Recent Posts

PropellerAds

Monday, March 28, 2016

Fidel Castro akosoa ziara ya Obama Cuba

Aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa Cuba Fidel
Castro amevunja kimya chake kuhusu ziara ya hivi
majuzi ya Rais wa Marekani Barack Obama nchini
humo.
Kwenye barua iliyochapishwa katika gazeti la serikali ya
nchi hiyo la Granma kiongozi huyo ameonekana kukosoa
ziara hiyo.
Fidel, aliyemkabidhi kakake Raul uongozi wa taifa hilo
mwongo mmoja uliopita, amesema Cuba haihitaji zawadi
zozote kutoka kwa Marekani.
Akijibu pendekezo la Bw Obama kwamba wakati umefika
wa kuunda urafiki na kuzika kwenye kaburi la sahau
masalio ya Vita Baridi bara Amerika, Fidel Castro
amewakumbusha wasomaji kuhusu uvamizi wa Bay of
Pigs uliofanywa na wakimbizi wa Cuba wakisaidiwa na
Marekani mwaka 1961.
Kwa Picha: Ziara ya Obama Cuba
Obama amtaka Castro asiiogope Marekani
Obama na Castro wajibizana Cuba
Amesema maneno ya Obama ya kuhimiza maridhiano ni
sawa na “rojo ya sukari” na kuonya kwamba raia wa
Cuba wanaweza kupata “mshtuko wa moyo”.
Fidel Castro, 89, aliongoza Cuba kuanzia 1959 hadi
2008 alipomkabidhi nduguye madaraka.