Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, March 16, 2016

Trump asema huenda fujo zikazuka Marekani

Chanzo cha habari bbc swahili
Mfanyabiashara tajiri Marekani Donald Trump, amesema
anafikiri kutatokea fujo iwapo ataongoza kwa wajumbe
kisha chama chake cha Republican kitakosa
kumuidhinisha awanie urais.
Bw Trump alishinda mchujo katika majimbo matatu
zaidi, likiwemo jimbo la Florida mnamo Jumanne,
ingawa alishindwa katika jimbo jingine muhimu la Ohio.
Hatua yake ya kushindwa Ohio huenda ikawawezesha
wahafidhina wadhibiti wa chama cha Republican, ambao
hawajafurahishwa na mtazamo wake, kumpendekeza
mgombea mwingine kwenye mkutano mkuu wa
kuidhinisha wagombea Julai.
Hayo yakijiri, Bw Trump amesema hatashiriki mdahalo
katika runinga ya Fox News wiki ijayo akisema
ametoshena na midahalo.
Katika chama cha Democratic, Hillary Clinton
ameimarisha uongozi wake na kumshinda mpinzani wake
wa pekee Bernie Sanders katika majimbo manne
yaliyofanya mchujo Jumanne.