahari za Mediterranean na Caribbean ingawa samani
wengi wa baharini hawana nguvu kubwa ya umeme kama samaki wa kwenye
mito.
Jambo la kukumbuka ni kuwa samaki hawa wenye nguvu ya umeme kwamjibu wa taarifa za kitalaam ni kuwa hawafai kwajili ya kitoweo.
Samaki hao wenye nguvu ya umeme wanatajwa kuwa ni miongoni mwa
samaki (10) hatari sana duniani,wakiwemo Lion Fish,. Piranha. Bull
Shark. 4 Great White Shark, Stone Fish. Puffer Fish, Box Jelly Fish na
Electric Eel.