Raia wanne wa Uingereza waliokuwa wakipiga picha
ndege nchini Kenya wameamrishwa kulipa faini ya pauni
1,400 ama wahudumie kifungo jela kwa kuchukua picha
hizo katika uwanja wa ndege jijini Nairobi kinyume cha
sheria.
Wanne hao kutoka Manchester nchini Uingereza
walipatikana wakichukua picha hizo katika uwanja wa
Wilson jijini Nairobi na wamekuwa wakizuiliwa kwa zaidi
ya juma moja.
Wanaendelea kuzuiliwa na polisi hadi faini hiyo
itakapolipwa.
Watu hao wanasema kuwa maafisa katika uwanja huo
wa ndege waliwapatia ruhusa kufanya hivyo.
Lakini walizua tatizo la kiusalama walipopatikana katika
baa ya uwanja huo wa ndege.
Baadaye walikiri mashtaka mawili ya kuingia na kupiga
picha ndege bila ruhusa shtaka lililo na faini ya pauni
700 kila mmoja wao.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 7, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 7,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Mag...
2 hours ago