Maafisa wa usalama nchini Mexico wamemkamata
mwanamume wanayesema alisaidia kulangua pesa kwa
niaba ya mlanguzi wa mihadarati Joaquin Guzman,
aliyejulikana sana kama "El Chapo" au "Shorty".
Juan Manuel Alvarez Inzunza, kwa jina la utani "King
Midas", alikamatwa akiwa likizoni katika jimbo la
Oaxaca, kusini mwa nchi hiyo.
Guzman, kiongozi wa zamani wa genge la Sinaloa, kwa
sasa anasubiri kuhamishiwa Marekani akajibu mashtaka.
Alikamatwa Januari baada yake kutoroka jela mwaka
jana.
Bw Inzunza anashukiwa kulangua takriban $300m-
$400m kwa niaba ya genge la Sinaloa kupitia mtandao
wa kampuni na vituo vya kubadilisha pesa za kigeni.
Mahakama ya dola mjini Washington iliomba Inzunza
akamatwe na huenda akapelekwa Marekani kujibu
mashtaka.
Guzman mwenyewe anatakiwa Marekani akajibu mashtaka
ya ulanguzi wa mihadarati California, na mauaji Texas.
Monday, March 28, 2016
Aliyesaidia El Chapo kulangua pesa anaswa
'Al-Shabab 100 wauawa' vitani Somalia
Kiongozi wa jimbo la Galmudug, katikati mwa Somalia
amesema wanajeshi wa jimbo hilo wamewaua zaidi ya
wapiganaji 100 wa al-Shabab kwenye mapigano
yaliyodumu siku nne.
Wapiganaji hao wa Kiislamu walikuwa wameingia jimbo
hilo wakitoroka mapigano mengine kaskazini katika jimbo
la Puntalnd.
Rais wa jimbo hilo Abdikarin Hussen Gulled ameambia
BBC kwamba wapiganaji 100 waliuawa na wengine
wengi kukamatwa.
Habari hizo hazijathibitishwa na taasisi nyingine.
Wapiganaji 30 wa al-Shabab wauawa Puntland
Wapiganaji wa al-Shabab walikuwa wamekabiliana na
wanajeshi wa jimbo la Puntland linalopakana na
Galmudug mapema wiki iliyopita.
Wamekuwa wakihamia maeneo ya kaskazini baada ya
kukabiliwa na wanajeshi wa Somalia wakisaidiwa na
wanajeshi wa nchi za Umoja wa Afrika (Amisom)
maeneo ya kusini na kati mwa Somalia.
Sharif aahidi kuangamiza magaidi Pakistan
Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif ametoa wito
kwa kuwepo ushirikiano zaidi kati ya idara za usalama
nchini humo ili kukabiliana na ugaidi.
Amesema hayo siku moja baada ya watu zaidi ya 70
kuuawa kwenye shambulio la bomu katika mji wa
Lahore. Kiongozi huyo ameahidi kuwaangamiza magaidi
hao.
Bw Sharif, aliyekutana na viongozi wa idara za
usalama, amesema taifa hilo litaimarisha juhudi za
kukabiliana na ugaidi.
Watu kadha wamekamatwa na silaha kupatikana kwenye
operesheni iliyofanywa na vikosi vya usalama, jeshi
limesema.
Kundi la Jamaat-ul-Ahrar lililotokana na kundi la
Taliban limekiri kutekeleza shambulio hilo.
Watu 300 walijeruhiwa na maafisa wa serikali
wamesema idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda.
Eneo hilo lilikuwa na watu wengi kuliko kawaida, kwani
Wakristo walikuwa wamekusanyika katika bustani
kusherehekea Pasaka.
Facebook yaomba radhi kuhusu Pakistan
Taliban wakiri kuhusika shambulio Pakistan
Hata hivyo, wengi wa waliofariki walikuwa Waislamu.
Mmoja wa waliofariki, mvulana Mkristo Sahil Pervez,
alizikwa Jumatatu.
Bw Sharif alitembelea majeruhi hospitalini.
Baadaye katika mkutano na maafisa wa usalama,
alisema ni jambo la umuhimu mkubwa kuwashinda
magaidi.
“Azma yetu kama taifa na serikali inaendelea kuwa
thabiti na adui huyu mwenye uoga anajaribu kushambulia
watu wasio na silaha,” amesema.
Aliapa kuwa serikali yake itawaangamiza magaidi hao
walioua “wanangu”.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis kwa
upande wake ametoa wito kwa serikali ya Pakistan
kulinda makundi ya kidini ya wachache nchini humo.
Fidel Castro akosoa ziara ya Obama Cuba
Aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa Cuba Fidel
Castro amevunja kimya chake kuhusu ziara ya hivi
majuzi ya Rais wa Marekani Barack Obama nchini
humo.
Kwenye barua iliyochapishwa katika gazeti la serikali ya
nchi hiyo la Granma kiongozi huyo ameonekana kukosoa
ziara hiyo.
Fidel, aliyemkabidhi kakake Raul uongozi wa taifa hilo
mwongo mmoja uliopita, amesema Cuba haihitaji zawadi
zozote kutoka kwa Marekani.
Akijibu pendekezo la Bw Obama kwamba wakati umefika
wa kuunda urafiki na kuzika kwenye kaburi la sahau
masalio ya Vita Baridi bara Amerika, Fidel Castro
amewakumbusha wasomaji kuhusu uvamizi wa Bay of
Pigs uliofanywa na wakimbizi wa Cuba wakisaidiwa na
Marekani mwaka 1961.
Kwa Picha: Ziara ya Obama Cuba
Obama amtaka Castro asiiogope Marekani
Obama na Castro wajibizana Cuba
Amesema maneno ya Obama ya kuhimiza maridhiano ni
sawa na “rojo ya sukari” na kuonya kwamba raia wa
Cuba wanaweza kupata “mshtuko wa moyo”.
Fidel Castro, 89, aliongoza Cuba kuanzia 1959 hadi
2008 alipomkabidhi nduguye madaraka.
Sunday, March 27, 2016
Taliban group claims Lahore park attack
A Taliban splinter group says it carried out a suicide
attack on a park in Lahore, Pakistan, which killed
more than 70 people, including children.
Jamaat-ul-Ahrar said it had targeted Christians
celebrating Easter, though police have said they are
still investigating the claim.
There were scenes of carnage as parents searched for
children amid the debris.
Pakistan's president condemned the attack, and the
regional government has announced three days of
mourning.
At least 300 people were injured, with officials saying
they expected the death toll to rise.
All major hospitals in the area were put on an
emergency footing after the blast, early on Sunday
evening.
Mali yakamata 2 waliopanga ugaidi Ivory Coast
Polisi nchini Mali wanasema watu wawili wamekamatwa
kaskazini mwa nchi, kwa kuhusika na shambulio
lilofanywa mwezi huu na Al Qaeda, katika eneo la
watalii nchini Ivory Coast.
Mmoja wao anasemekana kuwa ndiye aliyepanga usafiri
wa washambuliaji.
Mwenzake anatuhumiwa kuwa mshauri mkuu kiongozi wa
njama hiyo.
Wanaume wote wawili ni raia wa Mali.
Watu 19 waliuwawa pale wanaume waliokuwa
wamejihami kwa silaha kali kuingia kwa nguvu katika
eneo la pwani, la Grand Bassam, karibu na mji mkuu,
wa Ivory Coast, Abidjan.
Waliwapiga risasi waliokuwa wakikoga ufukweni, kabla ya
kuivamia hoteli.
Saturday, March 26, 2016
Pope delivers Easter message of hope after grim week of terror
Pope Francis preached an Easter message of hope after
a grim week in Europe, calling on Christians not to let
fear and pessimism "imprison" them.
Speaking amid tight security at the Vatican, the Pope
said: "Let us not allow darkness and fear to distract
us and control our hearts."
His message followed a condemnation on Friday of the
Brussels terror attacks.
Islamist violence is expected to be a prominent theme
of his traditional "Urbi et Orbi" Easter message.
Many pilgrims cancelled their planned trips to Rome in
the wake of the violence in Brussels, but St Peter's
Basilica in the Vatican was packed when Pope Francis
celebrated mass on Saturday evening.
The Pontiff entered a darkened basilica with just a
single candle guiding him. As he reached the altar,
the basilica's floodlights came on to symbolise the
resurrection of Jesus Christ.
Delivering his homily, Francis said: "Today is the
celebration of our hope. It is so necessary today."
The lengthy vigil service also included a papal baptism
for 12 adults hailing from China, South Korea and
other countries around the world.
On Sunday morning, Francis will preside over Easter
Mass and offer his annual Easter blessing.
On Friday, he denounced the "terrorist acts committed
by followers of some religions which profane the name
of God and which use the holy name to justify their
unprecedented violence".
Meanwhile, Vatican officials distributed sleeping bags to
100 homeless people.
The police presence in the streets around the Vatican
has been stepped up this year, as more pilgrims than
usual are expected after Francis declared a jubilee year
for the Catholic Church, calling it a "Holy Year of
Mercy".
Wagombea warushiana matusi Marekani
Wagombeaji wawili wa Urais wa chama cha Republican
nchini Marekani wamegombana vikali na kurushiana
matusi juu ya wake zao.
Seneta wa Texas, Ted Cruz, amemlaumu mpinzani
wake, mfanyabiashara Donald Trump kwa kuzusha uvumi
kuwa yeye alikuwa mzinifu na kumdanganya mkewe,
Heidi.
Bwana Cruz alisema uvumi huo ni takataka na akasema
kuwa anaelewa kuwa uvumi ulianzishwa na Bwana Trump
ambaye alisema hastahili kuwa Rais.
Bwana Trump alisisitza kuwa hakuhusika vyo vyote na
uvumi huo.
Mapema juma hili, Bwana Trump alimlaumu Seneta Cruz
kwa kuweka picha za mkewe, Melania, akiwa uchi
kwenye mtandao ili kumharibia sifa.
Friday, March 25, 2016
Midomo sasa kufichua siri za watu
Wataalamu nchini Uingereza wanasema wamevumbua
teknolojia ya kusoma midomo ya watu ambayo inaweza
kubaini wanasema nini bila kusikia wanachosema.
Teknolojia hiyo inaweza kusaidia sana kufahamu watu
wanaonaswa kwenye kamera za siri za CCTV wanasema
nini.
Wataalamu hao katika chuo kikuu cha East Anglia
wanasema teknolojia hiyo inaweza kutumiwa kukabiliana
na uhalifu na ugaidi.
Lakini pia inaweza kutumiwa na wanahabari wanaofuatilia
habari za wasanii na watu mashuhuri.
Watu ambao wamekuwa wakitumiwa kujaribu kusoma
midomo ya watu wamekuwa wakitatizika sana
kutofautisha sauti kama vile P na B.
Lakini wanasayansi hao wanasema teknolojia hiyo mpya
inaweza kutofautisha sauti hizo.
Wataalamu hao wanasema pia kwamba teknolojia hiyo
mpya itasaidia sana katika mifumo ya kukusanya habari
kwa kutumia kompyuta.
Akamatwa kwa kuipelelezea Korea Kusini
Raia wa Marekani aliyekamatwa nchini Korea Kaskazini
amesema kuwa aliiba siri za kijeshi za Korea kaskazini
ili kuisaidia Korea Kusini katika taarifa na waandishi wa
habari ilioandaliwa na Pyongyang.
Kim Dong Chul mwenye umri wa miaka 62 alikiri
kufanya hivyo siku ya ijumaa,akiomba msamaha kwa
kupeleleza.
Bwana Kim awali aliwaambia waandishi kwamba yeye ni
raia wa Marekani aliyezaliwa nchini Korea Kusini na
kwamba alikamatwa mwezi Oktoba kwa kufanya
upelelezi.
Bwana Kim amesema kwamba alikutakana na maafisa wa
upelelezi kutoka Korea Kusini mwaka 2011 ili kuifanyia
uchunguzi,kulingana na shirika la habari la KCNA
kutoka nchini Korea Kaskazini.
Alikamatwa wakati alipokuwa akichukua habari za
kijasusi za kijeshi na zile za kinyuklia kutoka kwa mtu
ambaye hakutajwa.
Kiongozi wa IS auwawa Syria
Kiongozi wa pili kwa ukubwa katika itifaki ya kundi la
wapiganaji la Islamic State ameuawa katika oparesheni
iliotekelezwa na Marekani nchini Syria mwezi huu,
vyombo vya habari vya Marekani vimesema.
Maafisa wa ulinzi wameliambia shirika la habari la NBC
kwamba Abdul Rahman Mustafa al- Qaduli,raia wa Iraq
anayejulikana kama Hajji Iman aliuwawa katika uvamizi
mwezi huu.
Waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani Ash
Carter alitarajiwa kuthibitisha kifo cha mwana jihad
huyo na kutoa maelezo ya uvamizi huo.
Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya dola milioni saba
kwa mtu yeyote ambaye angetoa habari za Qaduli.
Qaduli alizaliwa mwaka 1957 ama 1959 kaskazini mwa
mji wa Iraq wa Mosul ambao ulidhibitiwa na IS tangu
mwaka 2014.
Alijiunga na al-Qaeda nchini Iraq mwaka 2004 chini ya
uongozi wa marehemu Abu Musab al-Zarqawi akihudumu
kama naibu wake na kiongozi wa eneo la Mosul
kulingana na Marekani.
Baada ya kuachiliwa kutoka kwa jela za Iraq mapema
mwaka 2012,alijiunga na vikosi vya IS nchini Syria.
Korea Kaskazini yafanya zoezi la kushambulia makao ya rais
Korea Kaskazini imesema kuwa imetekeleza mazoezi ya
kuyashambulia makaazi ya rais wa Korea Kusini.
Zoezi hilo lilisimamiwa na rais wa taifa hilo Kim Jong-
un,kulingana na chombo cha habari cha KCNA ambaye
alilitaka jeshi kujiandaaa kuivamia na kuiharibu serikali
ya kusini.
Ni hatua ya hivi karibuni ya ishara za hasira za
Pyongyang.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye ameliagiza jeshi
lake kuwa katika hali ya tahadhari.
Lakini alisema siku ya Alhamisi kwamba uchochezi
utasababisha maafa makubwa kwa serikali na uongozi wa
Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini imekuwa ikijibu hatua ya Umoja wa
Mataifa ya kuiwekea vikwazo kufuatia majaribio ya
makombora yake ya masafa marefu ya kinyuklia.
Pyongyang vile vile imekasirishwa na mazoezi ya pamoja
kati ya serikali ya Korea Kusini na Marekani kusini mwa
mpaka wake.
Kama inavyojulikana kwa vitisho vyake ,ripoti hiyo
iliotolewa na KCNA ilitishia kuilipua nyumba hiyo ya
rais wa Korea Kusini inayojuliakana kama Blue House
hadi kuwa jivu.
Makombora yalirushwa kama umeme na kuanguka katika
maeneo yanayolengwa ikiwemo nyumba hiyo ya rais wa
Korea Kusini.
Haijulikani ni lini zoezi hilo lilifanywa,lakini ripoti hiyo
ilionya mwisho mbaya wa rais Park.
Makaazi hayo ya Blue House yalishambuliwa na
makomando wa Korea Kaskazini mwaka 1968.
Hatahivyo jaribio la kutaka kumuua aliyekuwa rais Park
Chung-hee halikufanikiwa,raia saba wa Korea Kusini
pamoja na makomando hao 31 kutoka Korea Kaskazini
waliuawa.
Baba Mtakatifu aosha miguu ya waislamu
Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameosha
miguu ya wahamiaji waislamu mjini Rome katika tukio la
unyenyekevu linaloambatana na itikadi ya kuanza kwa
msimu wa Pasaka.
Papa Francis alitembela makao ya wahamiaji, mjini
Roma na kuendesha misa ya kuanza kwa msimu wa
pasaka.
Ziara yake katika kituo hicho cha kutathmini uhalali wa
wahamiaji cha (Castelnuovo di Porto), inawadia huku
uhasama na taharuki ikienea kote barani ulaya kuhusiana
na kuwepo kwa wahamiaji waislamu hususan kufuatia
mauaji ya Paris mwezi Novemba na ya hivi punde huko
Brussels Ubelgiji.
Papa Francis alikashifu mauaji yaliyotokea Ufaransa na
Ubelgiji akisema kuwa hizo ni njama za watu wenye kiu
cha kumwaga damu ya binadamu.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani alilaumu
mtazamo wa watuhumiwa hao kuhusu maafa
waliyosababisha.
Aidha papa mtakatifu aliwashauri watu wa dini tofauti
duniani kuishi kwa amani.
''Haijalishi iwapo tunaimani tofauti la muhimu kwetu
sote ni tuishi kwa amani sisi ni ndugu alisema papa
mtakatifu.





